Bishop Hiluka
JF-Expert Member
- Aug 12, 2011
- 7,147
- 14,699
Tumekuwa tukiaminishwa kuwa uchumi wa nchi za Afrika unaendelea kuwa imara; ukuaji halisi unaongezeka, ikiashiria uwepo wa sera madhubuti za uchumi jumla, maendeleo mazuri katika maboresho ya miundo (hususan katika uboreshaji wa miundombinu), na mifumo ya sera nzuri na madhubuti kiujumla. Inawezekana, lakini kwa hii picha hapa chini, eti hizi nchi 10 ndiyo zina uchumi mkubwa Afrika na zinashikilia asilimia 72.19 ya GDP ya Afrika, basi bado tuna safari ndefu.