Nchi 10 kati ya 54 za Afrika na 72.19% ya GDP, bado tuna safari ndefu

Nchi 10 kati ya 54 za Afrika na 72.19% ya GDP, bado tuna safari ndefu

Natamani kusema ukweli kuhusu hizo takwimu lakini naona Manyang'au akina MK254 yatazidi kutukoga! Anyway, labda niseme hivi... Nyang'au lolote litakalojiona ndo lenyewe kwa post yangu hii, basi huyo ni demu wangu in advance 🤣🤣!

Awali ya yote, nitamke wazi hizo takwimu zinasikitisha lakini ndo uhalisia wenyewe. Kwa upande mwingine, nikijikita Kusini mwa Jangwa la Sahara, I must pay my respect to Kenya. Modern Economy ndiyo imeiweka Kenya hapo ilipo, na naweza kuthubutu kusema ndio the best economy in South of Sahara if not the whole of Africa! WHY?

Nigeria is rich in oil and gas! South Africa is rich in minerals and a bunch of Wazungu! Take away gas and oil from Nigeria, and take away minerals and a bunch of Wazungu from South Africa, the net outcome will top Kenya above them all.

Of course, hata Kenya kuna Wazungu wa kutosha but native Kenyans contribution is still very significant.

Hapo juu nimeona mawazo ya tangu enzi za ujima yakitolewa na Los técnicos kwamba eti madini na gas haviozi!

Hayo ni mawazo ya ujima na ni mawazo yasiyo na maana yoyote kwenye karne hii ya watu kushinda maabara kutafuta mbadala wa kila kitu!!

Miongo kadhaa iliyopita mkonge lilikuwa ni zao ambalo liliingizia Tanzania millions of dollar lakini leo hii mkonge upo kaburini kwa sababu watu wamepata alternative!!

Leo hii ni duniani kuna Space X ya Elon Musk na Blue Origin ya Jeff Bezos, na yote haya yakiashiria Mars Colonization kwavile wenye akili zao wanaamini huko kunaweza kuwa na hazina kubwa ya raslimali kama vile nishati na madini!!

Vision ya Blue Origin kwa mfano, inasema:-
Blue's vision is a future where millions of people are living and working in space. In order to preserve Earth, our home, for our grandchildren’s grandchildren, we must go to space to tap its unlimited resources and energy. If we can lower the cost of access to space with reusable launch vehicles, we can all enable this dynamic future for humanity.
Sasa watu endeleeni na mawazo yenu ya ujima ya kwamba mafuta na madini haviozi hadi mnapokuja kushituka watu wanasafirisha raslimali hizo hizo kutoka sayari nyingine kuja duniani!!!!

Haya mawazo yetu ya "No Hurry in Africa" yametulemaza sana, na inasikitisha hadi kesho bado watu wanaendelea kulemazwa na mawazo waliyotoa akina Nyerere miongo kadhaa iliyopita!!!

Na ni mawazo haya haya ya "madini na mafuta haviozi" ndiyo yaliyofanya consortium iliyotaka kujenga Gas Processing Plant pale Lindi igeukie Mozambique, hadi tutakapokuja kuona "now it's time" tayari Mozambique ishabeba soko la mafuta na gas!

Yaani badala ya kufikiria ni namna gani tunaweza kutumia raslimali tulizonazo at our advantage, bado tunaamini zikae tu, haviozi hivyo!

Na tutaendelea kuimba haziozi hadi tutakapokuja kushitushwa na maendeleo ya kiteknolojia kwamba, Wanasayansi kutoka nchi X hatimae wamegundua jinsi ya kugeuza available nitrogen which's 78% of air to natural gas or any other form of energy!

Wakati wa Mwalimu, ningemwelewa sana kwa sababu hata wasomi hatukuwa nao, lakini dunia ya leo kuwa na mawazo hayo hayo ni namna tu ya ku-justify our failure ya namna gani tunaweza kutumia raslimali zetu kwa faida!!
 
Tumekuwa tukiaminishwa kuwa uchumi wa nchi za Afrika unaendelea kuwa imara; ukuaji halisi unaongezeka, ikiashiria uwepo wa sera madhubuti za uchumi jumla, maendeleo mazuri katika maboresho ya miundo (hususan katika uboreshaji wa miundombinu), na mifumo ya sera nzuri na madhubuti kiujumla. Inawezekana, lakini kwa hii picha hapa chini, eti hizi nchi 10 ndiyo zina uchumi mkubwa Afrika na zinashikilia asilimia 72.19 ya GDP ya Afrika, basi bado tuna safari ndefu.

Ghana ni Masikini wa kutupwa ndio tupo nao sawa!
 
Chige,

Kwanza nianze kwa kusema Mimi sio demu wako 😂😂 but you have point, tukizidi hivi tutajipata kuwa tunanunua tu ba kufaidi Nchi zingine lazima tujishikie vipande vya Mars na Sayari zingine tufaidi madini na nishati.
 
Kimondo watakimaliza lakini sisi tutakuwa na reserve kwa vizazi vyetu "thats how resource sharing operates" ni ujinga kumaliza kila kitu kwa hofu ya ugunduzi mwingine outerspace.

Na huwezi jua, huenda ikawa ni gold variety isiyofikia thamani ya hii ya Africa.

Ni ujinga kukaa unaliwa ukisubiria iko siku na wewe utafaidi, tumia ulicho nacho kwa sasa kuboresha maisha ya kesho.
 
Ni ujinga kukaa unaliwa ukisubiria iko siku na wewe utafaidi, tumia ulicho nacho kwa sasa kuboresha maisha ya kesho.
Sio hasara if we serve for our future intelligent generation to come.
 
Tanzania ina ukubwa wa eneo la kilometa za mraba 947,303 na populations ya 59,734,218

Kenya ina ukubwa wa eneo la kilomita za mraba 580,367 na populations ya 47,564,296 (sensa 2019)

Hadi hapo tunaona ni nani anazaliana sana na ukumbuke Tz ni kubwa karibu mara mbili ya Ke.

Next time acha kuandika ujinga.
Wakenya ni wajinga wanasema tunazaliana sana wakati wao ndio wengi na wana eneo dogo.
 
Hehehehe!! Kweli ni aibu, hili bara sijui nani kaliroga, maana full umaskini na shithole kote ila wabishi kupita maelezo, unakuta mataifa yenyewe yana raslimali na madini ya kumwaga lakini kitakwimu yanatia huruma.
Yaani ukichukua figures za bara zima la afrika ukatafuta share yake globally unakuta Africa economy share inaanza na 0.0000000005%, 😆 😆 😆 😆 .Kwa Afria kazi ipo
 
South korea peke yake tu ina $1tril.

hiyo ni sawa na mchi zote za africa combined.
daa inasikitisha sana but sijui hawa wamefanyaje hadi wakaweza maana nchi hii ilipigana vita na imekuwa na historia ya mapinduzi kwa miongo mingi kama huku Africa lakini hatimaye wakafaulu,tujifunze walifanyaje na sisi tunakwama wapi?
 
Ukiangalia sana sana nchi waliojizalia wengi kama panya i.e Nigeria, Tanzania na Ethiopia, wananchi wao wanateseka sana ila Ethiopia sijaona ikiwa na madini ya maana kama Nigeria na Tanzania ambao wananchi wake wanaishi kama mandondocha.
Tzn na Nigeria mnazitaja sana lakini hapa Africa kuna nchi zenye utajiri wa madini na ardhi nzuri zaidi ya hizi 2,nchi kama Angola,Mozambique,South Sudan na DRC zina kila kitu kuanzia madini,ardhi yenye rutuba,misitu na mvua za uhakika lakini hali zao ni nafuu hata Tanzania
 
Kwa Afrika ni kawaida tu, maana kwa Tanzania watu ni wengi ila eneo la nchi ni kubwa sana na sehemu nyingine hapajaguswa kabisa. Shida ya hizi takwimu unakuta kuna nchi nyingine zinafanya sensa feki na kuficha idadi ya watu ili zionekane vizuri kwenye makaratasi ila kiuhalisia wanazaana kuliko hata panya. Hii lockdown ime onesha jinsi nchi zinavyozaliana hovyo hovyo hapa Afrika.
Kusema ukweli ongezeko la watu kwa nchi za EAC ni kubwa sana yaani tunaitafuta hiyo Nigeria..Kwa eneo niliko huku Tzn yaani kila mwezi nashuhudia watoto wabnaozaliwa ni wengi sana yaani ukipita mahospital labour rooms zimflock ,mbaya zaidi wanao zaa sana ni watu maskini na hawana uhakika wa maisha.
Hii ni fursa kwa kuwekeza kwenye sekta ya uzalishaji chakula na consumer goods za kawaida kama sabuni,mafuta na makazi ila tunakoelekea kutakuja kuwa na magenge ya vibaka sana
 
Inashangaza sana: Mwalimu Nyerere ali-serve kwa ajili yetu ili tukishasoma na kuelimika tuvitumie, eti na sisi leo tuna-serve for our future intelligent generation to come! Nadhani kuna mahali tumekosea.
Yaani huu ni ukweli,haya madini nk yatakuja kutudodea maana walioyagundua na wanaoyatumia ni wazungu wakigundua vingine itakuwa hasara.Toka nzaliwa nasikiaga mara kuna madini ya chuma liganga/mchuchuma na magadi soda engaruka tani zakutosha na process za uwekezaji zinaendelea inamaana huwa hazikamiliki yaanze kuvunwa? Tunatakiwa kutumia rasilimali zilizopo kuwaandalia mazingira ya ushindani wa zama zijazo watoto wetu
Hii ya kusema hayaozi watatumia wajao itakuja kututokea puani kama ambavyo havitunufaishi sasa ndivyo haitawanufaisha wajao kwa vile hakuna tunachofanya kuwajengea uweo kwa kutumia rasilimali zilizopo.Hakuna ajuaye ya kesho..watu washaanza kurusha puto ndio zinasambaza intanet nk mambo ya minara ndo inapotea hivyo
 
Kwa Tanzania population bado iko chini sana ukilinganisha na ukubwa wa eneo la nchi. Acha watu wazaliane, zipo huduma bora za afya hadi vijijini, kuna umeme na maji, kuna barabara za kufikisha mazao yao sokoni, kuna maeneo makubwa ya kilimo na kuna uzalishaji mkubwa hadi surplus. Sasa utasemaje ni masikini hao? Unajua maana ya masikini?
 
Yaani ukichukua figures za bara zima la afrika ukatafuta share yake globally unakuta Africa economy share inaanza na 0.0000000005%, [emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji38] .Kwa Afria kazi ipo
....
global-wealth-by-country-2019-v2.jpg
 
Back
Top Bottom