Narudia... ACHA POROJO!!
Na kwa mara nyingine nasisitiza hili taifa lipo hapa kwa ajili ya watu aina yako ambao hadi karne ya 21 bado wanalia lia kuhusu athari za wakoloni!!
And I repeat, KE kuwa na viwanda vingi hakukufanya Tanzania isiwe na viwanda!! Na ni kutokana na ukweli huo ndio maana hata Mwalimu alijenga viwanda vingi tu hata kabla jumuiya haijavunjika!!
An objective question lingekuwa ni kwanini basi viwanda hivyo vya Mwalimu havikuleta productivity iliyotarajiwa ingawaje jibu linafahamika!!!
Ni aibu miaka 59 baada ya uhuru, na miaka almost 40 tangu kuvunjika kwa EAC ya mwanzo halafu bado unadai eti KE ipo hapo kwa ajili ya Mkoloni alimwachia viwanda, na eti kwa sababu alichukua ndege za EAC!
Tanzania ina ardhi ya kutosha kuliko KE! Tanzania tuna raslimali nyingi kuliko KE! Tuna ukanda mrefu wa bahari kuliko KE! Tuna maziwa na mito mingi kuliko KE! Tuna mbuga nyingi za wanyama kuliko KE! Almost kila kitu tunacho kwa wingi kuliko KE halafu bado leo hii unazungumzia KE ipo hapo kwa ajili ya viwanda vya wakoloni wakati raslimali tulizonazo zinaweza kufanya makubwa kuliko yaliyofanywa na hivyo viwanda vya kikoloni!!
Nimekuuliza kama KE ipo hapo kwa ajili ya viwanda vya mkoloni, Ethiopia liyokuwa juu yetu ipo hapo kutokana na viwanda vilivyoachwa na nani?! JIBU HILO SWALI!!
Pili, nimekuuliza viwanda ambavyo vilijengwa na Nyerere vipo wapi?! Unataka kusema vilikosa effeciency kwa sababu ya viwanda vya mkoloni Mwingereza alivyoacha Kenya? AGAIN, JIBU HILO SWALI!!
Kila anayetaka kutumia ubongo wake sawa sawa anafahamu uchumi wa Tanzania mosi, ulivurugwa na ujamaa na pili, ulivurugwa baada ya nchi kuingia vitani Uganda! Hapo tena nimekuuliza; ni KE au wakoloni ndo walitufanya kuingia vitani Uganda?! Hapa pia, badala ya kuendelea kujiliza liza na historia, JIBU HILO SWALI!
Tanzania tulikuwa na viwanda kibao vya nguo... unataka kusema hivi vilikufa kwa sababu ya KE kuwa na viwanda vya kikoloni?!
Vile viwanda ambavyo vilikuwa Morogoro na Mwanza unataka kusema vilikufa kwa ajili ya viwanda vya wakoloni vilivyoachwa KE?
Pale Arusha kulikuwa na General Tyre East Africa! Unataka kusema kile kiwanda kilikufa kwa ajili ya viwanda vya vikoloni vilivyokuwa vimeachwa KE?
Pale Kurasini kulikuwa na kiwanda cha kusindika samaki... unataka kusema kilikufa kwa ajili ya viwanda vya kikoloni vilivyoachwa KE?! Au unataka kusema kilikufa kwa sababu KE alikuwa anahodhi manufacturing?!
National Milling iliuawa na viwanda vya KE?! RTCs ambazo zilienea kote Tanzania ziliuawa na viwanda vya KE?!
NImekupa mfano unaoweza kueleweka hata na mtoto wa darasa la pili kwamba, ingawaje Tanzania ndo watumiaji wakubwa wa Kiswahili, lakini KE ndo wana-take advantage zaidi ya Kiswahili kuliko Watanzania, to the point majority of Swahili sources online ni za Wakenya!!
Je, hilo nalo ni kwa sababu ya Wakoloni kuwekeza KE?!
Kisha unadai:
Hivi unajua unachoongea wewe?! Unaweza kutaja orodha ya viwanda ambavyo vilijengwa miaka ya 70 wewe?! How come tuanze kupanua sekta ya viwanda hivi sasa wakati tulikuwa na viwanda vya kumwaga miaka ya 70?! Viko wapi hivyo viwanda?
According to
African Business Magazine, Top 5 Banks in East Africa are Kenyan Commercial Bank, Barclays Bank (KE), Equity Bank (KE), Standard Chartered Bank (KE) na Cooperative Bank (KE)!
Sasa ulitarajia Standard Bank (TZ) na Barclays Bank (TZ) ziwepo kwenye hiyo orodha wakati tuliamua uchumi wetu kuuweka chini ya dola, na matokeo yake benki kama Standard Chartered Bank na Barclays zikataifishwa na kuundwa NBC ambayo na yenyewe tulishindwa kuiendesha!!??
And to be honest, hili jukwaa huwa nalikwepa sana kwa sababu najua nikikutana na watu aina yako, halafu mtu akaamua kueleza uhalisia, itakuwa tunajivua nguo wenyewe!!
But what else should I expect kutoka kwa mtu ambae, generally speaking, 90% ya post zake ni Ligi ya KE vs TZ?! Mbaya zaidi, hata kujenga hoja za kubadilisha nyekundu kuwa damu ya mzee, uwezo huo hauna!!!
Hoja zako zisizo na kichwa wala miguu zitasababisha nifanye kile kile ambacho huwa najizuia kukifanya kwenye hili jukwaa manake mtu ukielezea uhalisia inakuwa tunajivua nguo wenyewe!!!
Tena usini-quote manake hizi posts itabidi nizi-delete manake posts hizi hizi siku za usoni naogopa zitanisuta wakati nahangaika kuonesha KE si lolote si chochote mbele ya TZ ingawaje ukweli ni kwamba wametuzidi!!
Tena with due respect, Mkuu
Bishop Hiluka posts kama hizi ingekuwa unaziweka kule kule kwetu ili watu tujadili kwa uhuru manake hapa kama mtu ukiamua kuweka pembeni ligi ya TZ vs KE itakuwa tunajivua nguo wenyewe tu!