figganigga
Platinum Member
- Oct 17, 2010
- 28,132
- 64,416
Nafasi ya amani Afrika
Chanzo cha picha,ABI
Kwa mujibu wa Global Peace Index 2026, Tanzania ipo katika nafasi ya 17 barani Afrika kwa kiwango cha amani, huku ikiwa ya 98 duniani. Inazidiwa hadi na Zambia
MY TAKE
Kila siku wanadai eti wanalinda amani. Wanalindaje amani ambayo haipo?
Wanalinda Ulaji wao. Wanajua watu wakiwa wanahoji watawanyang'anya tonge mdomoni. Wamekula wakavimbiwa hela za walipa kodi hadi wanatamani watu wahamie Burundi kisa wanaohoji matumizi ya kodi zao.
Tanzania haipo kwenye Nchi kumi zenye amani Afrika.
Je, Samia na Mwigulu wanalinda kwa wivu mkubwa amani gani?
Kwa ufupi mumetuharibia amani ya Nchi kwa Utekaji, kuua watu wasio na hatia na kupoteza watu.
Hii ni aibu kwa Samia Suluhu na genge lake linalodai Tanzania kisiwa cha amani. Sasa ni kisiwa cha damu za watu
