The Assassin
JF-Expert Member
- Oct 30, 2018
- 4,942
- 20,077
Juzi tuliambiwa gharama za safari za rais za kitaifa na kimataifa zinagharamiwa na wafanyabishara ambao hawatajwi majina.
Katika akili ya kawaida, kama wafanyabishara wanagharamia safari za mkuu wa nchi nje ya nchi na ndani ya nchi maana yake tayari rais ameshakuwa compromised na wafanyabishara. Hivyo wafanyabishara wanafanya vile wanavyotaka.
Mwalimu Nyerere aliwahi kuonya mkuu wa nchi kuwekwa mfukoni na watu kadhaa ama kikundi flani cha watu ambao wanaweza kumpa maelezo na kumtuma cha kufanya.
Hali hii imejitokeza mbele ya macho yetu. Rais wetu anafadhiliwa na kikundi flani cha watu ambao wanamuelekeza cha kufanya kwani tayari kikundi hicho kinafadhili shughuli za rais na shughuli za serikali.
Kwa msingi huo, ndio maana unaona wafanyabishara wanajiamulia kupandisha bei ya mafuta ambayo yalinunuliwa kwa bei ya chini na hakuna kitu Serikali itawafanya.
Msukuma ameshangaa mafuta yaliyonunuliwa mwezi Februari kupanda bei ghafla sawa na mafuta yanayouzwa leo kwenye soko la Dunia.
Tukubaliane kwamba kaama nchi tumepigwa na kitu kizito kichwani. Mkuu wetu wa nchi yuko mifukoni kwa watu.