Nchi hii, kiini cha kila tatizo tulilo nalo inaonekana ni katiba mbovu; mlio kwenye system, naomba mtujuze, inabadilishwa lini?

Nchi hii, kiini cha kila tatizo tulilo nalo inaonekana ni katiba mbovu; mlio kwenye system, naomba mtujuze, inabadilishwa lini?

Katika haiji kwa sababu mnaisingizia.

Tatizo sio katiba hata kidogo,watu sio kwamba tutafute kiini cha tatizo bali tutafute kiini halisi cha tatizo,ishu sio katiba ishu ni watu wanaofuata katiba hiyo.

Katiba sio ishu kabisa.

Katiba ingefuatwa wale wabunge 19 waasingekuwa bungeni kwa maana katika iliweka taratibu nzuri tu ila shida watu wanaosimamia wameamua kuipuuza.

Sasa kwa ishu kama hii hautakiwi kuilalamikia katiba,walalamikiwe watu wanaosimamia hizo katiba
Katiba haina meno itaachaje kupuuzwa?.Katiba ina kingia kifua makosa ya watu itaachaje kupuuzwa.katiba inatoa mamlaka makubwa kwa mtu itaachaje kupuuzwa?.
 
Katiba inabidi ipatikane haraka tuweke wasomi na mtu akitaka kugombea Ubunge awe na degrees kuongozwa na la 7 ndio imefanya elimu yetu inadharauliwa
 
Katiba haina meno itaachaje kupuuzwa?.Katiba ina kingia kifua makosa ya watu itaachaje kupuuzwa.katiba inatoa mamlaka makubwa kwa mtu itaachaje kupuuzwa?.
Ni kweli kabisa, katiba inamuhakikishia mtu usalama wake awapo madarakani na hata akitoka madarakani, haijalishi kafanya nini, kwahiyo hata akipuuza au kuvunja katiba, katiba hiyo hiyo imempa unconditional protection, ataachaje kuipuuza?! Tunataka katiba mpya!
 
Katika haiji kwa sababu mnaisingizia.

Tatizo sio katiba hata kidogo,watu sio kwamba tutafute kiini cha tatizo bali tutafute kiini halisi cha tatizo,ishu sio katiba ishu ni watu wanaofuata katiba hiyo.

Katiba sio ishu kabisa.

Katiba ingefuatwa wale wabunge 19 waasingekuwa bungeni kwa maana katika iliweka taratibu nzuri tu ila shida watu wanaosimamia wameamua kuipuuza.

Sasa kwa ishu kama hii hautakiwi kuilalamikia katiba,walalamikiwe watu wanaosimamia hizo katiba
Hao watu watalalamikiwa wapi? Ikiwa speaker wa bunge amepewa kinga,hivyo hawezi kushtakiwa,ikiwa mahakama haipo huru..majudge wanateuliwa na Rais..hii nchi basi tu..labda Mungu aingilie kati siku moja.
 
hoja zangu tata kidogo unisamehe..

umesema nchi ina wapuuzi wengi sana, sasa watawala wapumbavu na wananchi wapuuzi wanawezaje kutuzidi akili... au wao ni wengi au sisi ni wapuuzi na wapumbavu zaidi yao?
tatizo ni pale wapumbavu wanapokuwa wengi wanaweza kumchagua raisi wao kipumbavu na wakaelewana ila we usiye mpumbavu usiwaelewe tanzania wapumbavu ndio wengi ilikuwabadili hnahtajika nguvu si ya kibinadamu
 
Taifa linahitaji Kiongozi imara atakayenyoosha watu na kuwaweka kwenye mstari then kupitia kiongozi huyo huyo Taifa ndio linaweza kufanya setup ya hayo yoote..

Leo hii unahitaki upate Katiba bora na tume huru kutokea CCM na watu wake walewale waliotapakaa kila mahala.....Leo hii CCM inaweza kukupa Katiba mpya lakini ikawa na limitations zilezile zenye ulinzi kwao na maslahi kidogo kwa wananchi....
Sasa mkuu pendekezo lako ni nini???.
Ok tuseme kiongozi ndio mwarubaini.... kiongozi imara tunampataje?? Bila katiba Mpya
Mwarubaini ya matatizo yote haya ni Katiba mpya na ni kikwazo kikubwa kwa CCM,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu ndio mana nasemaga hii nchi ina wapuuz wengi...sheria za hii nchii hazipo sawa na wao hawataki kurekebisha sababu wanajua watang'oka, sisemi kwamba mimi ni genious ila wao ni wapumbavu na upumbavu wao wameudhihirisha hadharani na wote tunajua hilo, mkuu unataka kuwatetea ?
Mkuu wewe, unaijua wajibu wako. Effectively je umefanya nini??? Kuibadilisha jamii iliyo kunzunguka kujua wajibu lao kwa serikali..
Au unapga kelele kwenye shimo lenye jiza tororo...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kiuhalisia ni vyema kila kiongozi aliye madarakani akawekewa guidance ya namna ya kuendesha serikali na muongozo huo uwepo kwenye katiba, isiwe utashi au mapenzi yake binafsi, bali katiba iseme hivyo na awajibishwe endapo hatoifuata.

Mfano leo ukaniambia kwamba tunakupa madaraka fulani, na haijalishi utakalofanya, hakuna anaeweza kukushtaki uwapo madarakani au hata ukitoka, sasa hapo mimi nina tofauti gani na ‘Mungu’? Hivi ni nini kitanifanya niogooe kulihujumu taifa? Mfano nikaamua kwenda kukopa dollor bilioni 3 halafu nikaemda kujenga nyimba ya dhahabu shambani kwangu, mtanifanya nini?

Na ukija kuchunguza udhaifu mwingi na madudu mengi yametokana na katiba kushindwa kuwabana na kuwawajibisha ipasavyo wahisika, inabaki kupiga kelele na kulialia hovyo majukwaani kama anavyofanya Ndugai, wakati kiuhalisia muhusika anaruhusiwa kikatiba kufanya hivyo.

Mlio kwenye system, katiba mpya tunaipata lini? Au ndio tusubiri kupigwa mnada kama ng’ombe sokoni?!
Kenya,South Africa,Ghana nk kuna Katiba mpya,je imekuwa muarobaini wa umaskini?

Kwamba Kenya au Ghana inaizidi Egypt kwa maendeleo maana huko hakuna cha Katiba mpya.Ujinga mzigo.
 
Kenya,South Africa,Ghana nk kuna Katiba mpya,je imekuwa muarobaini wa umaskini?

Kwamba Kenya au Ghana inaizidi Egypt kwa maendeleo maana huko hakuna cha Katiba mpya.Ujinga mzigo.
Suala sio katiba mpya tu, bali katiba mpya yenye maboresho sahihi ili kutibu mianya ya udhaifu iliyopo sasa
 
Naweza kuandika kitabu kizima, nikupe mfano, mtu anapohakikishiwa usalama wa kutowajibishwa akifanyanlolote lile akiwa madarakani au hata akitoka madarakani, nini kitamfanya aogope kulihujuma taifa? Huo ni mfano wa kinachotitaji kirekebishwa.
Mbona hata rasimu ya Warioba imeweka masharti ya kutoshitakiwa viongozi wakuu?
 
Kiuhalisia ni vyema kila kiongozi aliye madarakani akawekewa guidance ya namna ya kuendesha serikali na muongozo huo uwepo kwenye katiba, isiwe utashi au mapenzi yake binafsi, bali katiba iseme hivyo na awajibishwe endapo hatoifuata.

Mfano leo ukaniambia kwamba tunakupa madaraka fulani, na haijalishi utakalofanya, hakuna anaeweza kukushtaki uwapo madarakani au hata ukitoka, sasa hapo mimi nina tofauti gani na ‘Mungu’? Hivi ni nini kitanifanya niogooe kulihujumu taifa? Mfano nikaamua kwenda kukopa dollor bilioni 3 halafu nikaemda kujenga nyimba ya dhahabu shambani kwangu, mtanifanya nini?

Na ukija kuchunguza udhaifu mwingi na madudu mengi yametokana na katiba kushindwa kuwabana na kuwawajibisha ipasavyo wahisika, inabaki kupiga kelele na kulialia hovyo majukwaani kama anavyofanya Ndugai, wakati kiuhalisia muhusika anaruhusiwa kikatiba kufanya hivyo.

Mlio kwenye system, katiba mpya tunaipata lini? Au ndio tusubiri kupigwa mnada kama ng’ombe sokoni?!
Lazima tuidai na kila mtu awajibishwe kwa makosa ake
 
Back
Top Bottom