Nchi hii, kiini cha kila tatizo tulilo nalo inaonekana ni katiba mbovu; mlio kwenye system, naomba mtujuze, inabadilishwa lini?

Nchi hii, kiini cha kila tatizo tulilo nalo inaonekana ni katiba mbovu; mlio kwenye system, naomba mtujuze, inabadilishwa lini?

Naweza kuandika kitabu kizima, nikupe mfano, mtu anapohakikishiwa usalama wa kutowajibishwa akifanyanlolote lile akiwa madarakani au hata akitoka madarakani, nini kitamfanya aogope kulihujuma taifa? Huo ni mfano wa kinachohitaji kurekebishwa.
NI hatari sn ndiyo maana wanachezea pesa za umma
 
Kwa mwafrika hata umuweke katiba iliyotoka mbinguni,mambo ni ni yale yale
Nafikiri!tatizo letu linajulikana

Ova
 
Hata ije katiba ya huko kwa malkia maisha yetu ni yetu wenyewe, ukifeli una feli mazima.
Kwa katiba hii tu tuliyo nayo kuna mambo kibao yanakiukwa na wanayamezea
Hata hii wakisema waiweke hali itakuwa ile ile

Ova
 
Kwa katiba hii tu tuliyo nayo kuna mambo kibao yanakiukwa na wanayamezea
Hata hii wakisema waiweke hali itakuwa ile ile

Ova
Yanamezewa sababu katiba yenyewe inawapa ulinzi wahusika, kwahiyo katiba yenyewe inawalinda wanaoikiuka, ndio maana inabidi irekebishwe
 
Mkzuu wewe, unalijua wajibu wako. Effectively je umefanya nini??? Kuibadilisha jamii iliyo kunzunguka kujua wajibu lao kwa serikali..
Au unapga kelele kwenye shimo lenye jiza tororo...

Sent using Jamii Forums mobile app
Okay nimewaelimisha na hili jambo ni endelevu mkuu, na hii elimu tunawapa ni kama damage control tu sababu the damage is so huge to the extent that, sometimes people are left in dilema, mfano "the covid saga ", serikali iliposema hakuna korona tz na chanjo hazifai ilhali watu wanakufa na korona, kuna wakati kusema corona ilikuwa kosa la jinai ila chakushangaza serikali ile ile sasa(baada ya Magu kurest) inasema chanjo ni nzuri na inafaa na corona ipo WTF is that? Yan mtu mmoja alikuwa kawashikia mawazo watu wote hawa ?, chanjo zipo ila watu hawachanji unafikir kwanini ?

Mkuu kubali kataa hii nchi ina system mbovu kabisa inahitaji a complete overhaul.. Anyways kusema kwenye media kama hivi sio kupiga kelele kama ulivyosema sababu hata wewe usingejua kitu chochote nnachokisema. Wewe ungekuwa mimi ungefanyaje ?. How do you act to situations like these ? What is your main concern ? Okay umejua jamii naielimisha, what is the way foward ? Umejuaje kama wewe sio jamii yangu ?
 
Sisiemu hawaezi kubadili katiba milele,,hii katiba inawabeba kwa asilimia 100% bila kupepesa...

Ujinga wa wananchi na katiba ndio mtaji wa wanasiasa
 
Katika haiji kwa sababu mnaisingizia.

Tatizo sio katiba hata kidogo,watu sio kwamba tutafute kiini cha tatizo bali tutafute kiini halisi cha tatizo,ishu sio katiba ishu ni watu wanaofuata katiba hiyo.

Katiba sio ishu kabisa.

Katiba ingefuatwa wale wabunge 19 waasingekuwa bungeni kwa maana katika iliweka taratibu nzuri tu ila shida watu wanaosimamia wameamua kuipuuza.

Sasa kwa ishu kama hii hautakiwi kuilalamikia katiba,walalamikiwe watu wanaosimamia hizo katiba
Katiba inahusu. Hujamsoma mleta mada kuhusu accountability?

Jambo lolote kama linamfurahisha rais, hao subordinates wanalifanya hata kama ni kinyume na sheria na katiba ya nchi.

Ulinzi kutoka kwa rais ni mkubwa kuliko ule wa katiba kwasababu rais yuko juu ya sheria za nchi na katiba haimwajibishi kwa lolote lile.
 
Katiba inahusu. Hujamsoma mleta mada kuhusu accountability?

Jambo lolote kama linamfurahisha rais, hao subordinates wanalifanya hata kama ni kinyume na sheria na katiba ya nchi.

Ulinzi kutoka kwa rais ni mkubwa kuliko ule wa katiba kwasababu rais yuko juu ya sheria za nchi na katiba haimwajibishi kwa lolote lile.
Hakika, this has to be adressed
 
Kiuhalisia ni vyema kila kiongozi aliye madarakani akawekewa guidance ya namna ya kuendesha serikali na muongozo huo uwepo kwenye katiba, isiwe utashi au mapenzi yake binafsi, bali katiba iseme hivyo na awajibishwe endapo hatoifuata.

Mfano leo ukaniambia kwamba tunakupa madaraka fulani, na haijalishi utakalofanya, hakuna anaeweza kukushtaki uwapo madarakani au hata ukitoka, sasa hapo mimi nina tofauti gani na ‘Mungu’? Hivi ni nini kitanifanya niogooe kulihujumu taifa? Mfano nikaamua kwenda kukopa dollor bilioni 3 halafu nikaemda kujenga nyimba ya dhahabu shambani kwangu, mtanifanya nini?

Na ukija kuchunguza udhaifu mwingi na madudu mengi yametokana na katiba kushindwa kuwabana na kuwawajibisha ipasavyo wahisika, inabaki kupiga kelele na kulialia hovyo majukwaani kama anavyofanya Ndugai, wakati kiuhalisia muhusika anaruhusiwa kikatiba kufanya hivyo.

Mlio kwenye system, katiba mpya tunaipata lini? Au ndio tusubiri kupigwa mnada kama ng’ombe sokoni?!
Nitoe rai moja tuu, wananchi wasijikite sana na kudai katiba mpya inaonekana viongozi wa CCM wako alergic na neno katiba mpya. Practically hata katiba iliopo ikifinyiwa heavy upgrade (marekebisho ya kimsingi) basi matokeo yake ni sawa na katiba mpya.

Taasisi za kiraia zijikite hapo katika orodha ya mambo ya msingi na kuanza kuyadai kwa njia wanazoona zinafaa.
 
Katiba mpya ni mwiba kwa watawala wa ccm, hawajui inaweza kufika mahali katiba mbovu ikawageuka hata wao wenyewe......muda ni mwalimu mzuri.
Subili Lisu angie ikulu na katiba mbovu ndio wataelewa watajuta
 
Back
Top Bottom