Siasa ni taaluma inayohitaji mtu aisomee apate degree yake na kubobea kabla ya kufanya siasa.
Ni dhamira ovu kuhalalisha au kuziita fitina na figisu za uswahilini zilizoasisiwa na Kikwete na kundi lake kuwa ndio siasa.
Vyama vimepoteza malengo ya kuanzishwa kwake vimebakia kuwa vichaka vya wahuni wanaohujumu rasilimali za umma kujinufaisha huku wakidharau na kuziweka kando mamlaka za Dola na sheria za nchi kando kwa makusudi ili kukidhi haja zao kwa gharama za wananchi.
Wanaoitwa wanasiasa wote kwa sasa na wale watu wazima walioko kwenye siasa hadi leo tunawajua ujana wao na jinsi walivyotumia fursa iliyojitokeza kupindisha mambo ambayo yamaharibika sana na hakuna anayeona aibu.