Nchi iko pagumu sana. Trust me, tunajipa moyo tu

Magufuli ameiacha nchi kwenye hali mbaya sana,anampa mzigo mama Sami kuijenga upya....lile zee lile basi tu!!
 
Kuhusu upigaji uliogusia ni kweli unarudi kwa kasi ya ajabu tiombe tu Mungu soon makontena yataanza tena kupotea kama sindano. Niacheni mie nkapige picha kilimanjaro ninywe na mbege.
 
Kwanini hao wanaojinasibu wazee wa kufoka na kalamu wasinunue mahindi yote kwa bei nzuri kuwatia moyo na kuwaokoa wananchi wake kwa hili dhahama la kushuka kwa bei ya mahindi?
Ndio wamenunua kiasi ila kuna maelfu ya Tani za ziada zimezalishwa hakuna kwa kuyapeleka..

Tungekuwa na uchumi wenye linkage baina ya sekta Hali isingefika hapa..

Ila tahadhari mwakani supply itapungua bei zitapanda msije kuanza kulia Lia tena.
 
Maguful ndiye aliyesababisha Hayo. Tumwombee Mama, tusurudi Kule.
Enzi ya Magu upigaji ulishapungua kama sio kukoma kbs, miradi mikubwa ilikuwabikijengwa kwa kasi na tuliiona, wazembe walikaangwa hadharani, ofisi za umma zilishakuwa sehemu za kutolea huduma zinazostahiki kweli, miundombinu ilijengwa kwa speed but kwa sasa kila kitu ni zzzzzzzzz sio 1 wala mbili yote kimyaa mtu anazurura tu.
 
Saizi hakuna miradi mikubwa? Ujenzi sio wa kasi? Upigaji upi unaweza ubainisha hapa ? Au unaropoka Ili kutoa stress za maisha?

Yule mzalendo wenu aliharibu Sana hii nchi.
 
Piga hesabu ya bulk transport. Sasa gunia 10 unapeleka wapi? Wanachofanya watu ni wanajikusanya wanasafirisha in bulk kwa kulipia usafiri mmoja uliojaa mahindi tu.
We kichwa ngumu, sasa hiyo bulk unahisi ukilipa usafir mil. 1.5 ukigawa kwa gunia unapata bei gani??
Au unalopoka tu.??
 
Lawama zote kwa Awamu ya Tano iliyowafanya wawekezaji na Wafanyabiashara maadui. Leo Kenya wananjaa lakini walishaagiza Mahindi Brazil, wanalima Congo na Zambia unayo ya kutosha. Ya kwetu tutapeleka wapi na hatuna Mifugo ya kuyamaliza
Tuanzishe ufugaji wa kisasa,kuwe na idara maalumu za kuratibu ufugaji na utafutaji wa masoko nje ya nchi .
 
Ndio wamenunua kiasi ila kuna maelfu ya Tani za ziada zimezalishwa hakuna kwa kuyapeleka..

Tungekuwa na uchumi wenye linkage baina ya sekta Hali isingefika hapa..

Ila tahadhari mwakani supply itapungua bei zitapanda msije kuanza kulia Lia tena.
Serikali haina ya kukwepa kuhusu hili,unafikiri serikali ikiamua inashindwa?

Kwanini serikali na viongozi wake wanawahimiza vijana kwenda shambani wajiajiri wakati kuwatafutia masoko shida?

Tantrade na sijui taasisi inaitwa MAZAO mchanganyiko zinafanya nini? Serikali ina taasisi nyingi zinazoshughulikia MASOKO lakini wanakula mishahara tu na bi mkubwa anawaangalia

Serikali ina mkono mrefu na ngumu kukwepa hili mkuu.
 
Utafurahishwa na mambo makuu mawili๐Ÿ˜… 1.Kupigwa kipapai shambani.
2.Kupigwa tozo na bei mbovu sokoni.
Mimi huwa nalima kwa ajili ya chakula ila nikitaka biashara nasoma upepo kama ninunue au laa..

Ila ukinunua ni nafuu kuliko mtu kahangaika mwaka mzima anakuja kuuza 30,000 ..

Tahadhari mwakani mahindi yatapanda wengi watapunguza kulima mwaka huu kwa sababu za bei na mbolea kuwa Juu..

Msije sema hatukuwaambia.
 
Ndio kilimo cha bongo kilivyo, time ambayo utakula hasara ndio time ambayo unatakiwa uongeze nguvu ulime upya!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ