Nchi iko pagumu sana. Trust me, tunajipa moyo tu

Nchi iko pagumu sana. Trust me, tunajipa moyo tu

Kuna kitu kinakula moyo wangu I finally must vent out.

1. Nimevuna gunia 200 baada ya kulima ekari 20 za mahindi nataka kupeleka sokoni bei ya gunia tshs elfu 30, so nitapata million sita nikiuza yote. Kweli jamani this is too much. The leadership is seriously imposing new tax? Mnashindwa kuadress market challenges kwa watu million 45 walioko Shamba? Really????

2. Kuna influx ya vyuo Vya afya now than ever before. Ni mwendo Wa lab technician's, nursing, pharmacy, medical assistance courses etc. Nimeproject in 5 years to come tutakuwa na mrundikano Wa wataalamu Wa afya kuliko kawaida watakaokuwa hawaajiliki. Utapeli utaanza, kila chumba kitakuwa hospital bubu, madawa kuuzwa ovyo nk hii imeshaanza njmeiona somewhere. Afya zetu zitakuwa rehani. Ni kama hakuna sekta nyingine za kutrain serikali na taasisi binafsi zote ziko huko now. Sioni influx ya trainee kwenye lead productive sectors.

3. Ajira hakuna, kila mtu sasa analima masoko hakuna, mbinu za kujenga uchumi unaokuwa sizioni serious. Kuna ahadi tu za kuendelea kujengewa majengo mengi ya huduma mbalimbali za serikali bila kujenga watu Vya kutosha.

4. Nikirudi kwenye mfumuko Wa bei bei za mafuta, visavis gharama za uzalishaji wa mazao tozo barabarani usumbufu wa wakaguzi mazao, matrafiki, nk nk naishiwa hamu kabisa.

5. Ukiwaangalia viongozi concentration haipo kudeal na 80 % ya walipo watz inadeal na vitu very Petty.....

6. Upigaji umerudi kwa kasi ya ajabu. Sasa hivi kila ofisi ya umma hasa hizi nyeti zisizokwepeka deal zinapigwa balaa

My question is....watoto wetu wataikuta Tanzania ya namna gani sijui.

Jamani eeeh sijui kama hii tabu naipata Mimi tu. Kuna majibu hapa

Its soo frustrating.
Magufuli ameiacha nchi kwenye hali mbaya sana,anampa mzigo mama Sami kuijenga upya....lile zee lile basi tu!!
 
Kuhusu upigaji uliogusia ni kweli unarudi kwa kasi ya ajabu tiombe tu Mungu soon makontena yataanza tena kupotea kama sindano. Niacheni mie nkapige picha kilimanjaro ninywe na mbege.
 
Kwanini hao wanaojinasibu wazee wa kufoka na kalamu wasinunue mahindi yote kwa bei nzuri kuwatia moyo na kuwaokoa wananchi wake kwa hili dhahama la kushuka kwa bei ya mahindi?
Ndio wamenunua kiasi ila kuna maelfu ya Tani za ziada zimezalishwa hakuna kwa kuyapeleka..

Tungekuwa na uchumi wenye linkage baina ya sekta Hali isingefika hapa..

Ila tahadhari mwakani supply itapungua bei zitapanda msije kuanza kulia Lia tena.
 
Maguful ndiye aliyesababisha Hayo. Tumwombee Mama, tusurudi Kule.
Enzi ya Magu upigaji ulishapungua kama sio kukoma kbs, miradi mikubwa ilikuwabikijengwa kwa kasi na tuliiona, wazembe walikaangwa hadharani, ofisi za umma zilishakuwa sehemu za kutolea huduma zinazostahiki kweli, miundombinu ilijengwa kwa speed but kwa sasa kila kitu ni zzzzzzzzz sio 1 wala mbili yote kimyaa mtu anazurura tu.
 
Saizi hakuna miradi mikubwa? Ujenzi sio wa kasi? Upigaji upi unaweza ubainisha hapa ? Au unaropoka Ili kutoa stress za maisha?

Yule mzalendo wenu aliharibu Sana hii nchi.
 
Piga hesabu ya bulk transport. Sasa gunia 10 unapeleka wapi? Wanachofanya watu ni wanajikusanya wanasafirisha in bulk kwa kulipia usafiri mmoja uliojaa mahindi tu.
We kichwa ngumu, sasa hiyo bulk unahisi ukilipa usafir mil. 1.5 ukigawa kwa gunia unapata bei gani??
Au unalopoka tu.??
 
Lawama zote kwa Awamu ya Tano iliyowafanya wawekezaji na Wafanyabiashara maadui. Leo Kenya wananjaa lakini walishaagiza Mahindi Brazil, wanalima Congo na Zambia unayo ya kutosha. Ya kwetu tutapeleka wapi na hatuna Mifugo ya kuyamaliza
Tuanzishe ufugaji wa kisasa,kuwe na idara maalumu za kuratibu ufugaji na utafutaji wa masoko nje ya nchi .
 
Ndio wamenunua kiasi ila kuna maelfu ya Tani za ziada zimezalishwa hakuna kwa kuyapeleka..

Tungekuwa na uchumi wenye linkage baina ya sekta Hali isingefika hapa..

Ila tahadhari mwakani supply itapungua bei zitapanda msije kuanza kulia Lia tena.
Serikali haina ya kukwepa kuhusu hili,unafikiri serikali ikiamua inashindwa?

Kwanini serikali na viongozi wake wanawahimiza vijana kwenda shambani wajiajiri wakati kuwatafutia masoko shida?

Tantrade na sijui taasisi inaitwa MAZAO mchanganyiko zinafanya nini? Serikali ina taasisi nyingi zinazoshughulikia MASOKO lakini wanakula mishahara tu na bi mkubwa anawaangalia

Serikali ina mkono mrefu na ngumu kukwepa hili mkuu.
 
Utafurahishwa na mambo makuu mawili😅 1.Kupigwa kipapai shambani.
2.Kupigwa tozo na bei mbovu sokoni.
Mimi huwa nalima kwa ajili ya chakula ila nikitaka biashara nasoma upepo kama ninunue au laa..

Ila ukinunua ni nafuu kuliko mtu kahangaika mwaka mzima anakuja kuuza 30,000 ..

Tahadhari mwakani mahindi yatapanda wengi watapunguza kulima mwaka huu kwa sababu za bei na mbolea kuwa Juu..

Msije sema hatukuwaambia.
 
Ndio kilimo cha bongo kilivyo, time ambayo utakula hasara ndio time ambayo unatakiwa uongeze nguvu ulime upya!
 
Back
Top Bottom