Nchi iko pagumu sana. Trust me, tunajipa moyo tu

Nchi iko pagumu sana. Trust me, tunajipa moyo tu

Sisi tupo hapa anaweza kuja Mchina akafungua kiwanda Rukwa na kuajiri vijana wetu kwa ujira kiduchu. Baada ya miaka mitatu amekua billionaire.
Kulalamika na kulaumu si ndio Kazi ya wabongo,hata hivyo mahindi sio zao kuu la chakula Afrika au Duniani labda chakula cha mifugo
 
Luna kitu kinakula moyo wangu I finally must vent out.

1. Nimevuna gunia 200 baada ya kulima ekari 20 za mahindi nataka kupeleka sokoni bei ya gunia tshs elfu 30, so nitapata million sita nikiuza yote. Kweeeli jamani this is too much. The leadership is seriously imposing new tax? Mnashindwa kuadress market challenges kwa watu million 45 walioko Shamba? Really????

2. Kuna influx ya vyuo Vya afya now than ever before. Ni mwendo Wa lab technician's, nursing, pharmacy, medical assistance courses etc. Nimeproject in 5 years to come tutakuwa na mrundikano Wa wataalamu Wa afya kuliko kawaida watakaokuwa hawaajiliki. Utapeli utaanza, kila chumba kitakuwa hospital bubu, madawa kuuzwa ovyo nk hii imeshaanza njmeiona somewhere. Afya zetu zitakuwa rehani. Ni kama hakuna sekta nyingine za kutrain serikali na taasisi binafsi zote ziko huko now. Sioni influx ya trainee kwenye lead productive sectors.

3. Ajira hakuna, kila mtu sasa analima masoko hakuna, mbinu za kujenga uchumi unaokuwa sizioni serious. Kuna ahadi tu za kuendelea kujengewa majengo mengi ya huduma mbalimbali za serikali bila kujenga watu Vya kutosha.

4. Nikirudi kwenye mfumuko Wa bei bei za mafuta, visavis gharama za uzalishaji wa mazao tozo barabarani usumbufu wa wakaguzi mazao, matrafiki, nk nk naishiwa hamu kabisa.

5. Ukiwaangalia viongozi concentration haipo kudeal na 80 % ya walipo watz inadeal na vitu very Petty.....

6. Upigaji umerudi kwa kasi ya ajabu. Sasa hivi kila ofisi ya umma hasa hizi nyeti zisizokwepeka deal zinapigwa balaa
My question is....watoto wetu wataikuta Tanzania ya namna gani sijui.

Jamani eeeh sijui kama hii tabu naipata Mimi tu. Kuna majibu hapa. Its soo frustrating.
Kweli kabisa hali ya bei ya mazao hasa mahindi ni mbaya sana kwa mkulima, lakini tunapaswa kujiuliza shida ilianzia wapi, nakumbuka soko kubwa la mahindi yetu likikuwa ni nchi ya Kenya, sisi wenyewe tukapiga marufuku kupeleka mahindi Kenya, hali ya zao la mahindi ikaharibika sana, sasa leo tunataka kuona eti tatizo hili limeanza leo, ni kweli? Mleta mada fikiri vizuri, usijisahaulishe, ukute wewe mwenyewe ulishabikia ile ban ya serikali kupeleka mahindi nje ya nchi, tuanze kufikiri namna nzuri ya kurekebisha hii hali
 
Kweli kabisa hali ya bei ya mazao hasa mahindi ni mbaya sana kwa mkulima, lakini tunapaswa kujiuliza shida ilianzia wapi, nakumbuka soko kubwa la mahindi yetu likikuwa ni nchi ya Kenya, sisi wenyewe tukapiga marufuku kupeleka mahindi Kenya, hali ya zao la mahindi ikaharibika sana, sasa leo tunataka kuona eti tatizo hili limeanza leo, ni kweli? Mleta mada fikiri vizuri, usijisahaulishe, ukute wewe mwenyewe ulishabikia ile ban ya serikali kupeleka mahindi nje ya nchi, tuanze kufikiri namna nzuri ya kurekebisha hii hali
Aliwakomesha yule mliyekuwa mnamuita mzalendo
 
Tabia za nchi maskini sana duniani kama Tanzania ni kufikiri kuwa chanzo kikuu cha mapato ya serikali ni wananchi. Ila ikumbukwe kuwa asilimia kubwa ya watanzania ni maskini, hivyo kufanya hivyo ni kuendeleza umaskini. Nchi maskini hutegemea zaidi mapato kutoka kweye sekta ya huduma (service) wakati serikali za nchi tajiri wanapata hadi 90% ya mapato yake kutoka sekta ya viwanda na si huduma.
Tunahitaji akili kubwa kubadili mwelekeo la sivyo tutabaki na serikali maskini, nchi maskini na wananchi maskini. Mwisho wa siku tutagemea misaada, mikopo hadi kuuza nchi. TAFAKARI
Kusema ni rahisi Sana ila kufika huko kuna maumivu ambayo mlio wengi hamtaki
 
Kuna kipindi mahindi na mazao mengine bei ilikuwa juu sana.

Magufuli akaongea kwa ukali sana akasema kama unaona bei iko juu na wewe nenda kalime. Akaendelea kwamba wakulima ikiwezekana pandisheni tena bei, ni wakati wa wakulima nao kufaidi matunda ya kazi yao!

Aisee... Baada ya hii kauli chadema na kina Zitto na yale matahira yaliyokimbia nchi yalimtukana magufuli matusi yote unayoyajua.


Hitimisho:
Watz sisi ni watu wa ajabu sana! Hatujui tunataka nini, ndio maana kila siku nasema ukiwa kiongozi tekeleza wajibu wako ili siku zako za uongozi ziishe umuachie mwingine. Kwamba umeleta impact gani hiyo haikuhusu.
Kujaribu kuwapigania watz ni kujichosha bure.
Namshangaa sana hata Mbowe anapata tabu yote kisa nini? Kwa ajili ya hawa wajinga wa tz? Ambao mada yao kuuu ni simba na yanga?
Ha haaa ...😁😁
Aliyeturoga wa TZ kafa.
Hatujui tunataka nini na tunatokaje kwenye mkwamo huu... maaninah ... maaamaeh😢
 
Hali ni mbaya chief,hata mie naiona,
Tabaka tawala,halina majibu kabisa,hivi kweli kilo ya mahindi iuzwe shilingi 500!huyu mkulima atajenga vipi nyumba,atasomeshaje mtoto chuo kikuu,ataweka vipi akiba ya uzeeni?
Miaka 60 ya uhuru nchi haiwezi kuwahakikishia wakulima bei nzuri ya mazao yao!!
Hii ni shida,sasa hv kila kijana anaenda kwenye kilimo,wakati ilibidi wakulima wawe wachache,vijana wengine wawe kwenye viwanda,hii ni balaa,
Serikali inahangaika kuajiri polisi wengi!!Ili waje wakuze uchumi?!!
Haki ya Mungu,natamani kukimbia hii nchi,kwa vijana ambao hamjawa na familia na huko na Elimu nzuri,tafuta passport,ukiona fulsa nje,sepa fasta
Tabaka tawala ndio wameshusha bei? Unajua kwamba kuna ziada ya Malaki ya Tani ya mahindi nchini?

Acheni kilimo cha mazoea mtakufa maskini
 
Shida serikali imejiingiza kwenye biashara hawawezi ruhusu..huoni wamefungua maghala south sudani na wanafugua kongo na komoro.

Mahindi yakiuzwa nje watapata wapi mahindi ya bure bure ili wakatengeneze faida huko nje ya nchi.
#MaendeleoHayanaChama
Uongo
 
Kuondoa ruzuku kwenye mbolea, kodi kwa zaidi ya tani moja,kupanda kwa bei ya mafuta kunaongeza gharama kwa wakulima ambao ndio Watanzania wengi.

Vipaumbele vyetu ni vipi? Tuko serikalini kumsaidia nani? Kufanya nini?
Uweke ruzuku ya nini kwenye kitu hakina tija? JK alijaribu huu upuuzi ikawa hasara tupu..

Lazima kulima Mazao ya kimkakati ya biashara sio chakula
 
Inconsistency and unpredictability country ndio the United Republic of Tanzania. ..policies. Ukishakuwa na rais, wabunge, madiwani na mawaziri walioingia madarakani kwa rushwa, dhuluma, kwa kutumia vyombo vya dola na kumwaga damu za watu wao wenyewe huku waki promote ubaguzi wa ki vyama, kikanda, kikabila na kidini LAANA inaingia. Watendaji wengine wote RC, DC, RAS, majaji na mahakimu ...wanateuliwa na mtu mwenye mikono iliyo na harufu ya damu mbichi na laana. Kwa hiyo hakuna jema litakalozaliwa. Hawa ni viongozi zao la laana na bahati mbaya mno kila bunge likikaa wanaanza na sala kumkumbusha Mungu uovu wao. Baya zaidi mijadala yao ni ya hovyo mpaka unawaza. Kwa kifupi priority ya viongozi wetu hawa ni Uchaguzi ujao anaoatia wapi fedha, anapatia wapi rushwa, aende wapi apate per diem, amkalishe nani wapi iki chain iwe imara, akwepeje kodi, mshahara uongezekeje nk nk. Suala la mahindi na maisha yenu ni by the way. Poleni maana ni msiba wetu sote. Shida ni VIONGOZI.
Porojo za siasa hazikuzi uchumi,hayo unayoyasema hayana uhusiano na uchumi
 
Mkuu 'kasanga70', umemega menga kwingi mno hadi tonge likawa kubwa kiasi kwamba sio rahisi kulimeza lilivyo, na kulitafuna inakuwa shida!

Mada yako ni muhimu zaidi ya kiasi, na naona tayari unazo kurasa takribani saba hivi. Sijazisoma, lakini nitazisoma zote nione kama mada yako hii imepata michango makini inayostahiri.

Kwa sasa inabidi niseme tu kwamba ni nchi tunayojiendea bila dira maalum. Kila mtu anajipigia kivyake kadri anavyoona inamfaa.

Wakati ninasoma uliyoandika hapo kwenye mada ngumu sana, nikawa nawaza hizo gunia zako za mahindi na kujaribu kuziunganisha na swala lililopo sasa kwenye 'chart' la "Umachinga" kujaribu kuona kama kuna uwezekano wa mahindi yako kwa upande huo pia!

Nakwenda kusoma mada tokea mwanzo kabisa hadi ukurasa huu wa mwisho, nione yaliyochangiwa na wahenga hapa.

Nikupongeze kwa mada muhimu, lakini ngumu.
 
Mafuta ya kula yakipanda bei ni fursa kwako mkulima. Sasa lima alizeti upige pesa. Kuhusu mahindi NFRA wamepewa pesa wayanunue. Tafuta vituo vyao ukauze.
Kuna kituo kimoja cha NFRA Inyala yanaingia malori kwa malori kuingiza mzigo wa mahindi sijui yanatoka wapi sisi wakulima wa maeneo hayo hatuwezi uza hata gunia moja. Ni masoko yao wenyewe kuuza mahindi yao.
 
Yaani nnachojiulizaga hivi magufuli alikuwa anapata wapi hela za kuendeshea nchi kiasi kwamba hata misaada haikuwa tegemezi
 
Kuna kituo kimoja cha NFRA Inyala yanaingia malori kwa malori kuingiza mzigo wa mahindi sijui yanatoka wapi sisi wakulima wa maeneo hayo hatuwezi uza hata gunia moja. Ni masoko yao wenyewe kuuza mahindi yao.
Nimemsikia waziri akisema mtauzia kupitia vyama vya ushirika.
 
Imposing withholding tax kwa mazao kisa kuuza kwa wenye makampuni sijui waliwaza nini, kila nikifikiria hili moyo unaniuma sana, katika mazingira ya pembenei kupandwa na bei za mazao kudorola Leo umwambie mtu akatwe withholding tax si mtaumizana tu, jambo hili linaweza kuchochea bushara zisizo halali za kupeleka nje ya nchi kinyemela

Tax law experts na economist wetu mlifikiriaje kwa jambo hili, Mzee mwigulu liangalie mara 22, uzuri upo humu kiongozi kiukweli maendeleo tunahitaji lakini hawa wazee wetu vijijini tuwahurumie
Yaani katika watu mwigulu ni professional kwenye uchumi lakini sifuri kichwani sio wa kumtegemea
 
Back
Top Bottom