Nchi iko pagumu sana. Trust me, tunajipa moyo tu

Sisi tupo hapa anaweza kuja Mchina akafungua kiwanda Rukwa na kuajiri vijana wetu kwa ujira kiduchu. Baada ya miaka mitatu amekua billionaire.
Kulalamika na kulaumu si ndio Kazi ya wabongo,hata hivyo mahindi sio zao kuu la chakula Afrika au Duniani labda chakula cha mifugo
 
Kweli kabisa hali ya bei ya mazao hasa mahindi ni mbaya sana kwa mkulima, lakini tunapaswa kujiuliza shida ilianzia wapi, nakumbuka soko kubwa la mahindi yetu likikuwa ni nchi ya Kenya, sisi wenyewe tukapiga marufuku kupeleka mahindi Kenya, hali ya zao la mahindi ikaharibika sana, sasa leo tunataka kuona eti tatizo hili limeanza leo, ni kweli? Mleta mada fikiri vizuri, usijisahaulishe, ukute wewe mwenyewe ulishabikia ile ban ya serikali kupeleka mahindi nje ya nchi, tuanze kufikiri namna nzuri ya kurekebisha hii hali
 
Aliwakomesha yule mliyekuwa mnamuita mzalendo
 
Kusema ni rahisi Sana ila kufika huko kuna maumivu ambayo mlio wengi hamtaki
 
Ha haaa ...😁😁
Aliyeturoga wa TZ kafa.
Hatujui tunataka nini na tunatokaje kwenye mkwamo huu... maaninah ... maaamaeh😢
 
Tabaka tawala ndio wameshusha bei? Unajua kwamba kuna ziada ya Malaki ya Tani ya mahindi nchini?

Acheni kilimo cha mazoea mtakufa maskini
 
Shida serikali imejiingiza kwenye biashara hawawezi ruhusu..huoni wamefungua maghala south sudani na wanafugua kongo na komoro.

Mahindi yakiuzwa nje watapata wapi mahindi ya bure bure ili wakatengeneze faida huko nje ya nchi.
#MaendeleoHayanaChama
Uongo
 
Kuondoa ruzuku kwenye mbolea, kodi kwa zaidi ya tani moja,kupanda kwa bei ya mafuta kunaongeza gharama kwa wakulima ambao ndio Watanzania wengi.

Vipaumbele vyetu ni vipi? Tuko serikalini kumsaidia nani? Kufanya nini?
Uweke ruzuku ya nini kwenye kitu hakina tija? JK alijaribu huu upuuzi ikawa hasara tupu..

Lazima kulima Mazao ya kimkakati ya biashara sio chakula
 
Porojo za siasa hazikuzi uchumi,hayo unayoyasema hayana uhusiano na uchumi
 
Mkuu 'kasanga70', umemega menga kwingi mno hadi tonge likawa kubwa kiasi kwamba sio rahisi kulimeza lilivyo, na kulitafuna inakuwa shida!

Mada yako ni muhimu zaidi ya kiasi, na naona tayari unazo kurasa takribani saba hivi. Sijazisoma, lakini nitazisoma zote nione kama mada yako hii imepata michango makini inayostahiri.

Kwa sasa inabidi niseme tu kwamba ni nchi tunayojiendea bila dira maalum. Kila mtu anajipigia kivyake kadri anavyoona inamfaa.

Wakati ninasoma uliyoandika hapo kwenye mada ngumu sana, nikawa nawaza hizo gunia zako za mahindi na kujaribu kuziunganisha na swala lililopo sasa kwenye 'chart' la "Umachinga" kujaribu kuona kama kuna uwezekano wa mahindi yako kwa upande huo pia!

Nakwenda kusoma mada tokea mwanzo kabisa hadi ukurasa huu wa mwisho, nione yaliyochangiwa na wahenga hapa.

Nikupongeze kwa mada muhimu, lakini ngumu.
 
Mafuta ya kula yakipanda bei ni fursa kwako mkulima. Sasa lima alizeti upige pesa. Kuhusu mahindi NFRA wamepewa pesa wayanunue. Tafuta vituo vyao ukauze.
Kuna kituo kimoja cha NFRA Inyala yanaingia malori kwa malori kuingiza mzigo wa mahindi sijui yanatoka wapi sisi wakulima wa maeneo hayo hatuwezi uza hata gunia moja. Ni masoko yao wenyewe kuuza mahindi yao.
 
Yaani nnachojiulizaga hivi magufuli alikuwa anapata wapi hela za kuendeshea nchi kiasi kwamba hata misaada haikuwa tegemezi
 
Kuna kituo kimoja cha NFRA Inyala yanaingia malori kwa malori kuingiza mzigo wa mahindi sijui yanatoka wapi sisi wakulima wa maeneo hayo hatuwezi uza hata gunia moja. Ni masoko yao wenyewe kuuza mahindi yao.
Nimemsikia waziri akisema mtauzia kupitia vyama vya ushirika.
 
Yaani katika watu mwigulu ni professional kwenye uchumi lakini sifuri kichwani sio wa kumtegemea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…