Uchaguzi 2020 Nchi imeamka ikiwa na huzuni kubwa sana, Kwamba wabunge wote Bara 100% wameshinda wa CCM

Uchaguzi 2020 Nchi imeamka ikiwa na huzuni kubwa sana, Kwamba wabunge wote Bara 100% wameshinda wa CCM

Ndugu hakuna cha kushtakiwa wala nini Sheria ya ICC sio kufungua kule moja kwa moja ni lazima shauri lifunguliwe kwenye mahakama ya ndani then itakapofeli kutoa hukumu ndipo ICC inahusika.

Kuitwa ICC ni jambo moja na hukumu ni jambo lingine mpaka hapa mchezo umeisha,utaona mwenyewe.

Na Rais akitangazwa hupingi popote,imeisha hiyoo CCM hoyeee...
-Wewe hujaelewa wapi nimetaja ICC? MIMI nazungumzia taasisi kama EU,WB,USA hao ndiyo wafadhili wetu wakuu watunyime misaada kwa sababu ya kukiuka misingi ya democracy
-ICC wanashitaki wale ambao mfumo wa local courts umeshindwa hence hakuna haja ya exhaustion of local remedy.
 
Sanduku la kura linabebwa mtu anapanda nalo boda boda anatokomea nalo chombo cha habari kinaripoti eti
kituko chatoa mtu akimbia na sanduku la kura!!! Yaani sanduku la kura linaibiwa mchana kweupe then wanasema ni kituko? Badala ya kukemea?
CHADEMA Ni hodari sana kwa kuandika na kucheza movi za kihindi. Poleni sana ila Watanzania wanazijua sana hizo muvi za kihindi
 
Sasa naanza kuona siku mpya za mabadiliko kwa mbali,Lissu na CDM wamefanikiwa kwa zaid ya 90% katika kuileta Tanzania mpya kwa kuifanya dunia kuielewa Tanzania in its true nature-The way it is.Believe me-Mambo mengi yatabadilika kuelekea demokrasia ya kweli ikiwemo sheria kandamiz kuondoka,the biggest looser is gvt and kijani and this election ime propel dearth ya CCM kama chama,Just wait and see aftermath ya hii election and you will prove it.
Ndoto za mchana, kafanye kazi achana na hizo ndoto
 
Hatuwezi kuchagua MBUNGE Mpuuzi na MPUMBAVU kisa tu... Eti ni FAIRNESS..

mbn hamuulizi kuhusu KUPITA bila KUPINGWA ktk MAJIMBO zaidi ya 20+???
 
Huku kwetu Kawe hakuna huzuni, ni full shangwe. Watu tulishajichokea makelele, na kuogelea kwenye maji machafu mitaani kila mvua ikinyesha. Tunataka barabara za lami mitaani na kukomeshwa kwa mafuriko. Na mbunge anayeonekana live jimboni, sio kupitia luninga akiwa kwenye migomo au mahakamani.
 
CHADEMA Ni hodari sana kwa kuandika na kucheza movi za kihindi. Poleni sana ila Watanzania wanazijua sana hizo muvi za kihindi
kama ni movie ilikuwaje wasikamatwe?
kama tu wengine wanaopita karibu na kituo wanakamatwa bila sababu za msingi imekuwaje mpaka OCD anakimbia na sanduku? na yenyewe ni movie sio?
 
Fafanua kidogo, kura tupige wenyewe ,matokeo yatoke kama tulivyoamua, huzuni inatoka wapi?! Acha wavune walichopanda, waliamua kuwa viwanda vya matusi, malalamiko, kupinga kila kitu,kukosa sera na mikakati mbadala.
 
Pwani ina nini cha maana au ina kipi cha kuizidi Iringa tu achilia mbali Arusha?

Hiyo DSM majimbo yenye maendeleo makubwa ni yapi?
Hiyo Mwanza ya 2014 na ya sasa kumeongezeka nini zaidi ya daraja la furahisha?
Dsm - Pwani - Moro - Dom - Mpaka Mwanza Kuna mradi wa sgr, Mwanza Kuna mradi wa daraja la kigogo - busisi, mladi was maji ya ziwa Victoria (ndugu zangu tuliomaliza sengerema miaka ya 2012) shida ya maji ilivyokuwa na mingine mingi
 
Hyo sio sababu ya kuhalalisha wizi wa kura.
Ila wapinzani nao wametia dosari sana hasa kile kipindi wanatoka bungeni na kususia vikao wananchi nasi tunachoka na njia hii ya kususia, tunawachagua wa kututete bungeni wao wanatoka bungeni
 
This is too much. Hata sisi wana-CCM hatujafurahia. Level ya ubunge ngoma ingeachwa fair at least tukawapata wabunge cream kutoka na upinzani. Ambao kwa ukweli wamekuwa na mchango mkubwa sana sana toka 1992. Leo hii tunaingia kwenye bunge ambalo wabunge wote ni CCM 100%kutoka bara. Labda wa ACT kutoka Pemba kuingia bunge wa JMT, ila napo it depends na kama watakubali au itakuwa kama last time.

Kwa hakika ni uzuni. na wananchi tusishangilie hili. Nchi imeingia katika majaribio makubwa sana. kwa wale slow learners mtaanza kuona madhara yake not even far just 2022.

Nidiriki kusema haijawa njia sahihi na sio afya kwa demokrasia. Mapungufu na wizi ulikuwepo wa kiwango cha juu sana sana. Anyway, tumerudi nyuma hatua 30 katika demokrasia aliyotuachia Baba wa Taifa na Mzee Kikwete.

Hata Mwalimu Nyerere alikuwa anarusu fairness na amekuwa na wabunge wa upinzani before Chama kimoja. Mwinyi naye. Mkapa naye na Kikwete naye. Ila hii ya wabunge wote kutoka bara kuwa CCM... Duuuuh!. kweli tunatofautiana fikra
Nape acha Unafiq Mkuu
 
Back
Top Bottom