Uchaguzi 2020 Nchi imeamka ikiwa na huzuni kubwa sana, Kwamba wabunge wote Bara 100% wameshinda wa CCM

Uchaguzi 2020 Nchi imeamka ikiwa na huzuni kubwa sana, Kwamba wabunge wote Bara 100% wameshinda wa CCM

🤣🤣🤣🤣 nimesoma tu heading ya thread nimecheka sana kabla hata sijaingia ndani kusoma uzi wenyewe 😂😂😂. By the way kuna wana wengi sana humu walikuwa wanatukana wana ccm na kusema mwisho wao ni tar 28 mwez wa 10...labda mapema bado asubuhi nadhani wameanza kuziona Dalili za kinachoenda kumpata Lissu...
Ukitaka kujua kuwa watu walikuwa wanamwelea magufuli wewe piga hesabu ni madiwani wangapi, na wabunge wangapi ambao walikuwa madarakani wakajiuzulu na kuhamia ccm wakisema wanaenda kumuunga Mkono Rais katika juhudi za kuleta maendeleo.
Hao walishasoma nyakati mapema mno 😂😂😂

Na kama wabunge asilimia 90 watakaoenda bungeni watakuwa ccm basi jua kabisa kuna uwezekano wa Bunge kupiga kura ya kubadili katiba na kura ikapita na Magufuli akaendelea kugombea urais then maisha yaendelee
 
Kama usemayo nikweli Basi itakuwa hatari zaidi..
Upinzani Ni mhimu mahali popote pale na ndo huchochea maendeleo ya kitu fulani.
Kwani tuna upinzani au UKINZANI? kupinga kila jambo sio upinzani hata kidogo. Ngoja tuanze upya, kuna sehemu tulikosea kwenye msingi
 
Kwani tuna upinzani au UKINZANI? kupinga kila jambo sio upinzani hata kidogo. Ngoja tuanze upya, kuna sehemu tulikosea kwenye msingi

Kubwa lijalo bila kuvuta subira
 
Wapiga kura wenyewe wameamua hivyo.
Vyama vya siasa vya upinzani walionywa mapema, WAACHE UWANAHARAKATI.
Wawasemee watu Wawe na kauli muendelezo ( Cosistency ideas and thoughts)
Tujifunze na tusubiri 2025.
 
Kwani wabunge wameteuliwa si dio maana ya uchaguzi walikua wanaambiwa waseme sera wao wanatukana wamevuna ulicho panda
 
Kama usemayo nikweli Basi itakuwa hatari zaidi..
Upinzani Ni mhimu mahali popote pale na ndo huchochea maendeleo ya kitu fulani.
Kama utapinga hata yenye msingi hakuna faida ya upinzani .
 
Babu yangu alinambia asiesikia la mkuu huvunjika guu. Acha nchi iongozwe bila upinzani kwa miaka 5 tuheshimiane.

Nimesema Tundu anaiua chadema. Baada ya kuanza kuutukuza uulaya na kudharau utanzania alipoteza hata wale wananchi wachache waliokua wakimuonea huruma
Wa Tanzania hawapendi dharau
 
This is too much. Hata sisi wana-CCM hatujafurahia. Level ya ubunge ngoma ingeachwa fair at least tukawapata wabunge cream kutoka na upinzani. Ambao kwa ukweli wamekuwa na mchango mkubwa sana sana toka 1992. Leo hii tunaingia kwenye bunge ambalo wabunge wote ni CCM 100%kutoka bara. Labda wa ACT kutoka Pemba kuingia bunge wa JMT, ila napo it depends na kama watakubali au itakuwa kama last time.

Kwa hakika ni uzuni. na wananchi tusishangilie hili. Nchi imeingia katika majaribio makubwa sana. kwa wale slow learners mtaanza kuona madhara yake not even far just 2022.

Nidiriki kusema haijawa njia sahihi na sio afya kwa demokrasia. Mapungufu na wizi ulikuwepo wa kiwango cha juu sana sana. Anyway, tumerudi nyuma hatua 30 katika demokrasia aliyotuachia Baba wa Taifa na Mzee Kikwete.

Hata Mwalimu Nyerere alikuwa anarusu fairness na amekuwa na wabunge wa upinzani before Chama kimoja. Mwinyi naye. Mkapa naye na Kikwete naye. Ila hii ya wabunge wote kutoka bara kuwa CCM... Duuuuh!. kweli tunatofautiana fikra
Ubarikiwe kwa kulitambua hilo ndugu yangu
 
Hivi unajisikiaje wewe mwananchi wa hai, arusha mjini na Moshi mjini, mbeya mjini, mbunge wako kakaa miaka 10+ hamna kitu amefanya alafu unasikia Mwanza, Dar es Salaam, Pwani na mikoa mingine inapaa tu, roho lazma ziume na hayo ndo matokeo yake
 
''Nchi imeamka ikiwa ni huzuni mkubwa sana, Kwamba wabunge wote Bara 100% wameshinda wa CCM''

Hizo huzuni zitoke wapi wakati mwaka huu ''tumesema sasa basiiii'' (in Lissu voice)

Sisi sio kama Lowassa aliyesema hawezi kuingiza watu barabarani!

Wahenga walisema, ''kufa kufaana''.

Wewe ukiwa na huzuni mwingine ana furaha!

Tanzania kuna vituko!
Sanduku la kura linabebwa mtu anapanda nalo boda boda anatokomea nalo chombo cha habari kinaripoti eti
kituko chatoa mtu akimbia na sanduku la kura!!! Yaani sanduku la kura linaibiwa mchana kweupe then wanasema ni kituko? Badala ya kukemea?
 
Back
Top Bottom