Uchaguzi 2020 Nchi imeamka ikiwa na huzuni kubwa sana, Kwamba wabunge wote Bara 100% wameshinda wa CCM

Uchaguzi 2020 Nchi imeamka ikiwa na huzuni kubwa sana, Kwamba wabunge wote Bara 100% wameshinda wa CCM

Msisingizie wïzi, maneno ya jpm na majaliwa ktk kampeni kuwa raia wanajichelewesha wenyewe na wao jpm na majaliwa wanataka connection ndio maneno chachu kwa wananchi. Wànanchi wamechagua maendeleo.
Mengine ni visingizio, ktk mkutano wa mbowe hai wananchi wa haî wanampiga maswali mazito mbowe anasingizia wametumwa, hii ngoma wapizaní wamelala. Watumie muda huu kujipanga.
Kwa bungeni ni upinzaní gani tutaumiss zaidi ya kugomea bajeti?
Màjimboni ni nini tutamiss wàkati hawajawã na mchango?
Tusikariri kuwa piga ua lazima wawepo wapinzani mia bungeni, zîto amekua na hoja zaidi ya wabunge wote wa upinzani.
Unadhani wananch ni wajinga kama, yani miaka yote 60 mko nyie tu leo mlaumu upinzan? majimbo ambayo mko CCM pekee mmefanya nini??

ukiwa mjinga n ww peke yako, usijumlishe watu wengine kwenye huo ujinga
 
Mkuu Pagan Amum, ukweli lazima tuukubali na kuuheshimu kwama viongozi wa vyama vya upinzani, hasa wawakilishi wetu, hawakutenda kama tulivyowatarajia, katika kipindi cha utawala wa Serikali ya CCM.
√ Walipinga juhudi za maendeleo wakidai ni maendeleo ya vitu;
√ Mbaya zaidi walitumia lugha ya matusi, tuhuma za uzushi na kuhamasisha vurugu wakati wa kampeni; na
√ Isitoshe vyama vya upinzani, hasa CHADEMA, chama kikuu, na ACT-Wazalendo, viliwekeza nguvu zao zote kwenye wagombea Urais, ambao walishindwa kuwashawishi wapiga kura kwa hoja za kisera.

Kama ulivyosema afya ya kisiasa siyo nzuri sana uwakilishi kuwa wa chama kimoja cha siasa. Lakini kumbuka, CCM ina jinsi nzuri ya uendeshaji kudhibiti na kusimamia utekelezaji wa Ilani yake ya Uchaguzi kuliko vyama vingine vya siasa, ambavyo viongozi wake wamekuwa wakishutumiana kwa matumizi ya ruzuku na mali za chama

Mmebaki wenyewe bunge zima tuone sasa ndan ya hii miaka mitano nchi itakuwa kama urayaaaa
 
Kuna msemo unasema kama uwezi kupamba nao ,ungana nao.Mungu mwema.kila kitu kinasababu na sababu yenyewe ndio hii.Maisha lazima yaendelee atiiii
 
Mkuu unapinga wananchi kuamua au ulitakaje? Mimi na pengine hata wewe hatujachagua CHADEMA kutokana na msimamo wao wa kutaka watanzania kuwa mashoga ili tupate msaada toka Marekani na Canada huku viongozi wawe wanatuibia mali zetu na kujilimbikizia, kujinufaisha wao na familia zao. Wacha upinzani ufe tu, hawana jipya.
 
Hatutaki demokrasia uchwara!!! Demokrasia ya kuhimizana kuingia barabarani!!! Tunataka demokrasia ya kuhimizana kuingia kazini kujenga nchi yetu Tanzania.
Mmeipata sasa pigeni kazi. Maisha yatakuwa mepesi sasa....upinzani walitubana sana.....sasa hata mishaara itaongezeka
 
''Nchi imeamka ikiwa ni huzuni mkubwa sana, Kwamba wabunge wote Bara 100% wameshinda wa CCM''

Hizo huzuni zitoke wapi wakati mwaka huu ''tumesema sasa basiiii'' (in Lissu voice)

Sisi sio kama Lowassa aliyesema hawezi kuingiza watu barabarani!

Wahenga walisema, ''kufa kufaana''.

Wewe ukiwa na huzuni mwingine ana furaha!

Tanzania kuna vituko!
kumbe na wewe unatumia vpn kama korea kaskazini hahahhaha kumbe hata wewe unayapata mauchungu ya magu hahahaha nilikuwa nafikiri ni mimi mwenyewe hahahah
 
Nimekufuatilia kwa muda mrefu kupitia jukwaa la Kimataifa ukiwa ni hodari wa kuchambua mambo kiuweledi lakini ninasikitika kila mahali inapoguswa CCM hata kama inafanya uharamu unatetea, ajabu mpaka kwenye mambo ambayo yapo wazi ambayo ni haramu CCM wanafanya unatetea.

Nilichogundua kuwa hauna haya! And if you dont have this quality of bashfulness, then you can do whatever you wish! Because there's nothing can stop you from doing a shameless thing.

Na hauna hata chembe ya kumuogopa Mungu! Sina chama ila ninachokijua ni haki na batili.
Mkuu kwanza pole na kumradhi kwa kukukwaza. Yawezekana TUJITEGEMEE wa jukwaa la kimataifa akaonekana tofauti katika majukwaa mengine. Ukweli ni TUJITEGEMEE yuleyule.

Hata hivyo, linapokuja suala la nchi yangu Tanzania ( sina Tanzania nyingine, sina mbadala wa Tanzania) na Afrika kwa ujumla niko tayari kuitwa majina yoyote kama ni suala la kuitetea Tanzania, watanzania, Afrika na waafrika na wote wenye kujali utu ulimwenguni!! Siwezi kuona aibu katika hili. Hivyo, ninaomba uniwie radhi katika hilo pia.

Naitamani Tanzania imara kimaendeleo katika nyanja zote na Tanzania itakayoendelea kuwepo! Yeyote anayetamani Tanzania isiwepo ama irudi nyuma kimaendeleo awe tayari kuniita majina anayotaka, kwa sababu sitakubaliana naye na sitaona aibu katika hilo.

Tuendelee na mjadala Mkuu.
 
Back
Top Bottom