Mkuu kwanza pole na kumradhi kwa kukukwaza. Yawezekana TUJITEGEMEE wa jukwaa la kimataifa akaonekana tofauti katika majukwaa mengine. Ukweli ni TUJITEGEMEE yuleyule.
Hata hivyo, linapokuja suala la nchi yangu Tanzania ( sina Tanzania nyingine, sina mbadala wa Tanzania) na Afrika kwa ujumla niko tayari kuitwa majina yoyote kama ni suala la kuitetea Tanzania, watanzania, Afrika na waafrika na wote wenye kujali utu ulimwenguni!! Siwezi kuona aibu katika hili. Hivyo, ninaomba uniwie radhi katika hilo pia.
Naitamani Tanzania imara kimaendeleo katika nyanja zote na Tanzania itakayoendelea kuwepo! Yeyote anayetamani Tanzania isiwepo ama irudi nyuma kimaendeleo awe tayari kuniita majina anayotaka, kwa sababu sitakubaliana naye na sitaona aibu katika hilo.
Tuendelee na mjadala Mkuu.