Uchaguzi 2020 Nchi imeamka ikiwa na huzuni kubwa sana, Kwamba wabunge wote Bara 100% wameshinda wa CCM

Uchaguzi 2020 Nchi imeamka ikiwa na huzuni kubwa sana, Kwamba wabunge wote Bara 100% wameshinda wa CCM

Hatutaki demokrasia uchwara!!! Demokrasia ya kuhimizana kuingia barabarani!!! Tunataka demokrasia ya kuhimizana kuingia kazini kujenga nchi yetu Tanzania.
Sasa Watanzania wajiandae kuona faida na hasara ya vyama vya upinzani. Hadi 2025 watanzania wajiandae kisaikologia kudumazwa akili na siasa ya vyama kimoja. Habari ya mjini Sasa kila kitu ni ndiyo mzee . Walio kataa upinzani kisa wataletewa MAENDELEO tunayasubiri kwa hamu hayo MAENDELEO CCM itakayoyapeleka kwenye hayo majimbo. Ila mkumbuke kuwa haya Jimbo la spika ndugai like CCM tangu mwaka 1977 ila Hali ya MAENDELEO ni zero.
 
Hilo bunge najaribu kuwaza tu litakuaje
Litakuwa bunge la kipuuzi kuwahi kutokea, nashangaa mazuzu hapa mtaani wanafurahia wabunge wa upinzani kushindwa, hawajui hii inaenda kuruhusu sisi kama taifa tuwe wapuuzi, bunge la rubber stamp
 
Hahahahaaa huzuni imetanda ngome kuu za CHADEMA,

Mbeya CCM, HAI CCM, Kil mjini, CMM
Hatariiiiiii😂😂😂
 
Baba wa taifa alituset up kwa hili.. Ila tusimlaumu Sana.. Je sisi tumefanyeje kutoa hii Hali
 
Sasa watawarudishia na Bunge live
Salary Slip, kwahiyo ni kweli kwamba walitoa bunge live kwa kuhofia wananchi wataona cheche za waliokuwa wabunge wa upinzani ?, sas wakirudisha bunge live na hao wabunge wa ccm peke yao wakiwa hawana wa kuwa challenge binafsi sitaweza kupoteza muda kuangalia bunge hilo kwani naamini ltakuwa la hovyo sana
 
Mkuu kwanza pole na kumradhi kwa kukukwaza. Yawezekana TUJITEGEMEE wa jukwaa la kimataifa akaonekana tofauti katika majukwaa mengine. Ukweli ni TUJITEGEMEE yuleyule.

Hata hivyo, linapokuja suala la nchi yangu Tanzania ( sina Tanzania nyingine, sina mbadala wa Tanzania) na Afrika kwa ujumla niko tayari kuitwa majina yoyote kama ni suala la kuitetea Tanzania, watanzania, Afrika na waafrika na wote wenye kujali utu ulimwenguni!! Siwezi kuona aibu katika hili. Hivyo, ninaomba uniwie radhi katika hilo pia.

Naitamani Tanzania imara kimaendeleo katika nyanja zote na Tanzania itakayoendelea kuwepo! Yeyote anayetamani Tanzania isiwepo ama irudi nyuma kimaendeleo awe tayari kuniita majina anayotaka, kwa sababu sitakubaliana naye na sitaona aibu katika hilo.

Tuendelee na mjadala Mkuu.
Kwa anayoyafanya Magufuli ndiyo Tanzania unayoitamani?
 
Kwa anayoyafanya Magufuli ndiyo Tanzania unayoitamani?
Kwa swali lako hili naona bado hujaniwia radhi! Hata hivyo, nimeisha timiza wajibu wangu. Nikirudi mazima sasa kwenye swali lako, ili nikupe majibu sahihi utayoyaelewa utalazimika kwenda kusoma ilani za vyama vyote vilivyoshiriki uchaguzi. Katika usomaji wako angalia ni chama gani kilikuwa na ilani yenye mwelekeo wa Tanzania unayoitaka.

Mkuu, inabidi uende ukazisome kweli, vinginevyo ukirudi hapa tutashindwa kuelewana kile tutakachokuwa tunaulizana.
 
Niko balazani kwangu nikiangaza huku na huko kuona kama kuna kundi lolo la vijana linalo andamana, lakini mpaka sasa sijaona kikundi wala kikundu.

Kiufupi vijana munapenda sana kutiana ujinga.
Mukiwa nyuma ya keyboard munatamba sana, likija swala la kufanya, muna mbwela.
Haya, sisi tunaendelea kuongoza nchi.
 
Na kiko karibu kinakuja Insha Allah
Watu wa qawmi HUD a.s walimwambia Nabii HUD A.S "Man ashaddu minna quwwa" wakimaanisha ni nani mwenye nguvu kuliko sisi?!

Hajjaj ibn Yusuf ath-Thaqafi alikuwa ni ni Gavana aliyejipambanua mtu safi anayemfuata Mungu lakini alikuwa anakata shingo za watu kama mtu anavyokata machungwa!

Hawa wote walijisahau kuwa yupo aliyewaumba ambaye ni mwenye nguvu kuliko wao! Waischogundua kwamba hakuna dua mbaya kama dua ya aliyedhulumiwa! Haitoshi wanaua! "Bi ayyi dham'bin qutilat?" Kwa dhambi gani waliyoifanya wenzao mpaka wanawaua?

Utaratibu wa kuchagua wameuleta wao na kuugongelea msumari wa moto kuwa ndiyo unaopaswa ufuatwe. Wahusika wameufuata na kuwachagua wanaowataka wao wanawaua! Yaani ndiyo dhambi yao hiyo mpaka unatoa uhai wa wenzako?!

Historia inaonyesha wazi mfano wa njia mamlaka waliyoichukua italeta maafa makubwa mchini! Iwe mapema au mbali hii njia ni yenye kuleta maafa! Hili taifa nalipa miaka 2 litakuwa limeshaharibika!
 
Haki Ipo Kwa Mungu
Acha Aendelee Mpaka Hapo Atakapochoka Mwenyewe.
Mmna huo moyo wake wente betri, tunamtakia kila la kheri lakini ajue hakuna marefu yasiyo na ncha, na mwisho wake utakua mbaya sana
 
Niko balazani kwangu nikiangaza huku na huko kuona kama kuna kundi lolo la vijana linalo andamana, lakini mpaka sasa sijaona kikundi wala kikundu.

Kiufupi vijana munapenda sana kutiana ujinga.
Mukiwa nyuma ya keyboard munatamba sana, likija swala la kufanya, muna mbwela.
Haya, sisi tunaendelea kuongoza nchi.
na iwe fundisho kwa wapinzani wanaolishwa upepo na mitandao ya kijamii....
CC: MariaSarungi!
 
Back
Top Bottom