Uchaguzi 2020 Nchi imelipuka, kila kona, kila sehemu naona ni Tundu Lissu

Zikiwa zimebaki siku 3 kabla hatujaingia tarehe 28.10.2020 siku ya kufanyika kwa uchaguzi Mkuu Tanzania, nadiriki kusema kuwa nchi naona inamtaka Lisu..... Nimezunguka Mikoa 25 ya Bara na 3 ya Zanzibar, nimepita kila pembe ya nchi. Nimezunguka vijijini sana na kila kona ya nchi hii kwa shughuli za kikazi katika NGO aiseeee sijui nini kitokee ila nimeshuhudia kwa macho yangu na kuona namna Lisu anavyokubalika sana sana...

Ambacho sikuamini ni mwamko walionao vijijini ni mkubwa kuliko hata wa majiji. Vijijini wanasema kwa hii njaa ya miaka 5 hawawezi tena kuipa serikali hii kura... Jana nilivyokuwa narudi Dar es Salaam, nilipita takriban mikoa 7 kutoka kanda ya ziwa nimeshuhudia namna Mawakala wa upinzani walivyojipanga na kupeana semina wenyewe kwa wenyewe.....

Bahati mbaya zikwenda kukusanya data za kisaisa ila kwa haya nilioyaona katika hiyo Mikoa 28 sioni namna Tundu Lisu akashindwa huu uchaguzi...... Watu wamechoka, watu wana njaa, watu hawana fedha, watu wamekosa matumaini..... Tena ukiwauliza maswali wanakujibu waziwazi kuwa kwa mbunge huyo sawa tutampa wa CCM ila suala la Urais Hapana tunampa "Mbeba Maono"....
Ninamashaka sana ya uatfiti wako nadhani hauamini (not credible)! Siku moja mikoa saba, na unakuja na majibu ambayo unataka watu waamini! Tanzania ina mikoa 30, wilaya 139, Halmashauri 185, Kata... na vijiji 12,0000+ . Naomba kujua samble size ya utafiti wako, Sampling procedures nk ili niamini katika utafiti. Naomba tuwe wakweli wewe umepita barabarani, makao makuu ya mikoa, wilaya kadhaa unatoa taarifa ya Nchi, na mikoa saba. Hatujui ni watu gani uliwauliza inawezekana ni wenye mawazo kama yako au waliamua wakubalie tu! Hata JPM kwa miaka mitano ya Urais ,anaendelea na maendeleo ya Nchi yake, haendi nje ya Nchi hajamaliza kuitembelea hata robo ya Tanzania. Nyerere miaka 25 ya Urais , leo ukienda wananchi wanasema hatujawahi kutembelewa na Rais! Wewe siku moja unatoa majibu ya jumla jumla mikoa saba, taarifa siyo sahihi! Naomba tukutane Novemba 2020 uthibitishe utafiti wako. Wananchi wanaopata maji, umeme , Elimu Bure, waliopata ajira zilizokuwa zinakaliwa na vyeti feki, watumishi waliolipwa mapunjo ya mishahara (salary arrears), likiozo, wanaotibiwa kwa 30,000/= familia ya watu sita (6) kwa mwaka kupitia CHF iliyoboreshwa kuanzia zahanati- hadi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa. Wanaompata Dakatari kwenye kituo cha Afya, wanaosoma shule yenye maabara kijijini, wanaokoa muda wa safari, vifo kutokana na wingi wa madaraja na vivuko, waliopata hati za ardhi zao kwa muda mfupi bila usumbufu nk. Ninaamini tarehe 28.10.2020 wataongea kwa sauti tofauti na utafiti wako.
 
Hiyo nchi nahisi iko pale ndani ya jengo bovu la ofisi za ufipa, ila kama ni hii tz, nakuonea huruma kwa kudanganya nafsi yako.
 
Lissu ni mpango wa Mungu ndio maana familia ya shetani ilishindwa kumuua
 
Wewe bila shaka una kinyongo na Magufuli yawezekana ulikua hulipi kodi au ulikua na cheti hewa ukatumbuliwa au ulikua unafanya biashara za magendo.
Wewe unaona ni sawa mtu amebakiza mwaka 1 kustaafu unafukuza bila chochote, busara ilitakiwa
 
Huku ni kujifariji tu ila ccm ndiyo ileile na njia zao za kuwafanya waendelee kuwa madarakani bado ziko vilevile hakuna kilichobadilika,sasa hapo mtu unaanzaje kutegemea matokeo kuwa tofauti?
 
Ninamashaka sana ya uatfiti wako nadhani hauamini (not credible)! Siku moja mikoa saba, na unakuja na majibu ambayo unataka watu waamini! Tanzania ina mikoa 30, wilaya 139, Halmashauri 185, Kata... na vijiji 12,0000+ . Naomba kujua samble size ya utafiti wako, Sampling procedures nk ili niamini katika utafiti. Naomba tuwe wakweli wewe umepita barabarani, makao makuu ya mikoa, wilaya kadhaa unatoa taarifa ya Nchi, na mikoa saba. Hatujui ni watu gani uliwauliza inawezekana ni wenye mawazo kama yako au waliamua wakubalie tu! Hata JPM kwa miaka mitano ya Urais ,anaendelea na maendeleo ya Nchi yake, haendi nje ya Nchi hajamaliza kuitembelea hata robo ya Tanzania. Nyerere miaka 25 ya Urais , leo ukienda wananchi wanasema hatujawahi kutembelewa na Rais! Wewe siku moja unatoa majibu ya jumla jumla mikoa saba, taarifa siyo sahihi! Naomba tukutane Novemba 2020 uthibitishe utafiti wako. Wananchi wanaopata maji, umeme , Elimu Bure, waliopata ajira zilizokuwa zinakaliwa na vyeti feki, watumishi waliolipwa mapunjo ya mishahara (salary arrears), likiozo, wanaotibiwa kwa 30,000/= familia ya watu sita (6) kwa mwaka kupitia CHF iliyoboreshwa kuanzia zahanati- hadi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa. Wanaompata Dakatari kwenye kituo cha Afya, wanaosoma shule yenye maabara kijijini, wanaokoa muda wa safari, vifo kutokana na wingi wa madaraja na vivuko, waliopata hati za ardhi zao kwa muda mfupi bila usumbufu nk. Ninaamini tarehe 28.10.2020 wataongea kwa sauti tofauti na utafiti wako.
Soma andika vizuri..... Mikoa saba nimesema hiyo ni Jana on my way coming back to Dar.... From Kanda ya ziwa.. But nimezunguka mikoa yote 26 bara na 3 zanzibar kwa zaidi ya siku 81
 
Back
Top Bottom