Nchi imepigwa nusu kaputi. Vikosi vya uokoaji vimefika eneo la tukio vikiwa mikono mitupu

Nashindwa kuelewa kwanini iwe hivyo, sijui chanzo ni ajali kuhusisha shirika binafsi la ndege au kitu gani kingine?

Lakini historia yetu kwenye haya matukio ya ajali mara nyingi ndivyo zilivyo, tumezubaa sana, hasa nikikumbuka kuzama kwa meli ya MV Bukoba kama pangefanyika juhudi za dhati na haraka bado naamini zingeokoa maisha ya wengi sana waliofariki kwenye ile ajali.
 
"CCM chama Makini".Alisikika kichaa mmoja kutoka mirembe
 
Nchi ngumu hii
 
Ile video kwa Millard Ayo wale wanajeshi wawili wanapiga story tu badala wazame kwenye uokozi [emoji119]
Walikua wanasuburi watu wanywe kwanza maji wavimbiwe ndipo wazame sijawaona pengine hata vifaa hawakuwa navyo
 
Kila ukipanda Ndege unaelezwa ikitokea Dharura kwenye maji ufanye nini.
Chini ya siti kuna lifejacket unalivaa ukilivaa unaelea hata kama hujui kuogelea.

Hao ziimamoto na uokozi leo jumapili wanakunywa bia zao.
Waweza kuwa sahihi sababu elimu tuliyonayo inatusaidia kukariri sio uhalisia wa mazingira.

Ebu tuone na mazingira ya kwenye tukio

-Vioo vya madirisha na milango yote imefunikwa kwa maji, umebaki mkia tu

-ikumbukwe wakati wa kupaa na kutua ni sharti kufunga mikanda. Kwaio wahanga wote, kwa kanuni hii walikwa wamebanwa sawasawa kwenye viti vyao+paniki+elimu zetu zinazotolewa na wasaidizi wa ndege (pengine hawakuwa wamelitoa hili somo)+uzoefu wetu katika kupambana na haya majanga.

Kwaio mkuu, baadhi ya kanuni ni inapplicable. kutegemeana na hali.
 
Nchi nyengine hapa waziri husika alitakiwa kujiuzulu!! Kwetu uataambiwa una chuki na waziri !! Sisi mara nyingi tunataka mizimu ya baba zetu itufanyie kazi,tunataka kila kitu Mungu atufanyie kazi.Hatutaki kutumia akili kutatua matatizo yetu .Yani tunabahatisha !! Huna cheni ya mita 100 kuweza kusaidia kuvuta ndege halafu unataka Mungu akusaidie nini? Juzi ndege ya Korean air ilipata ajali ikiwa na abiri zaidi 170 na wote waliokolewa wakiwa wazima .sisi tumambulia 26 tu!! Dah inauma kwa kweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…