Kuhusu huyo mtoto wa Rugemalira naweza kumtetea. Hiyo familia imekuwa inajihusisha na Biashara tangu miaka ya 90.
Mzee wao ana kiwanda cha beer cha Heineken na biashara nyingine ikiwemo kampuni ya kuzalisha Umeme wa IPTL kama mbia.
Ndiyo maana hata baada ya kufungwa na JPM kuhusu Uhujumu Uchumi, yeye aliishia kutolewa baada ya kukosekana ushahidi wa kumtia hatihani.
Kumbuka Familia ya Rugemalira sio watumishi wa Umma.
Hivyo ni ngumu wao kuingia Benki Kuu kuchota fedha za Umma isipokuwa Watumishi na Viongozi waliopewa dhamana ya kutuongoza.
Kama kuna lawama, nadhani wanaostahili ni Viongozi wa Umma na sio hao akina Rugemalira.
Tujitahidi kuchagua Viongozi waadirifu kwenye nafasi zote za Uongozi badala ya kuwachagua Viongozi wezi, mafisadi, wachafu, wenye skendo n.k