Leo Magufuli anasifiwa na kukumbukwa kimafiki tu. Hiyo ndiyo kawaida ya Watanzania lazima wamponde aliyepo na kumsifia aliyepita, hata wewe
britanicca ukipewa madaraka sidhani kama utakuwa tofauti na waliopo.
Alipkuja AH Mwinyi, Mama Sitti aliandamwa kila mahali kuwa anafanya biashara Ikulu.
Akaja Mkapa, Mama Anna Mkapa tukaambiwa amejigawia mgodi wa Kiwira, mara amnamiliki Lamada hotel pale Msimbazi.
Wakati wa JK tukaambiwa anamiliki vituo vyote vya Lake Oil, na kwamba ile Big Bon ya Sinza ni mali yake.
Magufuli pamoja na ukali wake wankupinga ufisadi, hakuwa tofauti na watangulizi wake. Yeye alichagua kikundi kidogo cha wanafamilia wake na wasukuma kadhaa kama akina Biswalo Mganga, Makonda, Mnyeti, Dotto James, Mfugale, Kijazi etc ndiyo walikuwa wanakula mema ya nchi hii