Nchi inaongozwa na CCM, kwanini wanalaumiwa CHADEMA?

Nimesoma mara ya kwanza sijaelewa, nikarudia mara ya pili sijaelewa, nikarudia mara ya tatu Ila bado. Wenzetu hamna akili?
Kipindi CHADEMA wanapinga ukuta wa Mererani mlikejeli kaingia Samia anasema baada ya ukuti wizi ulizidi kupitia mahandaki!!

Yaani nyie watu Kila kitu lawama CHADEMA alafu baadae kitu hiko hiko kikifanywa na CCM mnanywea!!

Njooni sasa mseme CCM inatumika na wazungu ndio maana ilikejeli uwepo wa ukuta. Au wakikosoa wapinzani pekee ndio wanageuka mabeberu??
 
Kila Mtanzania anazo.
Walioficha kifo Cha mungu wako JPM ni CHADEMA?? Ila baada ya kifo mkaanza kudai eti Lissu kahusika!! Hahahahha

Kwamba hao walioficha ndio wazalendo eeh?? Ila aliyetoa taarifa kuhusu ugonjwa wake ndio mkamshambulia eti katumwa na Beberu!!
 
Nchi hii inaongozwa na CCM, ni kwa nini basi kila lawama ya kukwama kwa mambo wanatupiwa CHADEMA? Au CCM wanaona wanaostahili kuongoza nchi yetu ni CHADEMA?
Nguvu kubwa mno ya kidola imeshatumika mpaka Sasa kukivuruga hiki chama, hiki chama hakijawahi kushika dola Ila kinaogopeka mno na watawala.
 
Serikali ya ccm kila ikitaka kufanya jambo la maendeleo Chadema wanaleta figisu yani kwa lugha nyepesi Chadema ni kama wachawi

Sent from my TECNO Camon CX using JamiiForums mobile app
 
Nimesoma mara ya kwanza sijaelewa, nikarudia mara ya pili sijaelewa, nikarudia mara ya tatu Ila bado. Wenzetu hamna akili?
Utaelewa vipi na hizo pombe zako za kienyeji ulizo kunywa mchana wa jua kali? Kale kwanza chakula cha mchana ili akili yako ikae sawa.
 
Nakumbuka Kipindi Mbowe anasema chanjo iletwe mlisema anatumika na mabeberu, kaingia Samia kuanzia bunge mpaka mawaziri na serikali kwa ujumla Waka support Hilo suala tena ilifika hatua waliopinga chanjo wakasimamishwa teuzi!!

Kwahiyo zile lawama za CHADEMA kwenye chanjo zilikua na faida Gani kama Wana CCM na nyie mmesupport?? Au tukubaliane CCM inatumika na mabeberu?
Ndugu yangu, CCM ndio mabeberu.
 
Kwa ufuatiliaji wangu niliofanya kwenye mambo mbali mbali, nimegundua kwamba CHADEMA imekuwa ikiliaumiwa mara nyingi kwamba haitimizi wajibu wake hadi mambo yanaharibika. Kwamfano;

Wakati wa Bunge la katiba CHADEMA iliongoza vyama vingine kutoka kwenye vikao vilivyokuwa vinaendelea vya Bunge la Katiba kupinga jinsi Bunge hilo lilivyokuwa linaendeshwa.

Na mchakato wa kupata Katiba mpya ukaishia hapo. Lakini wabunge waliobakia walikuwa wengi na walipitisha Katiba Pendekezwa. Kwa nini mchakato wa kupiga kura ya maoni ili kuipitisha hiyo Katiba ulifutiliwa mbali?

Huo ni mfano mmoja tu, lakini ukiangalia hata ile marufuku ya kuzuia mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa ililengwa CHADEMA. Hoja iliyotolewa wakati ule na hata sasa ni kwamba mikutano hiyo inazuia watu wasifanye kazi.

Nchi hii inaongozwa na CCM, ni kwa nini basi kila lawama ya kukwama kwa mambo wanatupiwa CHADEMA? Au CCM wanaona wanaostahili kuongoza nchi yetu ni CHADEMA?
Ndo ushangae, hata nyongeza hewa ya mishahara wanalaumiwa Chadema😀
 
Nakumbuka Kipindi Mbowe anasema chanjo iletwe mlisema anatumika na mabeberu, kaingia Samia kuanzia bunge mpaka mawaziri na serikali kwa ujumla Waka support Hilo suala tena ilifika hatua waliopinga chanjo wakasimamishwa teuzi!!

Kwahiyo zile lawama za CHADEMA kwenye chanjo zilikua na faida Gani kama Wana CCM na nyie mmesupport?? Au tukubaliane CCM inatumika na mabeberu?
Vibaraka wa mabeberu walisema tutashitakiwa MIGA, mpaka sasa tunadunda na hakuna case yoyote.
 
Kwenye list ya wezi wa makinikia au majizi kwenye ripoti ya Tanzanite one kuna jina la Chadema yoyote?

Hivi unafahamu makamu wa Rais wa BARRICK Tanzania mlimpa ubunge wa makambako??

Alafu ndio mnajiuliza wakala wa Beberu ni yupi?
Wakala wa mabeberu ni aliyekuwa anaunga mkono mabeberu na masilahi yao over Tanzania and Tanzanians.
 
Walioficha kifo Cha mungu wako JPM ni CHADEMA?? Ila baada ya kifo mkaanza kudai eti Lissu kahusika!! Hahahahha

Kwamba hao walioficha ndio wazalendo eeh?? Ila aliyetoa taarifa kuhusu ugonjwa wake ndio mkamshambulia eti katumwa na Beberu!!
JPM ni shujaa wa Afrika.

Kuhusu kifo kila nafsi itaonja umauti, hata wewe hautaishi milele.
 
Vibaraka wa mabeberu walisema tutashitakiwa MIGA, mpaka sasa tunadunda na hakuna case yoyote.
Ukimrudishia mtu anayekudai kitu chake, unataka akushitaki ili iweje?

Kwani yale mabilioni ya ACACIA tulilipwa??
 
Kwa ufuatiliaji wangu niliofanya kwenye mambo mbali mbali, nimegundua kwamba CHADEMA imekuwa ikilaumiwa mara nyingi kwamba haitimizi wajibu wake hadi mambo yanaharibika. Kwamfano;

Wakati wa Bunge la katiba CHADEMA iliongoza vyama vingine kutoka kwenye vikao vilivyokuwa vinaendelea vya Bunge la Katiba kupinga jinsi Bunge hilo lilivyokuwa linaendeshwa.

Na mchakato wa kupata Katiba mpya ukaishia hapo. Lakini wabunge waliobakia walikuwa wengi na walipitisha Katiba Pendekezwa. Kwa nini mchakato wa kupiga kura ya maoni ili kuipitisha hiyo Katiba ulifutiliwa mbali?

Huo ni mfano mmoja tu, lakini ukiangalia hata ile marufuku ya kuzuia mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa ililengwa CHADEMA. Hoja iliyotolewa wakati ule na hata sasa ni kwamba mikutano hiyo inazuia watu wasifanye kazi.

Nchi hii inaongozwa na CCM, ni kwa nini basi kila lawama ya kukwama kwa mambo wanatupiwa CHADEMA? Au CCM wanaona wanaostahili kuongoza nchi yetu ni CHADEMA?
CHADEMA inalaumiwa ili ibomolewe mafisadi ccm waendelee kulamba asali taratibu,lengo ni kuidhoofisha CHADEMA hakuna sababu nyingine.
 
Back
Top Bottom