Nchi inapaa, kelele lazima zitasikika tu, mitano tena

Nchi inapaa, kelele lazima zitasikika tu, mitano tena

Tuliokuwepo tangu awamu ya kwanza tunafahamu kwanini kelele za huyooo huyooo, mchinjeee mchinjeee zinasikika kwa wingi. Nchi imepaa ndani ya muda mfupi tu wa awamu hii unexpected.

Ukiona nchi inapaa kwa kutumia vyanzo na rasilimali zilezile walizonazo awamu nyingine maana yake Kuna mirija ya zamani imefungwa na mingine mipya imefunguliwa.

Mirija iliyofungwa ndio chanzo kikuu cha kelele zinazosikika. Aina na ukubwa wa kilele hizo utategemea upana na urefu wa mirija iliyofungwa na watu na idadi yao waliokuwa wanategemea mirija hiyo.

Kumalizia mamiradi yote ambayo aliianziaha marehemu Magufuli kwa wakati na kuanzisha na kumaliza mingine was unexpected kwa mwanagenzi tena mwanamke tena muislamu tena mzanzibar.

Wote tunafahamu kelele zinazosikika Zina ukubwa Gani, ni za aina Gani, ni za akina nani, zinatokea upande gani na Zina harufu Gani.

Wamekwama, Sasa wanataka kuwachochoe askari ili wafanye jambo, maana wao wameshindwa na kukwama kwakuwa wananchi hawawaelewi.

Tunafahamu na tunawajuwa, songa mbeleen tuko nyuma yako kwa kukuwa tunawajuwa. Ukishajua jina la mbwa wao nusu ya kazi imekwisha. Bandari ndilo lililokuwa rija lao kuu kupita mamirija yao yooote, umeliziba ndindindi.
Kwani watu hawatekwi na kuuwawa?
 
Kwani watu hawatekwi na kuuwawa?
Kama wewe na mimi hatujatekwa basi wewe na mimi pia tuna kazi ya kufanya utafiti kujua watu wote wanaotekwa na tabia zao pamoja na kufahamu nani amewateka na kwasababu Gani.
 
nchi inapaa?
Wakati nachat humu jf ni kituo kikuu cha Jayaka Kikuu Morogoro cha SGR nasubiri usafiri kwenda Dar. Hapa tunao wazungu na wajapan pia tunasubiri usafiri wa SGR hapa. Mzungu mmoja akasema mbele yangu kuwa taarifa wanazokwenda Ulaya kutoka Afrika ni vita za wenyewe kwa wenyewe, ukame, njaa, wanyama na umaskini mkubwa (poverty). Wanashangaa kukuta kumbe Tanzania Kuna treni za umeme hivi. Akasema tunashangaa kukuta supermarkets zenye Kila kitu tulichokuwa tukidhani hakuna na kusababisha tuvibebe kuja navyo.

Mzungu anashangaa lakini mjinga wa hapahapa eti haoni kitu.
 
nchi inapaa?
Kwani huoni? Propaganda zenu kwa vijana wasiokuwa na passport ni dhambi kubwa. Wazungu hawawezi kumsifia kiongozi anaepinga ushoga na kunyonywa. Eti demokrasia kwao ni pamoja na kukubali ushoga kuwa mtindo rasmi wa nchi . Kufilan marufuku kwetu
 
Acha kucheza Kamali ya Vindege
Acheni propaganda za uongo kwa vijana zinazoweza kuirarua nchi. Mpumbavu analinganisha Tanzania na Korea Kusini eti zilikuwa ziko sawa huko nyuma kimaendeleo, lakini hasemi kuwa kila kitu kule Korea ni mali ya Marekani na Korea Kusini imepoteza Uhuru wake kwa Marekani na Marekani ndiye anaeamua kila kitu kiweje ndani ya Korea Kusini. Wapumbavu Hawa wanaacha kuilinganisha tz na nchi nyingine za Africa badala yake wanatafuta kipimo Korea Kusini ili propaganda zao zipate maana,

Kuna wakati taifa lazima liamke mapema dhidi ya Hawa jamaa. Hawataki kusema kampuni ya Hyundai ni ya wamarekani waliokimbilia Korea kutoka Detroit, Michigan. Samsung hivyohivyo, na ndiyo maana Trump anawataka warudi nyumbani wakatengeneze ajira Marekani.
 
Ah. Sawa.
Ah. Sawa.
Sio sawa kuifananisha Korea na Tanzania hata kwa bahati mbaya, labda kama unataka kuchochea vijana kwenye jambo lako. Korea Kusini imetekwa na mabepari wa Magharibi, hakuna demokrasia kaaabisa. Ndiyo tunataka tz tuikabidhi kwa mabepari kisha sisi tuwe watazamaji? Kwanini tuiifananishe tz na nchi nyingine za Africa zenye mazIngira yanayofanana? Propaganda za kipuuzi kwa vijana wetu wasiokuwa hili Wala lile.
 
Back
Top Bottom