Mwezi mmoja na siku kadhaa zinaendelea kuonyesha shauku ya watanzania kuona viongozi wasaidizi wa mkuu wa nchi na waziri mkuu walitangazwa na kuwaona wakifanya kazi, baada ya Rais kuwatangaza na kuwaapisha mawaziri wawili, waziri wa fedha na mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika mashariki, wakitegemea siku si nyingi majina ya wateule wengine wapo ubaoni.
Wajuzi na wachambuzi wa mfumo wa kiuongozi wameongea na kujadili mengi ila uhamuzi lazima unafanywa na walioshika mpini.
Kuanzia leo jioni au teseme mwishoni mwa juma hili balaza jipya linaenda kutangazwa na kuna baadhi ya mabadiriko yanaenda kuonekana kwa viongozi wengi waliokuwepo hapo nyuma kukatwa na kuwekwa mawaziri na manaibu wapya kabisa.
Tega sikio kujua nani ni nani ndani siku hizi mbili ndani au nje balaza linapotangazwa.