Mto Songwe
JF-Expert Member
- Jul 17, 2023
- 6,683
- 14,060
Chukua hii kwa ufupi:
Nchi ya China inayopatikana mashariki ya mbali ya bara la Asia.
Hii ni nchi moja yenye serikali mbili zilizo katika mgogoro wa vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo havijatamatika toka 1949 mpaka sasa.
Katika nchi ya China kuna serikali mbili zinazo ng'ang'ania mamlaka ya kutawala China moja au yote.
Serikali hizi ni Jamhuri ya China inayopatikana katika visiwa vya Taiwan na serikali ya Jamhuri ya watu wa China inayopatikana bara.
Asili ya vita hivi vya wenyewe kwa wenyewe ni mapinduzi ya wakomunisti wa China ambao kwa sasa wanaunda serikali ya Jamhuri ya watu wa China kuingia vitani na serikali ya Jamhuri ya China ilivyokuwa inatawala sehemu kubwa ya China kwa wakati huo chini ya chama cha Kuomintang.
Vita vyao vilipiganwa kwa muda mrefu mpaka pale wakomunisti walipotwaa maeneo ya China bara na kusimika Jamhuri ya watu wa China na serikali Jamhuri ya China kukimbilia kisiwani jambo lililowapa ugumu wakomunisti kwa wakati huo kuweza kabisa kuishinda Jamhuri ya China na kuiangusha moja kwa moja.
Mara kwa mara wakomunisti wamekuwa wakijipanga kuiangusha kabisa Jamhuri ya China nayo Jamhuri ya China kwa mara kadhaa imejaribu kutaka kutwaa tena madaraka ya China yote.
Kifupi mpaka sasa China ipo vitani wao kwa wao muda wowote wakishindwa kufikiana tamati kwa njia ya amani basi mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yataibuka tena China kati ya Jamhuri ya China na Jamhuri ya watu wa China( wakomunisti).