China hana ubavu wa kuanzisha vita na US ya maneno sawa lakini sio vita kamili ya silaha kufika hapo alipo china kasota sana so hawezi kubali kurudi mavumbini. Tulijionea hapa wakati Nancy Pelosi akisema lazima aende Taiwan China ikapiga sana kelele kusema asicheze na moto .Bibie Nancy akaenda Taiwan na akalala vizuri kabisaaa na akaondoka vizuri kabisaaa.Nafikiri unaizungumzia Jamhuri ya watu wa China ?
Sio kweli kuwa Jamhuri ya watu wa China inaihofia U.S maana kwa sasa U.S sio tishio kijeshi kwa Jamhuri ya watu wa China kama ilivyokuwa miaka ya 50 ninaweza sema Jamhuri ya watu wa China inajaribu kusogeza mbele muda ili kuona maafikiano ya amani baina yake Jamhuri ya watu wa China na Jamhuri ya China kama yatafikiwa.
Maafikiano ya amani yasipo fikiwa kuna asilimia kubwa kuzuka vita baina ya hizi serikali mbili katika muendelezo wa kugombania utawala wa China
Ndiyo maana hata mgogoro wa urusi na ukraine china yupo makini sana hata israel na palestine napo yupo makini mno.
Kuwa US ni tishio kwa china kijeshi hilo halina ubishi labda mtu aamue tu kuweka ubishi wa kitoto.
1.Unaongelea nchi yenye base za kijeshi sehemu mbalimbali duniani.
2.Unaongelea nchi ambaye imepigana vita kadhaaa mpaka vya nyuklia
3.Unaongelea nchi yenye watafiti wa dhana za kivita bora kabisa duniani.
4.Unaongelea nchi ambayo vita ndiyo DNA yake.
Unaongelea nchi inayoweka bajeti kubwa mno ya jeshi kila mwaka.
Obvious huwezi linganisha hii nchi na nchi kama China. Ndiyo China kapiga hatua kubwa sana kimaendeleo na kijeshi lakini siyo za eti kupambana kijeshi na kuishinda US.