Nchi nyingi nilizotembelea mikate ni chakula ila huku kwetu ni kitafunwa

🤣 🤣 🤣 pole. Now you know.

Jiandae kula mikate asubuhi, mchana na jioni wanabadilisha majina tu; burger, hotdog, pizza, sandwich yote ni mikate tu.
Kabisa burger na hotdog ni mkate ,wanacheza na majina tu
 
Nilishangaa nigeria kuna ugali, tena ugali kwa mlenda, nilijua ni tanzania tu ndio wanakula ugali kumbe hata nchi za afrika magharibi ugali upo. Huenda ugali ukawa ni chakula maarufu duniani.
jioni ya leo sina hamu ya kula ugali au wali, nakula mkate kwa juisi nilale. Nikikosa mkate nakula matunda sahani imejaa inatosha
 
Hata hapa bongo watu wanashindia mkate ila hali ya kiuchumi ikiyumba.
Nimeshuhudia chuo kikuu watu wakishindia mkate
 
Sema Mkuu huku Tz Maisha magumu Sana that way tunaishia kula ugali.
Siyo umasikini hata kidigo! Chakula ni sehemu ya utamaduni. Nilicheka sana nilipokuwa namsikiliza Rais wa Burundi wakati anahojiwa na BBC ni chakula Gani anakipenda alijibu maharage!
Kuna Ndugu yetu alikuwa china kusoma, Kuna wakati tulimtumia unga wa Dona Ili apike ugali maana alikosa hata Raha ya kuishi huko.
 
WATu tushakula ugali na wali kama mboga wewe mkate tu makelelehumu😁
 
Ni kweli,
 
chakula ni contenti sio Quantity,Kwa wenzetu mkate unaandaliwa kwa kuwekwa mayai,Maziwa kisha wakati wa mlo huambatana na mboga za majani au nyama kisha hushushiwa na matunda Au juice.Huu ni mlo kamili ila Sisi mpaka upate kitu kizitoooo.
 

Hata huku ni chakula, labda kwenu tu ndo vitafunwa
 
Wanaokula mikate ndio wenye akili kuliko wanaokula ugali
 
Niliiona hii nilicheka kinoma nikaimagine yaani daa eti yaani kwenye mlo usipoweka maharage haelewi isee inawezekana mwamba akija kwenu halafu anuse harufu ya ndondo na hamjampa anaondoka anasikitika daa wameamua kuninyima maharage powa tu!
 
Tatizo la nguvu za kiume halipo ila wafanyabiashara wa mitishamba walitengeneza liwe tatizo ili wapige hela kwa kulitangaza sana.

Vilevile kama umenotice kitu currently kuna wahuni wana advocate" Mental Health" kwa kufanya ionekane kuwa ni tatizo kubwa linalohitaji intervention wakati hata halipo watu wanatafuta namna ya kupiga hela za watu.

Rejea namna mafuta ya wanyama yalivyopigwa vita na watengenezaji wa mafuta ya mimea enzi hizo utabaini trend ilivyo.

Usicheze na wajasiriamali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…