Nchi nzima wananchi wameongeza chuki dhidi ya Chama cha Mapinduzi (CCM)

28 Aug 2021
Dar es Salaam, Tanzania

James Mbatia Jeshi La Polisi Wameota Masharubu

Mwenyekiti Wa Chama Cha Nccr Mageuzi James Mbatia Jeshi La Polisi Wameota Masharubu, Wametuvuruga,tuna Hasira Sana,ubabe Huu Hauvumiliki
Source : Mubashara Studio
 

Wenyewe wanasema huko ndiko kupendwa sasa:

 
Mambo ni Bam Bam
 
14 August 2020
Hai, Kilimanjaro
Tanzania

Madhara ya Marufuku ya Siasa kwa miaka 5 imesababisha CCM kukosa uvumilivu wa kisiasa na kutishia machafuko nchini
Kufuatia kupigwa marufuku shughuli
za kisiasa Tanzania sasa tunaona madhara yake katika maeneo fulani. Na athari zake zimekuwa kubwa kabisa kwa upande wa CCM kwa wanachama, makada, wafuasi na wapenzi wake kukosa kufuata sheria, jadi , kawaida ya waTanzania kushindanisha hoja kwa kutumia ushawishi na kubaki na ulemavu wa kifikra kuamua kutumia nguvu na mabavu.

Video : Tukio la wanaCCM jimbo la Hai mkoani Kilimanjaro

Shughuli za kisiasa zilitumika kutoa elimu ya kiuraia kuwajenga Watanzania kuamini katika kupiga kura ndiyo njia sahihi ya kumkataa mwanasiasa fulani baada ya kusikiliza hoja zake.

Lakini sasa tunaona baada ya viongozi wa juu wa nchi mwaka 2016 kuamua kuachana na haki hiyo ya msingi kabisa ya kikatiba kwa kupiga marufuku shughuli za kisiasa sasa baadhi ya waTanzania nao wameonesha wamekosa uvumilivu na kupoteza ufahamu kuwa huwezi kumpiga marufuku mwanasiasa fulani kufika eneo lako kisa mnatofautiana ktk mitizamo ya kiitikadi na mpo chama tofauti.

Tuliyoyaona kule wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro ni matunda ya serikali ya CCM Mpya kupiga marufuku viongozi wa vyama vya upinzani kufika maeneo fulani kwa miaka 5 sasa, sababu watawala wa CCM wanadai mbunge wa chama fulani siyo eneo lake la kibunge au kuwa uchaguzi umeisha hivyo hakuna kuendelea kufanya siasa za hoja kujenga ushawishi.

Katiba ya nchi iliona mbali kuwa ruhusa ya kufanya siasa ni afya kwa utulivu wa nchi ili ikifikia kipindi cha kampeni waTanzania wasiwe wabaguzi wa kisiasa au kimaeneo bali wawe na ufahamu wa kufanya maamuzi kupitia sanduku la kura.

Tumeona wanaojiita wanaomtetea Magufuli kuwa hawataki kuona watu wengine wanafika maeneo yao kwa kuwa hawajawaona kufika huko kwao, bila kufahamu kuwa wanasiasa hao wa upinzani walipigwa marufuku.

Na kuthibitisha wanaigiza tabia za viongozi wa juu wa serikali ya CCM Mpya wamejaribu na wao kufanya jaribio la mwendelezo haramu wa marufuku kwa kufunga barabara, kufanya vurugu na kupandisha mabango ya shutuma kuwa wanasiasa wa vyama vingine ni mabeberu, vibaraka wa wazungu n.k

Hii siyo afya nzuri kwa siasa za Tanzania kwa wananchi kuacha kutumia sanduku la kura kufanya uamuzi na kuamua kutumia njia zingine sisizotambulika kupeleka ujumbe hawataki uchaguzi, wagombea wa vyama vingine na kampeni za kisiasa.

Kama nilivyojaribu kufafanua haya ndiyo matunda na matokeo ya kuminya siasa kufanyika, kuzuia midahalo, kuzuia kutoa maoni ktk vyombo vya habari, asasi za kiraia NGO, kuwaumiza wapinzani na sasa vikundi vya watu huko Hai Kilimanjaro wameamua kuiga vitendo vya serikali na watawala wa CCM Mpya kujichukulia sheria mikononi, kupuuza haki za mtanzania na mwanasiasa kujumuika na waTanzania wa mikoa, wilaya na majimbo mengine kufanya shughuli za kisiasa.

Hali hii isipodhibitiwa na serikali ya CCM nchi itakuwa haifuati utawala wa sheria na katiba kuanzia ngazi za viongozi waliopo ktk nafasi za uongozi wa dola na mpaka mitaani kama tulivyoona kwa baadhi ya wananchi wa wilaya ya Hai.

Nadhani hili tukio la watu kukosa uelewa wa haki za kiuraia za kwao na za wengine kufanya shughuli za kisiasa, wasomi na wazoefu kama Mzee Pius Msekwa wataona walikosea kuunga mkono kuzuia shughuli za kisiasa na kuwa ni hatari kwa usalama wa nchi pia kinyume na vile walivyofikiria wakati walipounga mkono marufuku ya kufanya siasa baada ya uchaguzi kuisha 2015.

Published on 10 Jul 2018
Video hii ikimuonesha mmojawapo wa thinktank ya CCM Mpya ikimuunga mkono Magufuli kupiga marufuku shughuli za kisiasa
Pius Msekwa: Hauoni kwamba kuzuia mikutano ya hadhara ni kuuwa upinzani?, Sumaye alinihoji

 
Hapana mzee. Mama kaibgizwa chaka. Hii bajeti ni ya mwenda zake pesa alitapanya kwa kuhonga ashinde uchaguzi. Ziliisha na haya ndio madhara yake
Unajifariji kwa kulitetea hilo bogus la zenji ndipo akili zilipoishia
 
Unajifariji kwa kulitetea hilo bogus la zenji ndipo akili zilipoishia
Hahaha mbona mna hasira naye sana. Huyu amepanda vyeo step by step hadi kufikia Makamu wa Rais. Hawezi kuwa Bogus
 
sisiemu imefahamika ndio wanalea na kukuza magaidi nchini.
 
Nakuomba radhi Hamza kwa kukuweka katika kundi la waoga. Wewe hauko katika kundi hili.
Vyovyote unakavyoisema bado maana ni ileile. Watanzania ni wachoyo sana. Hakuna mtu anataka kujitoa kafara kwa ajili ya nchi. Ngoja CCM na serikali yake waendelee kutupiga per rectal (PR) fingers.
 
30.08.2021
Dar es Salaam, Tanzania

KESI YA MBOWE DHIDI YA MWANASHERIA MKUU, DPP NA IGP NGOMA NGUMU UWAMUZI KUTOLEWA TAREHE 25 SEP 2021


Source : CHADEMA MEDIA TV
 
30.08.2021
Mahakama Kuu ya Tanzania
Kivukoni Front
Dar es Salaam, Tanzania

VILIO NJE YA MAHAKAMANI, KESI YA FREEMAN MBOWE YAAHIRISHWA


Source: Wasafi Media
 
Tup
Tupe andiko ,au umetoa kijiweni tu.Elimu !!Elimu!!
 
30 August 2021
Dar es Salaam, Tanzania

WAFUASI WA CHADEMA WAANGUA VILIO MAHAKAMANI KESI YA MBOWE


Source : Bongo5
 
Nachoshukuru polisi nao wapo kwenye tozo wanapelekwa kama mapunda kama wao hawajui kulinda raia na mali zao ni jukumu lao
Daah mzee zile kazi acha tu. Hivi tunavyowaogopa wakiwa na marungu na mabunduki ndivyo na wao wanaogopa kusema "SU" Kwa mabosi wao.

Sio kwamba na wao wanapenda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…