CCM Asilia ikitaka kurejesha utengamano nchini, inabidi itambue CCM Mpya ilivyokengeuka na ijisahihishe. Ili kurejesha imani kwa waTanzania inapata kuelewa haya yafuatayo :
Katika vyama vyote vya siasa vilivyosajiliwa Tanzania kwa muda huu 2021, CCM ni chama dhaifu kupita vyote hata cha CHAUMA chini ya mwenyekiti mzee Hashim Rungwe ni chama thabiti kuliko CCM.
Sababu ni kuwa mwendazake baada ya kuua mihimili ya dola, mahakama na bunge akamalizia kukimaliza chama kilichomweka madarakani. Muda huu CCM haina Mwenyekiti wa Taifa wala Katibu Mkuu wa chama.
Hali hii imefikiwa kwa vile CCM ilishindwa kumdhibiti mwendazake kufanya mambo yake ya kuwaondoa vigogo tishio ndani ya CCM na kuleta "wageni" na kuwazawadia vyeo kwa sharti wamuimbie mapambio anayopenda kusikia.
Kina Bashiru Ally Kakurwa, Humphrey Polepole ni aina ya viongozi ambao viongozi walikuwa hawawezi kumuambia chochote Mwenyekiti ambacho wao wanaamini kinyume na kama kina Nape Nnauye , January Makamba na hata wazee kama Yusuf Makamba, Abdulrahman Kinana.
Tukija katika dola, mwendazake aliiyumbisha na kuivuruga kabisa mfumo wa utumishi serikalini yaani civil service. Aliwachukua watu wasio na ujuzi wa utumishi serikalini na kuwapachika vyeo vya u DED, Makatibu Wakuu na kujaribu kuhitimisha pigo kuu la kuua utumishi serikalini kwa kumuapisha Dr. Bashiru Ally Kakurwa kama Katibu Mkuu Kiongozi ambaye ktk historia ndiye Katibu Mkuu aliyekuwa hana uzoefu kabisa ktk utumishi wa serikali kuu.
Tukija katika mhimili wa Mahakama tuliona alivyouburuza na kuwapa vyeo vya ujaji kwa vigezo dhaifu mfano kuandika hukumu kwa kiSwahili huku kesi hiyo ikiwa ni nyepesi mno.
Bunge pia lilipelekeshwa kwa Spika kuelekezwa kuwashughulikia wabunge wake kwa kuwatoa nje ili waje kushughulikiwa na mwendazake nje ya Bunge. Wabunge wa CCM pia hawakuepuka kipigo cha kisiasa toka kwa mwendazake, ktk kuelekea uchaguzi wa 2020 walishughulikiwa na 'wajumbe' na kama waliweza kupenya walikutana na rungu la Mwenyekiti wa CCM.
Vyeo katika ngazi za uwaziri tumeona waliojiunga mwishoni ktk CCM toka vyama mbadala walitunikiwa vyeo huku wale waliokulia ktk UVCCM na Jumuiya za CCM toka utotoni wakiambulia kuwa backbenchers. Yote hii ilikuwa kuonesha CCM imekufa na sasa mtu mmoja ndiyo kila kitu hivyo wasifurukute au kuwashwa kuhoji au kutoa mawazo mbadala.
Tanzania ilikuwa inaelekea kubaya, lakini kama uzi huu ulivyotabiri wa mwana JF Mvuv, inaonekana ndani ya CCM ndiyo kulikuwa na fukuto kubwa la kutokubaliana na kinachoendelea na sasa tunasikia baada ya mwendazake kuondoka, wabunge wa CCM na SPIKA mwanaCCM wanaanza kutoa maoni ambayo yanaonekana na waimba pambio wa mwendazake kuwa ni unafiki.
Ili kuirejesha Tanzania katika mstari wa haki ikiwemo na CCM yenyewe Asilia kuweza kuaminika kusimamia haki na katiba ya nchi, Tume ya Kijaji lazima iundwe.
Tume ya KiJaji ipewe hadidu rejea Kuchunguza ukiukwaji mkubwa wa katiba, haki za binadamu na ukatili uliotendeka ktk utawala wa CCM iliyojiita CCM Mpya.