Nchi nzima wananchi wameongeza chuki dhidi ya Chama cha Mapinduzi (CCM)

Nchi nzima wananchi wameongeza chuki dhidi ya Chama cha Mapinduzi (CCM)

1626528026102.png
 
Unaelewa hata nazungumzia kitu gani?

Unaelewa kuwa huko Mwanza leo Chadema wamezuiwa kwa virungu kufanya mkutano wao wa ndani wa mambo ya katiba ambao ni haki yao ya kikatiba na mpaka sasa hivi watu 128 wamekamatwa na kuwekwa ndani wakati Shaka anachanja mbuga kufanya mikutano ya hadhara?

Narudia tena,waliokuwa wanaiita takataka kuwa ni 'Mama' shame on you!
View attachment 1856958
Hapa ni wapi?
 
Kwa sisi tuliofatilia hali ya kisiasa na kijamii kuanzia kuingia kwake madarakani 2015 na uchaguzi wa muhula wa pili 2020 tulijua kabisa na kubashiri janga linaloenda kuikabiri nchi yetu.

Kwa sisi tulioona na kushuhudi uhuni ule wa uchaguzi, matumizi mabaya ya fedha kudhibiti Haki na demokrasia nchini tulijua kabisa baada ya uchaguzi hali ya kiuchumi itakuwa mbaya sana. Nyote ni mashuhuda sasa.

Nchi nzima si wanaccm, chadema wala Chauma. Si wanasiasa hadi wasio na siasa wote wameichukia ccm hasa iliyokita mizizi na fikra za John Pombe magufuli, fikra za kikandamizaji.

Kwa wale tuliosikia zile tetesi kwamba Hayati alikodisha vikosi vya cyber kuja kuchakachua mifumo mingi ya kiteknolojia na internet ili kurahisisha mazingira ya kushinda uchaguzi tuliwaza kabisa kuwa kama ni kweli hizo pesa anazowalipa zinatoka wapi? au ndio amekomba pesa zote za hazina? Kuna wengine wanafika mbali na kusema huenda pesa alizokopa world bank na Uchina kwa ajili yanujenzi wa SGR na Stigler ndio hizo zilitumika ktk mikakati michafu ya uchaguzi october 2020 na hivyo tunalipa ghalama.

Sasa Awamu ya sita imetuchanganya. Huwezi kumjua Mpiga mapambio wa zamani na mpinzani wa zamani. Wote wamekuwa kitu kimoja. Adui wao amekuwa mmona tu, naye ni CCM.

Asante sana CCM kqa kutuunganisha. Sasa ongeza na tozo zingine ili tujenge nchi kwa haraka zaidi.

CCM nambali one.
Maza nchi imemshinda kabisa hakuna la maana anafanya
 
Unaelewa hata nazungumzia kitu gani?

Unaelewa kuwa huko Mwanza leo Chadema wamezuiwa kwa virungu kufanya mkutano wao wa ndani wa mambo ya katiba ambao ni haki yao ya kikatiba na mpaka sasa hivi watu 128 wamekamatwa na kuwekwa ndani wakati Shaka anachanja mbuga kufanya mikutano ya hadhara?

Narudia tena,waliokuwa wanaiita takataka kuwa ni 'Mama' shame on you!
View attachment 1856958
Huyu maza kweli ni takataka atasababisha vita aisee
 
😂😂😂😂😂

Hapana mzee. Mama kaibgizwa chaka. Hii bajeti ni ya mwenda zake pesa alitapanya kwa kuhonga ashinde uchaguzi. Ziliisha na haya ndio madhara yake
 
Mi nikiwa mwananchi mzalendo nasema EE MWENYEZI MUNGU ENDELEA KUTUTUNZIA AMANI KATIKA NCHI YETU.Kumbukeni syria,libya,nigeria,congo,somalia nk tafadhali
 
CCM Asilia ikitaka kurejesha utengamano nchini, inabidi itambue CCM Mpya ilivyokengeuka na ijisahihishe. Ili kurejesha imani kwa waTanzania inapata kuelewa haya yafuatayo :

Katika vyama vyote vya siasa vilivyosajiliwa Tanzania kwa muda huu 2021, CCM ni chama dhaifu kupita vyote hata cha CHAUMA chini ya mwenyekiti mzee Hashim Rungwe ni chama thabiti kuliko CCM.

Sababu ni kuwa mwendazake baada ya kuua mihimili ya dola, mahakama na bunge akamalizia kukimaliza chama kilichomweka madarakani. Muda huu CCM haina Mwenyekiti wa Taifa wala Katibu Mkuu wa chama.

Hali hii imefikiwa kwa vile CCM ilishindwa kumdhibiti mwendazake kufanya mambo yake ya kuwaondoa vigogo tishio ndani ya CCM na kuleta "wageni" na kuwazawadia vyeo kwa sharti wamuimbie mapambio anayopenda kusikia.

Kina Bashiru Ally Kakurwa, Humphrey Polepole ni aina ya viongozi ambao viongozi walikuwa hawawezi kumuambia chochote Mwenyekiti ambacho wao wanaamini kinyume na kama kina Nape Nnauye , January Makamba na hata wazee kama Yusuf Makamba, Abdulrahman Kinana.

Tukija katika dola, mwendazake aliiyumbisha na kuivuruga kabisa mfumo wa utumishi serikalini yaani civil service. Aliwachukua watu wasio na ujuzi wa utumishi serikalini na kuwapachika vyeo vya u DED, Makatibu Wakuu na kujaribu kuhitimisha pigo kuu la kuua utumishi serikalini kwa kumuapisha Dr. Bashiru Ally Kakurwa kama Katibu Mkuu Kiongozi ambaye ktk historia ndiye Katibu Mkuu aliyekuwa hana uzoefu kabisa ktk utumishi wa serikali kuu.

Tukija katika mhimili wa Mahakama tuliona alivyouburuza na kuwapa vyeo vya ujaji kwa vigezo dhaifu mfano kuandika hukumu kwa kiSwahili huku kesi hiyo ikiwa ni nyepesi mno.

Bunge pia lilipelekeshwa kwa Spika kuelekezwa kuwashughulikia wabunge wake kwa kuwatoa nje ili waje kushughulikiwa na mwendazake nje ya Bunge. Wabunge wa CCM pia hawakuepuka kipigo cha kisiasa toka kwa mwendazake, ktk kuelekea uchaguzi wa 2020 walishughulikiwa na 'wajumbe' na kama waliweza kupenya walikutana na rungu la Mwenyekiti wa CCM.

Vyeo katika ngazi za uwaziri tumeona waliojiunga mwishoni ktk CCM toka vyama mbadala walitunikiwa vyeo huku wale waliokulia ktk UVCCM na Jumuiya za CCM toka utotoni wakiambulia kuwa backbenchers. Yote hii ilikuwa kuonesha CCM imekufa na sasa mtu mmoja ndiyo kila kitu hivyo wasifurukute au kuwashwa kuhoji au kutoa mawazo mbadala.

Tanzania ilikuwa inaelekea kubaya, lakini kama uzi huu ulivyotabiri wa mwana JF Mvuv, inaonekana ndani ya CCM ndiyo kulikuwa na fukuto kubwa la kutokubaliana na kinachoendelea na sasa tunasikia baada ya mwendazake kuondoka, wabunge wa CCM na SPIKA mwanaCCM wanaanza kutoa maoni ambayo yanaonekana na waimba pambio wa mwendazake kuwa ni unafiki.

Ili kuirejesha Tanzania katika mstari wa haki ikiwemo na CCM yenyewe Asilia kuweza kuaminika kusimamia haki na katiba ya nchi, Tume ya Kijaji lazima iundwe.

Tume ya KiJaji ipewe hadidu rejea Kuchunguza ukiukwaji mkubwa wa katiba, haki za binadamu na ukatili uliotendeka ktk utawala wa CCM iliyojiita CCM Mpya.
 
Back
Top Bottom