CCM ni adui wa kula mwenye akili timamu na wasema kweli pamoja na wanaotetea Haki na usawa wa raia tangia enzi za TANU&ASP na baadaye CCM tokea 1977.Kuthibitisha hilo,tazama na kusoma comments za watetezi wa CCM humu jukwaani,hawana uwezo wa kujenga hoja,wanatukana na kukejeli hoja zote za Watanzania wasema kweli na watetezi wa Haki za raia, Ukitetea Haki za Wananchi watakuita wakala wa mabeberu au mpinzani has a CHADEMA.
Ukidai Katiba Mpya unaitwa CDM,ukidai Haki unaitwa mpinzani;Je,CCM na serikali yake wanamwakilisha nani?Wanapotetea wanyonge huwa wanawatetea dhidi ya wapinzani au mabeberu?Hivi hao mabeberu huwa ni akina nani kwa mujibu wa CCM?Hivi nchi yetu ilipata Uhuru wake wa kweli au tulipewa bendera?
CCM kama chama cha siasa imewezesha nini kwa uwepo wake madarakani kwa miaka 60 iliyopita?Nchi yenye raslimali kama Tanzania kuwa tegemezi,omba omba na kutegemea wahisani kwa karibia kula kitu huku viongozi wakiishi kifahari na matumizi makubwa kwenye mambo yasiyo na tija?Watanzania wanagharamia afya,elimu,Maji,umeme nk.kwa kulipia makato na michango ya lazima.Je,kodi wanayolipa ni kwa ajili ya kustarehesha watawala?
Ah,hata maswali hayatajibiwa.Niishie halo kwa sasa.Ila anayeiunga mkono CCM na watu wake anatakiwa kupimwa akili.Siyo kwa mateso haya!