Unfortunately, "international relations" (as in diplomacy) doesn't work that way. Vinginevyo nchi kama Saudi Arabia au Misri zingesuswa na mataifa ya Magharibi. Mahusiano ya kimataifa huangalia zaidi maslahi kuliko siasa za ndani. Angalia wawekezaji wanavyomiminika Rwanda licha ya rekodi isiyopendeza ya haki za binadamu nchini humo. Angalia Nigeria, je imesuswa kwa sababu ya Boko Haram? Tena hao Wamarekani na Waingereza ukitaka uswahiba nao, waambie unapambana na ugaidi, watamwaga misaada kama hawana akili nzuri.