Nchi yenye watu wenye rangi, dini au kabila tofauti inaweza kustawi?

Nchi yenye watu wenye rangi, dini au kabila tofauti inaweza kustawi?

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
9,189
Reaction score
16,128
Hivi inawezekana kwa nchi yenye watu tofauti ikastawi. Maana kwa kuangalia harakaharaka naona nchi karibu zote ambazo zina usalama na zimeendelea ni zile ambazo watu wa rangi, dini na lugha moja wanakaa pamoja.

Kuna exceptions chache sana. Ni kama haiwezekani kwa nchi yenye diversity kubwa kuendelea. Pia naona ni kama haiwezekani kwa demokrasia kufanya kazi kwa nchi ambayo watu wana rangi, dini na lugha tofauti.

Inawezekana kujenga taifa imara na lenye kustawi kwenye nchi ambayo ina watu wenye dini, lugha na makabila tofauti?
 
Toa mifano ili ueleweke zaidi!

Au ungekuja na mfano kama huu

Mahali pamejaa wenyeji tupu na mahali ambapo pamechanganyika! Ni mahali gani ambapo patastawi kwa haraka?

Mungu hajawahi kuwa mjinga aisee!

Kunapokuwa na tofauti tofauti za kabila na hata dini tofauti! Kwa sababu tu wengi huwa hatuna wivu wa maendeleo na badala yake dini/kabila zimejaa vinyongo na roho ya kwa nini wao na sio sisi!

Lakini ingelikuwa kila dini /kabila zijawe na wivu wa kwa nini sisi hatusomi tukafika mbali na kwa nini palipo wao maendeleo yapo pia?

Tungelifika mbaali kwa haraka mno
 
Wee jamaa unaakili kubwa sana, umefikiria kutu ambacho sijawahi kuwaza👊haiwezekani mkuu kujenga nchi ikastawi ndani ya watu wenye mitazamo tofauti.

Mfano ni humu jukwaani watu wanashinda wakibishana kuhusu dini, ukabila, ukanda nk..

Kwawenzetu unakuta nchi nzima ni wakristo tuu au waislamu tuu, Hawa wakitaka Jambo lao linawezekana sababu wanaongea lugha moja...

Sisi niwale fungulia mbwa kila mtu na Jambo lake. Hawa wanaamini hivi wale wanaamini vile, vurugu tupu.

Hatuwezi kufika popote.
 
Mbona China imeendelea sana ?!
Asilimia kubwa ni Wahan. na maeneo yaliyoendelea sana ni ya wahan. Wanapata shida kwenye maeneo ya watibet na wa-Uighur na waislamu. Wanachofanya ni kupeleka wahan wengi huko ili kupata homogeinity. Diversity inawapa shida sana.
 
Hivi inawezekana kwa nchi yenye watu tofauti ikastawi. Maana kwa kuangalia harakaharaka naona nchi karibu zote ambazo zina usalama na zimeendelea ni zile ambazo watu wa rangi,...

Mbona US imezewekana, au hujui unachoongea ndugu?
 
Hivi inawezekana kwa nchi yenye watu tofauti ikastawi. Maana kwa kuangalia harakaharaka naona nchi karibu zote ambazo zina usalama na zimeendelea ni zile ambazo watu wa rangi...
Umetoa wazo linalofikirisha sana lenye ukweli ndani yake japo siyo kwa 100%, lakini lina ukweli kwa kama 80%
 
Mbona US imezewekana, au hujui unachoongea ndugu?
USA imekuwa ni nchi ya wazungu wakristo kwa sehemu kubwa ya historia yake. Weusi wamekuwa ni watumwa na baadaye raia daraja la pili. Wahindi ni kama wameuliwa wote.

Miaka ya karibuni imekubaliana na mchanganyiko wao. Siasa zao zimebadilika kabisa. Zimekuwa za kibaguzi za kubomoa nchi. Pengine ndiyo sababu inaporomoka.
 
Mbona US imezewekana, au hujui unachoongea ndugu?
USA imeendelea muda mrefu wakati races nyingine zikiwa treated like sub humans. Baada ya kuendelea ndiyo inaruhusu hawa wengine nao wapate haki sawa na White Christians japo siyo kwa 100%.

Jamaa ana point. Worldwide trend ya maendeleo ni kwa nchi zilizo ethinic and religious homogeneous. Au kwenye hiyo nchi kuwe na dominant ethinic group ambao watawapeleka mputa mputa wengine wasio wenzao bila kujali kama wapo...mfano Singapore ethinic Chinese ndiyo kila kitu na the way Lee alivyowapelekesha ni kama vile hakujali kuna ethinic Malayans au Indians
 
Halimradi tuna heshimiana.

Halimradi tuna heshimu mila na desturi za kikabila.

Halimradi tuna heshimu mila na desturi tulizo ziweka kwa pamoja kufikia azma hiyo.

Ni changamoto, na tunajua hivyo, mfano mzuri ni Marekani, ambapo ndoto hiyo ya Ustawishaji wa makabila, Unaendelea.
 
Umewaza vema kabisa. Na Tanzania hatutakuja tuwe na maendeleo ya maana
 
Ilijengwa wakati huo wakiwa wengi ni wenyewe tu. Siku hizi wameingia wasomali, waafhuganistan, wasyria, na wengine hakuna hatua kubwa wanazofanya na ndiyo maana China inakuwa tishio la kuipiku USA
 
Hivi inawezekana kwa nchi yenye watu tofauti ikastawi. Maana kwa kuangalia harakaharaka naona nchi karibu zote ambazo zina usalama na zimeendelea ni zile ambazo watu wa rangi, dini na lugha moja wanakaa pamoja.

kuna exceptions chache sana. Ni kama haiwezekani kwa nchi yenye diversity kubwa kuendelea. Pia naona ni kama haiwezekani kwa demokrasia kufanya kazi kwa nchi ambayo watu wana rangi, dini na lugha tofauti.

Inawezekana kujenga taifa imara na lenye kustawi kwenye nchi ambayo ina watu wenye dini, lugha na makabila tofauti?
Inawezekana endapo tu, pale juu litakaa kundi linalojielewa. Tutalipataje hilo kundi? Katiba mya. Tukae tujadili namna gani tutalipa kundi la pale juu, tukishajadili tuliweke kwenye katiba. Umeongea mada nzito, fikirishi mana kwenye wengi, kelele nyingi hakuna maelewano hakuna kusonga mbele labda awepo dicteta mpole vinginevyo ni mkorogo.
 
Ila hata huko Marekani imegawanyika sana kiitikadi tangu zamani wakati wanapata uhuru na wakati wa kuandika katiba mpya kati ya majimbo ya Kusini(red states) na ya Kaskazini(Blue states) hadi waliamua kutoondoa utumwa kabla ya Abraham Lincoln ili majimbo ya kusini yasijitenge.
 
Toa mifano ili ueleweke zaidi!

Au ungekuja na mfano kama huu

Mahali pamejaa wenyeji tupu na mahali ambapo pamechanganyika! Ni mahali gani ambapo patastawi kwa haraka?

Mungu hajawahi kuwa mjinga aisee!

Kunapokuwa na tofauti tofauti za kabila na hata dini tofauti! Kwa sababu tu wengi huwa hatuna wivu wa maendeleo na badala yake dini/kabila zimejaa vinyongo na roho ya kwa nini wao na sio sisi!

Lakini ingelikuwa kila dini /kabila zijawe na wivu wa kwa nini sisi hatusomi tukafika mbali na kwa nini palipo wao maendeleo yapo pia?

Tungelifika mbaali kwa haraka mno
Point
 
Back
Top Bottom