Nchi za Afrika za Francophonie na Common wealth zinalipa Trillion 3000 kila mwaka kwa Ufaransa na Uingereza kama fidia ya faida za ukoloni

Nchi za Afrika za Francophonie na Common wealth zinalipa Trillion 3000 kila mwaka kwa Ufaransa na Uingereza kama fidia ya faida za ukoloni

Tofauti yangu na wewe ni kwamba wewe unalaumu Wafaransa wana mikataba ya siri mibaya ambayo Waafrkka hawawezi kujiondoa wakijiondoa wanauawa.

Mimi nasema mikataba hiyo ya CAF/Ufaransa iko wazi inajulikana na tatizo ni viongozi wa Afrika wanaoangalia interests zao zaidi ya za Wafaransa.

Achana na hao Wafaransa, Thabo Mbeki rais msomi wa Afrika ya kusini, aliyeanzisha idea ya "African Renaissance", idea ya kuirudisha Africa katika kujitambua na maendeleo, alitia saini mkataba wa doka bili9ni 10 za kampuni ya BAE ya Uingerwza kuhusu manunuzi ya sioaha (dellal kama la radar enzi za Mkapa, na kampuni ile ile).

Thabo Mbeki alijua kuwa BAE imezidisha bei ya silaha kwa mara mbili na nusu, na Afrika ya Kusini haikuhitaji hizo silaha. Na kwamba hizo hela ni nyingi sana na zingeweza kutumika kwenyw shughuli nyingi sana za kijamii, including kusaidia kupigana na HIV/AIDS South Africa.

Lakini Thabo Mbeki aliamua kununua sulaha kwa sababu tu wazee wa ANC walikuwa wanapewa rushwa ya dola za Marekani milioni 300 ambazo walitaka kuzitumia kwenye uchaguzi.

Tanzania tulipigwa deal kama hilo kwenye ununuzi wa radar mpaka Claire Shirt akaibana BAE tukarudishiwa sehemu ya hela.

Na hapo itaona Tanzania na South Africa hazijatawaliwa na Ufaransa.

Sasa hapo utasema tatizo ni Wafaransa au viongozi wa Africa?

Tafuta documentary inaitwa "Shadow World : Inside The Global Arms Trade" uangalie jinsi biashara ya silaha ilivyogubikwa na rushwa na jinsi viongozi wa Afrika wanavyojiingiza kwenye hii rushwa kwa hiyari yao wenyewe.

View: https://youtu.be/aT6Xhkdrq8M?si=fQvWWbzYppLJHBju
 
Usiende Mbali Tanzania hii kuna Mgodi umejazwa maji na kutiwa SUMU. Wakoloni walikasirika kufurushwa. Wamekuja Waturuki na Wachina wameushindwa wametoa ripoti kwamba maji na Sumu yaliyojazwa kwenye huo Mgodi ukiyavuta kuja Nchi kavu yataathiri vyanzo vyote vya Nchi kavu na watu watapoteza Maisha.

Mgodi Upo Mpanda Mjini Mkoa wa Katavi eneo la Kampuni. Reli ya kutoka Tabora Mpanda inaishia ndani ya Mlima/Handaki la Mgodi huo wa Dhahabu. Afrika tumeonewa sana na makaburu.
Naupata huo mgodi mkuu.
 
1. Benki kuu za nchi hizo zinatakiwa (sio ombi, ni amri) kuweka asilimia 50% ya hazina yake yote katika benki za ufaransa.
Na serikali ya ufaransa ina haki zote za kutumia pesa hizo bila ruhusa kutoka nchi husika.
Pia ndio maana pesa zao (nchi nyingi Afrika magharibi: Senegal, ivory coast, mali, benin, niger, burkina faso etc) zinaitwa CFA Franc.

2. Right of First Refusal.
Ufaransa kama koloni lao la zamani wana haki ya kukataa kwanza kwa uwekezaji wowote ule unatakiwa kufanywa katika nchi hizo.

Mfano;
Benin kagundua kuwa ana madini ya urani(uranium) katika ardhi yake, taarifa inabidi ziwafikie serikali ya ufaransa kwanza, nayo itangazie makampuni ya uchimbaji madini kuhusu hiyo fursa. Kama makampuni na serikali itaona hiyo fursa haina tija kwao, wataikataa, hapo sasa ndio serikali ya Benin inaweza tangaza fursa hiyo kwa nchi wawekezaji wengine ambao si wafaransa.

Kwa ufupi ni kwamba, ufaransa kajibinafsishia hizo nchi milele.
Kuna watu watakuwa kuni za kucomea jehanum.
 
Hivi ni utani ama kweli. Mbona naona ni kama jambo lisilowezekana. Sasa huko kwenye umoja wa Africa viongozi Huwa wanakutana kujadili nini kama unyonyaji ni mkubwa hivyo
Mfaransa kazidi! Kuna kipindi waliingia mgogoro na Italia, waziri mkuu wa Italia akawaambia France hamna haki ya kutufunzs maadili nchi inayoendeleza ukoloni barani Afrika mpaka sasa.

Hata waziri mkuu wa sasa aliingia mgogoro na Macron naye akampiga dongo hilo hilo kuwa France ni nchi inayoendeleza ukoloni Afrika, na akaongelea baadhi ya mambo wanayoyafanya kwenye makoloni yake.

Kuna ripoti nyengine zinasema uchumi wa France bila makoloni ya Afrika utaporomoka sana yaani hamna kitu.

Mfano mwepesi ukitaka kuliona hili pindi Russia ilipomtoa kwenye makoloni yake yalimotokea mapinduzi ya kijeshi, France kwenye umoja wa EU na kwenye Nato akawa ana push kwa hasira agenda ya Ukraine iruhusiwe kutumia silaha za Nato kupiga moja kwa moja nchini Russia.
 
Mfaransa kazidi! Kuna kipindi waliingia mgogoro na Italia, waziri mkuu wa Italia akawaambia France hamna haki ya kutufunzs maadili nchi inayoendeleza ukoloni barani Afrika mpaka sasa.

Hata waziri mkuu wa sasa aliingia mgogoro na Macron naye akampiga dongo hilo hilo kuwa France ni nchi inayoendeleza ukoloni Afrika, na akaongelea baadhi ya mambo wanayoyafanya kwenye makoloni yake.

Kuna ripoti nyengine zinasema uchumi wa France bila makoloni ya Afrika utaporomoka sana yaani hamna kitu.

Mfano mwepesi ukitaka kuliona hili pindi Russia ilipomtoa kwenye makoloni yake yalimotokea mapinduzi ya kijeshi, France kwenye umoja wa EU na kwenye Nato akawa ana push kwa hasira agenda ya Ukraine iruhusiwe kutumia silaha za Nato kupiga moja kwa moja nchini Russia.
Sasa kuna Mtu atakuuliza transaction zinafanyikaje, kiufupi hii kitu ni illegal Issue ni kama unavyosikia Mtu kala Rushwa hivyo inatumika akili nyingi sana kulifanikisha hili
 
Hao wafaransa washenzi sana na pia waafrika ambao wapo kwenye huo uonevu nao ni wapumbavu sana.
Blaise Kompaore wa Burkinafaso aliahidiwa Urais wa milele na Ufaransa endapo atamuua Thomas Sankara.., lilivyojinga na binafsi likamuua na kuanza kulipa hizo pesa. Allasaine Outarra wa Ivory Coast aliahidiwa Urais wa milele na Ufaransa, likamuibia kura Laurent Bagbo kwa msaada wa Ufaransa na likaanza kulipa pesa Ufaransa, hapa kuna ubinfsi, lakini pia kuna vitisho vya kuwawa ndio vinasababisha walioe pesa!
 
Kwa hiyo na sisi serikali yetu ya nchi ya Tanganyika inamlipa Mwingereza aliyetutwala kwa dhamana baada ya vita kuu ya 2?
Hii historia ya wapi hii? Kwamba mwingereza ameanza kuitawala Tanganyika baada ya vita vya pili vya dunia? Hii sijawahi kuisikia!
 
Fake news, hizo nchi kwanza hazina uwezo wa kugenerate hizo dollar billioni 500 kwa mwaka za kulipa kadeni na bado zijiendeshe

Hakuna Siri sa ivi duniani kwenye ulimwengu wa kidijitali, labda uniambie hua wanalipana hizo pesa kwenye magunia, ila kama ni transactions za kibenk ingekua ishajulikana kitambo tu,

Btw, nchi Gani hizo mbili ambapo wafaransa walifanya ivo?
Mkuu usikaze fuvu kubisha

Tumia akili kufikiria sio mihemko

Hili linalosemwa hapo halijatoka kwa baba yako nachingwea wameongea viongozi tena kiongozi mkubwa wa bukinafaso wewe Nani ambaye hata huo mktaba hujui walitumia peni au penseli kusainia

Inshort ukifunzwa Jambo hasa hayo ya kizelendo jitahidi kujenge hoja sio unaongea Kama huna korodani
 
Hata mgodi wa buhemba jamaa walifungulia mkondo wa maji ni balaa humo wananchi wanachimna wanahangaika wanasema sijui maji yanatokea wapi, they channelled Mara river there
 
Kwa sasa naandika kwa kifupi sana, ila nitaleta andika kamili kesho au baadae.

Nitaanza na Francophone Africa. mnafahamu kwamba Ufaransa iliwasainisha makoloni yake yote mkataba unaoitwa ‘Agreement for the continuation of colonialism’ kabla hajawapa ‘uhuru feki’?

Msingi wa mkataba huu ni kwamba Ufaransa anadai alipwe kwanza fidia ya maendeleo yote ya kiutawala na miundo mbinu ambayo aliwekeza kwenye nchi hizo ili aweze kuondoka.

Kuna nchi mbili ziligoma kusaini , kilichowakuta kiliwaogopesha makoloni mengime yote na wakasaini. Wale waliogoma, Ufaransa aliondoka , lakini alichukua kila kilicho chake ambacho kinahamishika, vile ambavyo havihamishiki walivichoma moto vyote, waling’oa reli, walichoma moto majengo yote ya kiutawala, walichoma moto maghala yote ya chakula, walitia sumu visima vyote, waliharibu kila kitu! Ndio wakaondoka, kuona dhahama hiyo, wote waliobaki walisaini.

Kupitia mkataba huo wa siri wa kinyonyaji, nchi za Francophone Africa wanalipa Dollar Billioni 500 kila mwaka kwa Ufaransa, na sharti kuu ni iwe siri , wananchi wasiambiwe.

Marais wengi wapya wa nchi hizo kila walipoingia madarakani walikutana na mkataba huu, na hawakuamini walichokiona, na wakagoma kulipa, kila aliyegoma aliuwawa au kupinduliwa. Angalia histora ya Marais wa nchi hizo, utashangaa, wengi sana wameuwawa na kupinduliwa.

Burkinafaso mfano, walishamuuwaga Thomas Sankara, hata huyu Rais wao wa sasa, huu mkataba ulimuumiza sana roho, na akawafukuza wafaransa na kusema wazi kabisa , haogopi kufa, na hata majaribio ya mapinduzi wameshamfanyia majaribio zaidi ya 10, na bado wanaendelea kumuwinda. Ameina bora akatafuta alliance na Urusi, na wameingia military pact ya kumlinda kwa malipo kidogo. Inshort huyu Dogo kawaambia Ufaransa lije jua ije mvua, halipi hiyo pesa!! Na kawatimua nchini kwake!

Huo mkataba nitauleta na nitauchimbua msharti yake yalivyo makali, inaumiza sana. Dollar billion 500 kila mwaka wale mbwa wanavuna, inauma sana!

Mzee wa kazi dola bilioni 500????

Hivi hiyo figure umeisoma vizuri ama??

Angalia kwanza GDP ya Taifa tajiri kabisa Afrika afu rudi kwenye figure ndio ujue sio hela ya kizembe kabisa


Na ingekuwa hivyo kama kweli basi hakuna Taifa ambalo lingemudu


Deni oingekuwa haliambiliki
 
Back
Top Bottom