FRANCIS DA DON
JF-Expert Member
- Sep 4, 2013
- 38,920
- 44,970
- Thread starter
- #101
Tofauti yangu na wewe ni kwamba wewe unalaumu Wafaransa wana mikataba ya siri mibaya ambayo Waafrkka hawawezi kujiondoa wakijiondoa wanauawa.
Mimi nasema mikataba hiyo ya CAF/Ufaransa iko wazi inajulikana na tatizo ni viongozi wa Afrika wanaoangalia interests zao zaidi ya za Wafaransa.
Achana na hao Wafaransa, Thabo Mbeki rais msomi wa Afrika ya kusini, aliyeanzisha idea ya "African Renaissance", idea ya kuirudisha Africa katika kujitambua na maendeleo, alitia saini mkataba wa doka bili9ni 10 za kampuni ya BAE ya Uingerwza kuhusu manunuzi ya sioaha (dellal kama la radar enzi za Mkapa, na kampuni ile ile).
Thabo Mbeki alijua kuwa BAE imezidisha bei ya silaha kwa mara mbili na nusu, na Afrika ya Kusini haikuhitaji hizo silaha. Na kwamba hizo hela ni nyingi sana na zingeweza kutumika kwenyw shughuli nyingi sana za kijamii, including kusaidia kupigana na HIV/AIDS South Africa.
Lakini Thabo Mbeki aliamua kununua sulaha kwa sababu tu wazee wa ANC walikuwa wanapewa rushwa ya dola za Marekani milioni 300 ambazo walitaka kuzitumia kwenye uchaguzi.
Tanzania tulipigwa deal kama hilo kwenye ununuzi wa radar mpaka Claire Shirt akaibana BAE tukarudishiwa sehemu ya hela.
Na hapo itaona Tanzania na South Africa hazijatawaliwa na Ufaransa.
Sasa hapo utasema tatizo ni Wafaransa au viongozi wa Africa?
Tafuta documentary inaitwa "Shadow World : Inside The Global Arms Trade" uangalie jinsi biashara ya silaha ilivyogubikwa na rushwa na jinsi viongozi wa Afrika wanavyojiingiza kwenye hii rushwa kwa hiyari yao wenyewe.
View: https://youtu.be/aT6Xhkdrq8M?si=fQvWWbzYppLJHBju