Nchi za Kiarabu muda wa kuishinda Israel ni sasa

Nchi za Kiarabu muda wa kuishinda Israel ni sasa

Unajitia moyo sio?nadhani moyoni wako una majeraha makubwa Sana kila ukiangalia wapendwa wako na nchi Yao walivyoburudishwa,ila mbele za umma unakaza...poleni sana Kwa madhila yaliyowapata
Kwani majeraha tena? siyo majeraha, ni donda ndugu la miaka 70.

Upo hapo ulipo?
 
Kwani majeraha tena? siyo majeraha, ni donda ndugu la miaka 70.

Upo hapo ulipo?
70 yrs! Dah hakuna namna Sasa Itabidi wajisalimishe Kwa Jehovah Nisi,bendera ya Ushindi kila kitu kitakuwa sawa...
 
6 Haya ndiyo asemayo BWANA; Kwa makosa matatu ya Gaza, naam, kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate; kwa sababu waliichukua katika hali ya kufungwa kabila nzima, wawatie katika mikono ya Edomu;
7 lakini nitapeleka moto juu ya ukuta wa Gaza, nao utayateketeza majumba yake.
Amos 1:6:7
 
Kwa hasira ya kipigo ilichopata Israel katika nusu karne inatumia silaha ya kuwanyima chakula na maji wapalestina wa Gaza.
Wamesema hata mateka wote wakiachiwa bado hakuna mafuta wala mahitaji muhimu yatakayoingia humo.Hiyo ina maana watu wa Gaza hawatofaidika na chochote katika kuachia huru mateka.Sasa washahadie wakubali kufa kishujaa kuliko kurudi nyuma.Ni kufa wote au kuishinda Israel watakapokufa na mateka wao.
Kwa upande wa Israel ama ikubali kusambaratika kwa kushindwa kuwaokoa watu wao wanaodaiwa na ndugu zao au ikubali kupeleka mahitaji Gaza na baada ya hapo kuundwa kwa taifa la Palestina katika mipaka ya angalau 1967.
Nchi za kiarabu zina kitu kidogo tu kumalizia ushindi wa Hamas.Wafungue mipaka kwa nguvu kuruhusu miasaada iingie Gaza.Wakipigwa na wao warudishe mapigo kwa pamoja.
 
6 Haya ndiyo asemayo BWANA; Kwa makosa matatu ya Gaza, naam, kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate; kwa sababu waliichukua katika hali ya kufungwa kabila nzima, wawatie katika mikono ya Edomu;
7 lakini nitapeleka moto juu ya ukuta wa Gaza, nao utayateketeza majumba yake.
Amos 1:6:7
Hayo maneno yametoka kwa nani
 
Hata waungane wote hawawezi moto wa Israel.
Kwa vipi wasiweze.Wana silaha gani inayoweza kuzui kupigwa na wote kwa pamoja.
Tatizo hawana umoja na wanapenda kubaki madarakani.
Jaalia kila taifa la kiarabu likarusha silaha waliyonayo.Iron dome na patriot zitashindwa nguvu.
Patriot na Iron dome huwe zimewekwa makombora idadi maalum.yakiisha lazima ipite angalau saa moja ndipo ianze kazi tena.Huo muda wa saa moja makombora mangapi yanakuwa yameshatua yalikolengwa.
 
Hivi Israel ikijibu kwa nuklia si mtaanza kulia kulia kutuwekea picha za watoto

Sent from my Infinix X663 using JamiiForums mobile app
 
Hivi Israel ikijibu kwa nuklia si mtaanza kulia kulia kutuwekea picha za watoto

Sent from my Infinix X663 using JamiiForums mobile app
Nyuklia ni silaha za maonesho tu.Kila aliyenazo hawezi kuzitumia.jIsrael ndio kabisa hawezi kuzitumia labda zitumbuke zenyewe kimakosa.Wapi atapiga ambapo athari yake haitoingia mpaka ikuluni mwao.
 
Viongozi wa nchi za kiislamu wasijitumbukize katika ujinga utakaowagharimu dunia na akhera yao.Kama ni maazimio ya umoja wa mataifa kuhusu Palestina yapo makumi kadhaa na hayajatekelezwa hata moja.Kinyume chake maazimio hayo yanavunjwa mbele ya macho yao.
Anthony Blinken ameitembelea Israel kuipa pole kutokana na mashambulizi ya Hamas kwenye ardhi zao.Sambamba na yeye ndege za mizigo zimekuwa zikipeleka shehena kubwa za silaha nchini Israel ambayo tangu hapo haina upungufu wa vifaa hivyo.
Sambamba na hilo tena meli kubwa ya kivita na ya kisasa kuliko zote imeshapelekwa jirani kabisa na Gaza na karibu na Israel.Meli hiyo kwa ukubwa wake na vifaa vilivyomo na idadi ya askari wanaokuwemo humo ni sawa na kusema kambi kubwa ya kijeshi ya Marekani imesogezwa karibu kuisaidia Israel kuimaliza Palestina.
Wakati wa press conference hapo jana kati ya Blinken na Netanyahu kiongozi huyo mkubwa wa Marekani alitaja udugu alionao na Israel.Katika kuomboleza vifo vya raia wa Israel alitokwa na machozi katikati ya hotuba yake.
Baada ya kuondoka hapo imeelezwa ratiba inaonesha ataendelea na ziara kuzitembelea Jordan,Misri na Saudi Arabia.
Nini anakwenda kuwaambia nchi hizo.Huku muda huo huo Israel inaongeza ukatili wake kwa wapalestina ikitaka watu milioni moja na ushei wahame makazi yao katika kipindi cha masaa 24.Pamoja na kwamba haiwezekani kwa muda huo watu idadi hiyo kuhama pia huko wanakoelezwa waende hakuna mazingira ya kuwapokea.Kote ni kifo tu.Watakaoshindwa kuhama watakapouliwa itatolewa sababu kuwa waliambiwa wahame.Kule wanakotakiwa kwenda hakuna nyumba,maji ,chakula na umeme na bado hakuna uhakika kuwa hawatadondoshewa mabomu
Kama ni udugu uliomliza Blinken kwa ndugu zake Israel,jee waislamu na waarabu hawana udugu ulio bora zaidi na wenzao wa Palestina.Waislamu wakizidi kuwa wajinga watamalizwa kabisa.
ACHA KICHAPO KIENDELEE KAMA KAWA
 
Back
Top Bottom