Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Katibu mkuu wa jumuiya ya kiarabu mwishoni mwa wiki hii ameitembelea Lebanon na kukutana na kiongozi wa chama kinachoiwakilisha Hizbullah katika serikali ya Lebanon
Bwana Hossam Zaki baada ya kukutana na kiongozi huyo alifanya mahojiano na vyombo vya habari kikiwemo Alqahera cha Misri na kusema nchi za kiarabu zimeamua kuindosha Hizbullah kutoka orodha ya vikundi vya kigaidi.
Nchi za kiarabu awali mwaka 2016 zilikubali kuacha ushirikiano na kundi hilo kwa madai kuwa kilikuwa ni kikundi kibaya na chenye kuhatarisha amani ya mashariki ya kati.
Kauli hiyo ya jumuiya ya kiarabu inakuja wakati vita kati ya Israel na Hizbullah vikinukia kuanza hasa kutokana na shinikizo la Israel ambapo Hizbullah imekuwa ikirusha silaha za kivita kadhaa wa kadha kaskazini ya Lebanon na kusababisha hasara kwa jeshi la Israel pamoja na kulazimika kwa raia wanaokaribia laki moja kuhama makazi yao.
Aljazeera