Mkuu kuna kitu kinaitwa COMMON SENSE, ni kwamba huna au umeumizwa na Israel kuwa na uchumi mkubwa kiasi akili zimekuruka ?
Hivi kwa akili ya kawaida kabisa nchi iliyozungukwa na maadui, muda wowote inarushiwa makombora inaingiaje kwenye list ya nchi yenye furaha ? wewe hapo tu ulipo ukiishi mtaa unatupiwa mawe mda wowote utakuwa na amani ?
Israel kungekuwa na amani isingekuwa mara mbili tu, ingekuwa ni mara 10.
Hebu ona tu nchi kama Marekani hapo wayahudi ndio wanaikimbiza Listi ya mabilionea wakiwa ugenini, kungekuwa shwari peaceful huko nyumbani kwao ingekuwaje ?
Ebu punguza upumbavu, akili ziniruke kwani Israel akiwa na uchumi mkubwa inanipa hasara gani au ww inakupa faida gani?
Ww umeleta mada ijadiliwe kwa hiyo na ndo tupo hapa tuna kutoa upumbavu ulio kujaa kichwani.
Nimesha kwambia kuwa uchumi wa Israel unabebwa na vitu vingi mno na mataifa mengi tena yenye uwezo ,nchi yeyote itakayo bebwa kama Israel na ikashindwa kuendelea basi hiyo nchi itakuwa imejaa wapumbavu walio pitiliza kuizidi hata Haiti.
Nimesha kwambia kuwa bidhaa za Israel zinaingia ndani ya Ulaya , Uingereza na Marekani bila ya kutozwa kodi sasa nchi ya aina hiyo itashindwaje kuendelea?
Huwezi kuilinganisha na zingine ambazo hazina ofa kama hizo.
Nime kutolea mfano Iran ina rundo la vikwazo na imeondolewa kwenye mfumo wa kifedha wa kimataifa wa SWIFT ,hapewi mkopo wowote kutoka IMF,au World bank lakini bado uchumi wake unaendelea kusavave.
Iwapo uchumi wa Israel ungekuwa unapitia yale inayo yapitia Iran na bado ukakua basi hapo Israel ingehitaji pongezi.
Iran mpaka sasa anatumia viwanda vyake vya ndani kukidhi mahitaji yake ya bidhaa kwa 80% kitu ambacho hata Marekani ameshindwa kukifanya.
Wakati Israel ni 48% bidhaa zingine anategemea kutoka nje,hali ya kuwa ana raia wachache sana ukilinganisha na Iran na ndio maana mashambulizi ya wahuthi dhidi ya meli za Israel yamesababisha mfumuko wa bei nchi Israel.
Mwaka 2023 Iran imekuwa ni taifa la pili kwa kuuza bidhaa nyingi za viwandani baada ya Uturuki.
Sasa Iran utailinganishaje na Israel inayo lelewa kama mtoto?
Hivi hapo mashariki ya kati kuna taifa lenye rundo la maadui kuizidi Iran?
Yaani Israel yenye maadui hakina Hizbulah na hamas uta mlinganisha Iran yenye maadui kama akina Marekani na washirika wake wa ulaya na hapo mashariki ya kati?
Alafu nime kuambia mataifa yenye maisha bora na sio mataifa yenye furaha , Maisha bora kwenye nchi fulani huwa yana pimwa kutokana na kipato cha mtu mmoja mmoja ndani ya nchi husika ,sasa hiyo Israel yako hata kwenye 15 bora hayumo wakati waarabu wana nchi zaidi ya 4.
Matajiri wa kiyahudi walioko Marekani sio wageni bali ni wamarekani mbona huelewi si kila muyahudi ni Muisrael na si kila Muisrael ni myahudi.
Na kama unataka kutumia watu wenye asili ya kiyahudi kuipaisha Israel basi hata Iran itafaidika juu ya hilo, maana ndani ya Marekani na Ulaya kumejaa matajiri,wanasayansi na maprofesa wenye asili ya kiajemi hao wote wakihamishia mitaji yao ndani ya Iran basi Iran itakuwa na uchumi mkubwa kuizidi Ufaransa.
Marekani ina matajiri ,wabunifu na wasomi kutoka kila jamii ,kuanzia Wahindi, wayahudi, Waajemi ,waasia walatini, waafrika,na wazungu kwa hiyo hoja yako ya kuwa Marekani inaendelea kisa jamii ya wayahudi haina mashiko.
Alafu myahudi pekee mwenye utajiri mkubwa ndani ya Marekani ni mmiliki wa kampuni ya Meta.
Muanzilishi wa kampuni kubwa na tajiri kuliko zote ndani ya Marekani naduniani yaani Apple ni Mmarekani mwenye asili ya kiarabu kutoka Syria.
Na unacho takiwa kujua ni kuwa Wayahudi wameanza kuingia ndani ya Marekani baada ya vita ya 2 ya dunia na kuikuta Marekani imesha endelea zamani kiteknolojia ,kwa hiyo hoja yako ya eti Marekani anaitegemea Israel ili aendelee ni hoja ya kipumbavu.