Red Giant
JF-Expert Member
- Mar 9, 2012
- 15,657
- 20,967
Duniani leo nchi za kijamaa (communism) zimebaki chache sana. Imebaki China, Vietnam, Cuba, Tanzania na zingine mbili tatu. Mtu anayesema Tanzania siyo nchi ya kijamaa anakuwa anakosea sana. CCM chama kinachoongoza nchi yetu ni chama cha kijamaa. Katiba yetu inasema hivyo, na hata sheria na taratibu za kuendesha nchi zimetungwa kwa mtazamo huo wa kijamaa.
Ukiangalia nchi hizi nne, ni Tanzania pekee ambayo ni nchi ya kijamaa lakini inafuata mfumo wa vyama vingi. China, Vietnam, na Cuba hakuna habari za vyama vingi. Sababu ni kuwa ujamaa na vyama vingi hauendani kabisa. Ujamaa ni mfumo fulani wa kidikteta, hauwezi kuendana na siasa za vyama vingi.
Matatizo ya kisiasa tuliyonayo leo yanatokana na kuchanganya ujamaa na mambo ya vyama vingi. Ingekuwa vizuri tuchague moja.