Tupo pamoja kabisa.
Haya mambo bwana, siyo always black and white. Kwamba Singapore au South Korea wamefanya hivi na sisi tungefanya vile basi tungekuwa kama Singapore au South Korea. Mfano dhahiri ni pale Afrika Kusini. Wale jamaa ni ubepari wa model ya kiwestern kabisa na wana pia katiba nzuri courtesy ya post-apartheid South Africa but kipi wanachoweza kujivunia kwa sasa? Last I checked treni zao za umeme zimecollapse, SA airways inakufa, gap kati ya maskini na tajiri ni kama mbingu na ardhi, yaani South Africa imebaki kubebwa na miundombinu ya mkaburu tu, vinginevyo South isingekuwa tofauti na Zimbabwe.
At the core ya nchi kuendelea mimi naipa model ya uchumi nchi inayofuata (socialism au capitalism) kwenye nafasi ya pili. Nafasi ya kwanza naipa will power na determination ya viongozi (hapo weka usimamizi, inspiration na mobilization ya watu walio chini yao au wanaowasimamia) kuhakikisha nchi inaendelea. Capitalism + excellent leadership = excellent results. Socialism + excellent leadership = excellent results. Mfano hapo nitakupa nchi hata nisizozipenda lakini zinaonyesha kwamba haijalishi philosophy ya nchi kiuchumi bali determination. Iran. Iran ni nchi, can you imagine wanatengeneza satellites zao, ndege zao za kivita, vaccines zao za corona, n.k. pamoja na vikwazo lukuki wanavyowekewa na marekani? Wanafanya hivyo kwa sababu wale maayatollah wanadetermination ya ajabu kweli kweli ya kuiweka nchi yao kwenye levels za juu pamoja na kile kinachoonekana kwa ulimwengu kwamba ni madikteta. Bila vikwazo Iran ingekuwa first world. Huwezi kusema ni kwa sababu ya mafuta maana Saudi Arabia wana uchumi wa mafuta zaidi lakini Saudia wamebaki tu kuwa matajiri ndondocha.
Tanzania hata bila kubadilisha sana model yake na falsafa yake ya uchumi inaweza kupaa fasta kama tukiwa na viongozi excellent. Ni jana tu tulikuwa na Magufuli (the man wasn't a saint lakini alikuwa na determination ya ajabu katika kufanya mambo yatokee). Ni ajabu sana kuona miaka mitano tu ya determination inavyoweza kuleta matokeo yasiyo ya kawaida. Maombi yangu ni isiwe miaka mitano tu ya determination, bali hii spirit iendelee no matter who is at the helm.
Bottom line: mi siyo anti capitalism ila nawaza kwamba chanzo cha ufukara wetu ni ujinga wa viongozi unaohamia hadi kwenye upuuzi kwa sisi tulio chini yao. We unazungumzia upumbavu wa kukosa vyoo mashuleni, umesahau kwamba hata madawati nalo lilikuwa tatizo sugu mpaka Magufuli alipokuja na solutions zake za vodafasta kujaribu kulipunguza? (Sijui kama liliisha).