Nchi za kijamaa (communist) na siasa za vyama vingi huwa haviivi

Hakuna nchi iweya kijamaa au kibepari hawaweki mkono katika hilo. Utofauti mkubwa ni pale serikali inataka yenyewe iuze mpaka karanga. Unajua, mfano nakupa. Suala la maji, unaweza sambaza nchi nzima kwa miezi miwili tu?. Serikali iruhusu private sector kufanya distribution na kuuza maji yenyewe ibaki kama regulator tu utaniambia. Utasema bei kubwa tutauziwa ila nikwambie bei ya sasa ni mara *20 ya bei halisi ya kuuza maji mfano. Dar. Shida kubwa ni upotevu mkubwa sana wa maji, fedha, ubadhilifu n.k ndo inaleta hizo bei. Private sector is more efficient on that.
 
Yeah nakubaliana na wewe kwamba kuna mambo fulani serikali ikishirikiana vyema na private sekta yanaweza kwenda fasta. Japo I would not say kwamba serikali ijiondoe kabisa hasa kwenye sekta za kimkakati. Mfano sidhani kama ni busara control ya umeme iachiwe private sekta.

Halafu ifikie wakati tukubali kwamba private sekta haitaletewa vitu mezani tu. Lazima ijiprove kwamba wanaweza, wanashindana na wanashinda. Kwani mitandao ya simu voda, tigo na airtel walipenya na kutawala jamii ya kijamaa Tanzania baada ya serikali kujiondoa kwenye biashara ya mawasiliano? No, ni majamaa mababe yanayojua biashara yalikuja na teknolojia yakajua jinsi ya kudili na mifumo ya kijamaa na yakashinda.

Vivyo hivyo private sekta itakayoshinda isisubiri serikali ibwage manyanga. Kwa taarifa yako serikali ikiweza kutumia vyema raslimali zilizo chini yake kwa ufanisi hakuna sehemu kitabuni palipoandikwa kwamba mambo yanayoendeshwa na serikali lazima yashindwe. Private sekta ijiprove, na ijiprove bila kusubiri, kwamba wao ni wabia muhimu wa maendeleo ya nchi wanamofanyia biashara. Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania si wapuuzi kiasi hicho kushindwa kushirikiana na sekta binafsi yenye uwezo, ufanisi na vigezo vyote katika kusukuma gurudumu la maendeleo ya nchi.
 
Uangalie vizuri mle kwenye mabano nimeandika Communism. Tatizo ni kuwa kiswahili hakitofautishi haya maneno socialism na communism.
Hapa nazungumzia ujamaa Communism ambao mali zinamilikiwa kijumuia, kama mashamba ya ujamaa, maduka ya ujamaa, udikteta wa chama kimoja, na sifa zingine kama uporaji wa mali za wananchi nk.
 
Umechanganya.
Uchumi wao ni wa kibepari ujamaa umebakia kwenye mgawanyo wa raslimali.
Hii ndio mfumo sahihi yaani uchumi ushikwe na sekta binafsi kodi imilikiwe na serikali kisha igawe sawa kwa wote
Upo sahihi. Kezilahabi amewahi andika kuwa ujamaa unapaswa kuja baada ya ubepari. Sema Nyerere alikuwa haelewi kabisa mambo ya uchumi. Mbaya zaidi hadi leo fikra zake zinadumishwa.
 
Mkuu ungeanza wewe kuleta hayo machafuko, na sisi tungefuata. Anza Mkuu.
 
Upo sahihi. Kezilahabi amewahi andika kuwa ujamaa unapaswa kuja baada ya ubepari. Sema Nyerere alikuwa haelewi kabisa mambo ya uchumi. Mbaya zaidi hadi leo fikra zake zinadumishwa.
Nyerere hakurusu fikra huru kinyume na fikra za mwenyekiti
 
Juzi kati nilibahatika kusoma kitabu kinaitwa China Disruptors. Kinazungumzia makampuni makubwa yaliyoanzishwa Na watu binafsi. Yanavyoendeshwa na yalivyoanza.
Matajiri hao wanalia kila siku sababu mifumo ya kijamaa(Communism) haijaisha yote. Makampuni ya serikali yanashindana na binafsi huku yakipendelewa. Bado mageuzi mengi hasa kwenye masuala ya fedha hayajafanyika. Wakina Ma wanapiga kelele daily kuhusu reforms zaidi.
Wanasema ili China iendelee kupiga hatua tena, inabidi kufanya mabadiliko mengi zaidi.
 
Ndicho nilichomaanisha. Mbona kama tupo sawa?

Shida yangu ni hawa ndugu zangu waliomezeshwa kuwa ujamaa ni mbaya, wanaomeza kila kitu bila kutathmini na kuchanganya za kwao.
Mkuu nafikiri wewe ndiyo umemeza kuwa ujamaa (Socialism/wellfare states) unaofanywa na nchi za magharibi, kama zinazojiita social democrats(ujamaa wa kidemokrasia), na zinazofanya ujamaa wa kijima(communism) ni kitu kimoja.
 
Ndicho nilichomaanisha. Mbona kama tupo sawa?

Shida yangu ni hawa ndugu zangu waliomezeshwa kuwa ujamaa ni mbaya, wanaomeza kila kitu bila kutathmini na kuchanganya za kwao.
Mifumo yote sababu imetengenezwa na wanadamu, ina mapungufu yake. Mfano, Ukomunist na Ubepari yote ni mifumo iliyoua mamilioni ya watu.

Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app
 
Point nzuri. Ila private sector sio dude liko tu pale linakula mtori. Private sector inahitaji kukuzwa na kulelewa kama mtoto. Akishakuwa unamwacha ajiendeshe. Mfano. Unajua mikopo ya benki nchi kama japan na south Korea ni asilimia 2-5%. Huwezi shindana na hawa wa 20-25%. Suala la hakuna sehemu imeandikwa serikali lazima ibume, nakubaliana na wewe. Ila point ni kuwa, serikali haiwezi kuwa efficient kwa mambo yote. Unajua serikali yako inafuga mpaka ng'ombe au hujui? Au hujui serikali inavua samaki mzee, hujui serikali ina miliki daladala.? Sasa mtu wa kawaida afanye nini? Hii inaua innovation haiwapi watu kumiliki sehemu ya uchumi na wakaleta new ideas.

Haya makampuni unayoyaona hapa huko kwao yanalelewa. Nilishawahi sikia kuna nchi huwa inayapa capital at zero interest rate. Sasa hapa kwetu, kabla hujaanza unakatwa kodi from nowhere.
Suala la pili, sheria zetu haziipi private sector kipaumbele. Kuna baadhi ya maeneo huruhusiwi kuwekeza hata kama ni mtanzania.
Ukiachana na hayo yote, kuna wasio na nia njema. Wao wapo serikalini kupiga chao wasepe. Ujamaa wa miaka 60 bila shule kuwa choo mpaka Mmarekani ajenge ni uzwazwa.
 
Fair points.

Hii nchi ilikotoka ni mbali na hata hapa tulipofikia -- yaani nafasi ya private sekta nchini mwetu -- ni hatua kubwa sana. Hayo unayoyainisha ya hadi serikali kumiliki daladala (hapa utakuwa unamaanisha UDART) au kufuga ng'ombe (hapa utakuwa unazungumzia ranch za taifa) ni legacy za iliyokuwa serikali ya kijamaa kindakindaki, serikali ya Nyerere. Hatuwezi kubeza tulikotoka maana kulikuwa na ulazima fulani wa kuwa na nchi ya uchumi wa namna hiyo kwa wakati ule.

Mimi bado nishikilie msimamo wangu kwamba private sekta itakayojitokeza na kuonyesha uwezo wa kukaribia, kuwa sawa na hata kuizidi serikali kwenye operations zake, hakuna sababu ya kwa nini isistawi katika nchi yetu.

Je hilo litabidi serikali ijiondoe kwenye kuendesha UDART ili private sekta wapate nafasi? Hapa sina uhakika sana. Nashawishika kuamini kwamba kama lengo la UDART sio biashara tu bali kupunguza msongamano, itabidi itafutwe namna ya kumpata mtoa huduma au watoa huduma private kwa namna itakayohakikisha ushindani unaoleta ufanisi bila kuathiri lengo la msingi.

Nadhani hizo ndizo deliberations za serikali kuhusu maamuzi ya ifanye yeye au iwaachie private sekta. Wenzetu wana mifumo imara sana maana hata kama wamefikia hadi kuwa na combat forces private (refer blackwater waliotumiwa kama private contractors na marekani kwenye vita yao huko Iraq) bila shaka hatuwezi kujifananisha nao. Historia ya nchi nayo inamatter sana katika hili. Marekani uprivate private umekubuhu kwa sababu watu wa marekani walihamia huko wakiwa makundi private yaliyokuja kuunganika baadaye sana kutengeneza taifa linaloitwa Marekani.

So tusiige kila kitu.
 
Sawa boss. Seems we are in one page but separate line.
Sijazungumzia kuiga na nimetolea mfano wa korea na Japan kwa makusudi kabisa. Hizi nchi at one point tulikuwa tunacheza nao bao. Mtu anaweza jiuliza why Tanzania miaka 60 bado tunapiga jelamba la kujenga vyoo vya shule wakati wenzetu wanawaza technologia? Just to remind you, hizi nchi hazina madini wala misitu wala natural resources wanaweza sema ndio tegemeo. Jawabu ni moja tu, ni mfumo wa uchumi waliochagua ndio unaotutofautisha. Just to put it clear, why kuna a huge gap kati ya South na North Korea lakini hizi nchi ni similar almost in everything? Jibu ni hilo moja, mfumo wa kuendesha nchi ndio umewatofautisha. Kwa kisukuma tunaota country institution settings.
Huwezi kuwa regulator na owners at the same time. Kuna baadhi ya mambo lazima serikali ifanye moja kwa moja na kuna mambo lazima ifanye delegation kwa private sector. Hii itaisaidia kuwa efficient zaidi.
Mfano. Reli sio lazima iendeshwe na serikali 100%, hata UDART sidhani kama ni ishu za legacy hapo ni ukiritimba tu.
Imani yangu na hii nasimamia siku zote, mfumo wa ujamaa au ukomunisti ni wa kidikteta na hauna majibu ya ustawi wa watu. Na bado siamini katika 100% ubepari. We must/have to stay somewhere in between.
Mfumo wa sasa ni wa watu wachache na kundi kubwa la. Maskini wakiendelea kuteseka kwa kulinda legacy za kijinga na zisizo na manufaa.
 
Nachukia ujamaa wa kikomunisti! Nauchukia hapa na kwenye mwezi na kurudi
 
Tupo pamoja kabisa.

Haya mambo bwana, siyo always black and white. Kwamba Singapore au South Korea wamefanya hivi na sisi tungefanya vile basi tungekuwa kama Singapore au South Korea. Mfano dhahiri ni pale Afrika Kusini. Wale jamaa ni ubepari wa model ya kiwestern kabisa na wana pia katiba nzuri courtesy ya post-apartheid South Africa but kipi wanachoweza kujivunia kwa sasa? Last I checked treni zao za umeme zimecollapse, SA airways inakufa, gap kati ya maskini na tajiri ni kama mbingu na ardhi, yaani South Africa imebaki kubebwa na miundombinu ya mkaburu tu, vinginevyo South isingekuwa tofauti na Zimbabwe.

At the core ya nchi kuendelea mimi naipa model ya uchumi nchi inayofuata (socialism au capitalism) kwenye nafasi ya pili. Nafasi ya kwanza naipa will power na determination ya viongozi (hapo weka usimamizi, inspiration na mobilization ya watu walio chini yao au wanaowasimamia) kuhakikisha nchi inaendelea. Capitalism + excellent leadership = excellent results. Socialism + excellent leadership = excellent results. Mfano hapo nitakupa nchi hata nisizozipenda lakini zinaonyesha kwamba haijalishi philosophy ya nchi kiuchumi bali determination. Iran. Iran ni nchi, can you imagine wanatengeneza satellites zao, ndege zao za kivita, vaccines zao za corona, n.k. pamoja na vikwazo lukuki wanavyowekewa na marekani? Wanafanya hivyo kwa sababu wale maayatollah wanadetermination ya ajabu kweli kweli ya kuiweka nchi yao kwenye levels za juu pamoja na kile kinachoonekana kwa ulimwengu kwamba ni madikteta. Bila vikwazo Iran ingekuwa first world. Huwezi kusema ni kwa sababu ya mafuta maana Saudi Arabia wana uchumi wa mafuta zaidi lakini Saudia wamebaki tu kuwa matajiri ndondocha.

Tanzania hata bila kubadilisha sana model yake na falsafa yake ya uchumi inaweza kupaa fasta kama tukiwa na viongozi excellent. Ni jana tu tulikuwa na Magufuli (the man wasn't a saint lakini alikuwa na determination ya ajabu katika kufanya mambo yatokee). Ni ajabu sana kuona miaka mitano tu ya determination inavyoweza kuleta matokeo yasiyo ya kawaida. Maombi yangu ni isiwe miaka mitano tu ya determination, bali hii spirit iendelee no matter who is at the helm.

Bottom line: mi siyo anti capitalism ila nawaza kwamba chanzo cha ufukara wetu ni ujinga wa viongozi unaohamia hadi kwenye upuuzi kwa sisi tulio chini yao. We unazungumzia upumbavu wa kukosa vyoo mashuleni, umesahau kwamba hata madawati nalo lilikuwa tatizo sugu mpaka Magufuli alipokuja na solutions zake za vodafasta kujaribu kulipunguza? (Sijui kama liliisha).
 
Bila ya kuwa na dira ya taifa na kuwa na watu sahihi kusimamia dira ni ngumu Kama taifa kupata maendeleo ya kweli wimbo utakuwa ule ule kila miaka maendeleo maendeleo wakati hakuna kitu chochote zaidi ya siasa za kijinga

Angalia matendo ya viongozi wa Tanzania utasema Wana determinations za kuleta maendeleo nchini?

Huwa namuona Botha kaburu alikuwa Kama prophet kwenye hotuba yake ambayo alizungumzia mambo mengi Sana juu ya mwafrika akidai ni ngumu Sana mwafrika kujitawala na hili lipo wazi kabisa.

Mwisho kongole mkuu una Jenga hoja na kujibu vizuri Sana.
 
Ndo maana tunataka tuandike katiba mpya tuachane na huu mfumo primitive
 
Mkuu tusijikatie tamaa kama waafrika. Hapa tunabrainstorm tu na pale tunapojicriticize kama waafrika ni kwa maana ya kwamba tunaweza kufanya vizuri zaidi ya tunavyofanya. Zipo nchi za waafrika zinafanya vizuri so mchezo: Namibia na Botwsana come to mind.

Hao akina Botha ni wabaguzi wa rangi wapuuzi tu na wala tusiwatumie kama reference.
 
Swali muhimu la kujiuliza why Botswana na Namibia waweze sisi tupo pale pale? Miaka 60 ya uhuru

Licha ya kuwa mbaguzi Botha haiondoi ukweli wa mambo aliyo yasema maana yanaonekana kupitia tawala zetu mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…