Nchi za kijamaa (communist) na siasa za vyama vingi huwa haviivi

Unajua maana ya communist state na socialist state na utofauti uliopo?pia jaribu kupitia democratic socialism

Kinachotokea bongo ni uroho wa madaraka na baadhi ya vyama kujiona vina hatimiliki ya hii nchi.
 
Hapana. Nchi za kijamaa ni nyingi. Na hizo ulizotaja sio za kijamaa. China, Vietnam, Cuba,tz,ni inchi za kikomunist. Nchi za kijamaa ni USA
Nchi za kijamaa ni nchi zote za Ulaya Magharibi, Marekani, Canada na Índia. Nchi za kibepari ni nchi za kiarabu karibu zote za Kiislamu kasoro Yemen na Tunísia, Libya na Jamhuri ya Saharawi. Nchi unazo fikiri na unadhani ni za kijamaa ni nchi za kikominist.

What is socialism? What is capilism? What is Communism?

Tanzania is a Democratic Socialist state and not Communist.

No country in Africa which is a Capitalist.
 
Kati ya idea mbovu kabisa kuwahi kutokea dunian mojawapo ni ujamaa huu.

Ni mfumo fulan hiv wa kidictator tu wakuua watu na kuwafanya watu waishi kimaskini sanaaaaaa refer Tz ya nyerere , North Korea , Cuba
Ujamaa ndio mfumo halisi wa mwanadamu, ubepari ulikuja baadae. Unavyoishi na família yako ni kijamaa, unasaifia elimu, afya kwa mke, watoto na jamaa wa karibu.

Capitalism unamiliki means of production and distribution of wealth and kuto husika na social services.
 
I agree. Basically, unachoongea ndicho naongea ila mimi na wewe tunatofautia kitu kimoja, wewe unaamini katika mtu mimi naamini katika mfumo. Risk ya kuamini mtu ni kuwa mtu huzaliwa, huishi, hufa ila mfumo huisha. Let assume magufuli was a deterministic leader, the question is how can we create/make/breed/form/produce more magufulis?. A strong institutions is the only way. Kuzani labda kuna mtu kama magufuli atakuja mbeleni tena ajenge vyoo ni kujidanganya.

South Africa sio nchi ya kuwekea mfano kabisa unless you want to highlight the negative effects of apartheid policy.

Your missing one point. Nasema south/North kama mfano ningeweza kuwa absolutist nikajiuliza tu bila kutaja hizo nchi. 60 years, watu wanaishi nyumba za miti, 60 years watu hawana maji tena Dar es salaam hapo achilia mbali Singida, 60 years kuna watu wanasomea chini ya miembe, 60 years watu wanakufa kwa kukosa huduma mhimu za afya? My friend, let be fair huu ni ujamaa wa aina gani?. Hii model imeprove failure everywhere! Na ni mfumo wa kishenzi kabisa so to speak.
Kama ndio ujamaa basi tuone atleast kila mmoja apate kidogo, kusiwe na wamasaki wala wa Kaliua. Tunahubiri ujamaa wakati hatupractice ujamaa.
Again, my point ni ile ile moja, we need strong institutions not a strong man/women. Kesho unaweza akaja mtu akaamuru mtu yeyote mwenye pesa bank hela yake ihamishiwe serikalini! {Worst case scenario}. Usiseme haiwezekani, ndivo nchi za kijamaa zinaendeshwa. A lot of bureaucracy, unfair legal system etc. Mtu unamiliki estate/shamba ila anakuja mtu anasema ardhi ni mali ya serikali hii estate kuanzia leo ni ya serikali, unaweza guess madhara yake?
Anyway, huu ni mjadala usio na tija pia,. To conclude, we have to strike a balance between the two, mixed economy with strong institutions.
 
Yeah ni kama umemaliza kila kitu. Ningeongezea tu kwamba usipuuze umuhimu wa mtu. I can tell you ile kauli maarufu inayoanza na "watu", ya watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora ni ukweli wa milele. Yote kati ya yote it begins with us, people. North Korea ipo vile kwa sababu ya watu, South Korea ipo vile kwa sababu ya watu.

At the end of the day naondoka na kauli yako: hatuna sababu ya kuendelea kuwa maskini miaka yote hii 60. Mawazo yote ni mema.
 
Kila la heri mkuu. Nami naondoka na hilo moja. Siasa safi na uongozi bora hujengwa na taasisi imara.
 
Una maanisha nini unaposema Mwafrika ni ngumu kujitawala? Kabla ya wazungu hawajaja Afrika, kulikuwa hakuna tawala huku? Nini mchango wa hao wazungu katika kuharibu tawala zetu huku Afrika na kusimika madikteta? Mfano, kule Kongo Patrice Lumumba, alikuwa mstari wa mbele kuongoza vuguvugu la kuhakikisha Zaire inapata Maendeleo kutokana na Rasilimali zake, lakini hao makaburu (kina Botha) kwa kutumia Military Power yao, walimuweka muuaji Mobutu kuwa Rais. Hapa utasema vipi waafrika hawawezi kujitawala? Hizi ni colonial mindset, na ndio zilitumika kuhalalisha ukoloni wa kina Leopold II kule Kongo, na hatimaye kuua mamilioni ya wakongo.

Hawa wazungu, wakiacha kuwalinda watawala wanaokula nao pamoja, nakuhakikishia Afrika itakuwa na tawala nzuri na zinazojali ustawi wa watu. Afrika iliharibika hatua zake za Maendeleo ya kisiasa, kiuchumi wakoloni walipoigawana Afrika. Na hadi leo bado wapo, na ndio wanaendelea kuitesa Afrika.

Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app
 
Mnazungumzia sana mifumo, mimi nina ufahamu wa kupevuka wa uchumi masoko ( market economy ) na masoko fedha( financial Matkets), mfumo kodi ( fiscal policy ). Na runnings and control systems zake.
Mfumo huwa imara tuu, ukisimamiwa na strong personalities.

Mfano kama Mwendazake Magufuli angeamua kufanya chochote chema kwa nchi yetu angekifanya na kufanikiwa( he was a strong personality ), na hapo ndio angekuwa ameacha utaratibu wa kufanikisha hilo jambo ambalo ameeamua kulifanya. System.

Watu hutengeneza mfumo kadiri wanapofanya na kufanikiwa mambo muhimu, na mfumo mzuri na endelevu huwa hautungwi ila una evolve.

To push people to do things differently from what they are used to for ages, you need a strong personality to push it, by choice we prefer it to be done by a logic person.

Weak people referes these strong personalities as DICTATORS.
 
On point.
 
Kama mzungu anaweza kupandikiza madikteta katika bara la Afrika ni wazi kwamba mwafrika hawezi kujitawala ndio maana mzungu anamtumia mtu asiye na uwezo kujitawala yeye kumtawala.

Kuhusu Patrice Lumumba kifo chake nacho kinaonesha ufinyu wa mawazo ya mwafrika ambapo tuna ona kwamba mzungu anamtumia mwafrika kumuua mwafrika mwezake Sasa hapa mwenye kosa ni nani mwafrika au mzungu?

Mpaka mzungu kuwa na nguvu ya kuingia kwenye tawala za waafrika ni wazi kwamba mwafrika hawezi kujitawala mkuu

Baada ya mataifa mengi ya Afrika kupata Uhuru hasa kwenye miaka ya 1960 viongozi wengi walikuja kuwa hatari kuliko hata wakoloni wenyewe na mwisho waliishia kupinduliwa hata hapa Nyumbani kwetu Mzee wetu Baba wa taifa alipitia kipindi fulani Cha kutaka kupinduliwa kwa aina ya uongozi wake.
 
100% I agree to disagree. Sipendi mzungumzia magufuli siku zote, RIP by the way. Unaweza kuwa sahihi but your missing some recipe. Uchumi sio kama kuswaga kundi kubwa la ng'ombe, is a science based on a testable facts. Strong personality? Labda sijui nini unamaanisha. Kwa kweli niwe muwazi sijui nini unamaanisha.
Anyway, strong personality doesn't shape anyone rather hurts everyone except the few, the chosen. Sitaki kufikiria nini kingetokea endapo magufuli angekaa madarakani 20 years!
Mtu ni mtu, akiachwa afanye kwa utashi atafanya kwa utashi na vile anaamini ila mfumo mzuri wa uchumi humfanya afanye mazuri kwa mtazamo wa ki-nchi na sio wa kibinadamu.
Logical person hawezi nunua ndege 11 by cash na anakopa hela ya kujengea maabara za shule, this is nonsense. Hafu anasimama anachukua kipaza sauti anawaambia faida tutakayo ipata tutapeleka kwenye maendeleo. Anyway.
 
Afrika kuvamiwa na kutawaliwa kimabavu na wazungu, ndio kipimo cha kuwa hawakuwa na uwezo wa kujitawala?



Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app
 
Tanzania ni unafiki tu tunao u practice, hao wengine wameweka wazi kabisa kuwa ni chama kimoja na dunia iwaelewe hivyo.
 
Nyerere hakutaka kupinduliwa kwa sababu ya utawala wake, bali ni wajinga fulani waliotaka wazungu & waasia waondoke serikalini-Wahafidhina wa sera ya Afrikanaizesheni.

Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app
 
Watu wote wanaozungumza kuhusu mifumo sijui hapa huwa wanamaanisha katiba? Kwamba ukiwa na katiba kwa mfano kama ile ya Kenya ya posts zote za kiserikali kushindanishwa ndiyo wao wanaona itaguarantee maendeleo? Toka Kenya wawe na huo mfumo what has changed? Watu wale wale tu, mambo yale yale tu, uchumi ule ule tu wa mwenye nacho kuzidi kuwa nacho na asiye nacho kuzidi kuwa kapuku. Hiyo GDP yao ni very skewed.

Mi huwa nasema kwamba Tanzania pamoja na matatizo yetu (mengi yanasababishwa na viongozi wetu kuwaza kitotototo na kufanya maamuzi mabovu) mtu masikini ana hope ya kutoboa kama akiamua. Kwani hao matajiri wetu wa mjini hata hao wanaoishi Masaki waulize kama wazazi wao wana historia ya utajiri. Haya yote ni matokeo ya sera za kimakusudi za Nyerere za kuset nchi kwenye mfumo ambao wote tutaanzia chini ili kama ni kuinuka basi tuinuke wengi kama siyo wote. Tuna mengi ya kujivunia kuliko kujidharau.
 
Nyerere hakutaka kupinduliwa kwa sababu ya utawala wake, bali ni wajinga fulani waliotaka wazungu & waasia waondoke serikalini-Wahafidhina wa sera ya Afrikanaizesheni.

Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app
Usiwaite wajinga mkuu walikuwa na sababu zao za msingi ambazo wewe unaziita kwa kijinga kwa kutumia uzani gani kwamba zilikuwa za kijinga?
 
Usiwaite wajinga mkuu walikuwa na sababu zao za msingi ambazo wewe unaziita kwa kijinga kwa kutumia uzani gani kwamba zilikuwa za kijinga?
Huwezi muita Amir Jamal sio Muafrika sababu kwa sababu ya rangi yake. Hoja zao hazikuwa za msingi ndio maana nasema walikuwa ni wajinga (wasio na ufahamu), sababu wao Uafrika kwao ilikuwa ni rangi, badala ya uwajibikaji.

Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…