Nchi za Kikristo zinawezaje kuishi kwa amani namna nii?

Nchi za Kikristo zinawezaje kuishi kwa amani namna nii?

kuwapo kabla ya ulimwengu sote tulishakadiriwa tutakuwa vipi kabla ya kuumbwa kwetu si yesu tu , hiyo ni elimu ya Mungu .Yesu hana ujuzi wa kujuwa kabla ya kuzaliwa kwake.
Yaani wewe Islam unifunze maandiko Mimi? Hahah yaani Mimi kazi yangu mwalimu alafu niende kwa diamond nianze kumkosoa muziki wake sio uchizi huo.
Tafsiri zako unakosea kosea unajua kwanini?

Unajaribu kuisoma biblia kiislam.
 
Mimi Si kazi yangu kukuambia nimetoka wapi na nimesoma vipi , Mimi nakuwekea mistari ya biblia kukubali au kukataa si kazi yangu, Haki na batili iko wazi , kazi kwako kukubali au kukataa ukweli. Kila mtu atabeba mzigo wake.
 
Hizi ni baadhi ya nchi zinazo endeshwa kwa misingi ya kikristo na huwezi kuwa kiongozi wa dola ikiwa wewe si mkristo Malta, Armenia, Vatican, England, Denmark, Norway, Iceland nk.

Swali langu ni kwanini huwezi sikia vikundi vya waasi wa kilokole au waasi wa kikatoliki wakiwa msituni wakimpambania mola wao?

Kwanini nchi nyingine kama Syria utasikia sijui wa sunni wameingia msituni kupambana na wasia? Je wanafeli wapi?

Je, nchi zinazo jinasibu zinaongozwa kwa dini ya amani zinawezaje kukosa utulivu miaka nenda rudi?
Elimu, elimu, elimu.
 
Hata Kama Ni mkristo ndo ukariri kariri vifungu weee then uvitafsiri unavyojua wewe? Huna akili hata chembe, yaani unazidiwa na huyo mbongo Islam niliekuwa tunaeleweshana
 
Wanafuata misingi ya Yesu Kristo. Maana siku zote alihubiri upendo na kupendana na kila mtu wa kabila na Imani zote.
Hakubagua wala kusema watu fulani wachukiwe na wala hakuwaagiza mitume wake waeneze Dini kwa upanga. Siku zote alihubiri kuhusu Amani.
 
Yesu alihubiri amani lkn hakuvumilia wapumbavu. Wale vichwa vigumu wanajua shughuli yake. Vizazi vya nyoka.
 
Yesu alihubiri amani lkn hakuvumilia wapumbavu. Wale vichwa vigumu wanajua shughuli yake. Vizazi vya nyoka.
Yesu hakuhusu wewe wala Mimi , alitumwa kwa wayahudi tu ndiyo maneno yake
 
Yesu mwenyewe alikuwa akikataa kuitwa Mungu lkn now unapomwita Mungu ndivyo inavyopasa kwa sababu anayeabudiwa ndio Mungu ukumbuke Mungu baba kwenye mwanzo 6: ..... Mungu alighairi kabisa kuwa amemuumba mwanadamu kutokana na kukithiri kwa maovu, hivyo Basi yesu alichukua jukumu lakutomkatia tamaa na hatimae kumkomboa.

Ndipo Mungu alipomkabidhi yesu wanadamu kwa maana yakumpa jina lake ili Sasa kupitia jina la yesu, Mungu aabudiwe.

Shida inakuja moja, wanadamu wanafanya juhudi kumtenganisha yesu na Mungu Jambo ambalo haliwezekani, wanadamu kwahili watachemka. Yesu na Mungu kuwatenganisha haiwezekani. We fikiria hali ya Mungu kukubali yesu aabudiwe na akishakuabudiwa Basi Mungu anaridhika kwamba ameabudiwa yeye. Ndo sababu yesu alisema Mimi na baba tu umoja.
Nimeuliza swali ambalo lipo wazi kabisa ila umeenda kuzunguka zunguka, ushaeleza sana kuhusu Yesu na hayo nambo yake ila unakwepa kutoa jibu la moja kwa moja kuwa Yesu si Mungu na ndio maana hata yeye alikataa kuitwa Mungu.

Narudia tena kwamba tatizo lako hautaki kukubali kwamba na huyo Baba yake ni waungu bali unataka ibakie kuwa Mungu ni mmoja tu(Baba) ila hapo hapo unaona kuwa Yesu anafaa kuitwa Mungu kwa sababu ana sifa za uungu.
 
Ni kweli kutokana na kusoma kwangu biblia Sana Sana, kwa Sasa mtu akiniuliza swali hili kumjibu kuwa yesu sio Mungu haiwezekani. Lakini pia kumjibu moja kwa moja kwamba yesu Ni Mungu pia haiwezekani.

Kulingana na maandiko, jibu zuri kwa swali Hilo naweza kusema kwamba yesu Ni MWANA WA MUNGU.

Jibu hili linabalance kotekote.
Kwanini tunasema hivi? Ukisoma mithali 8:22 hapa yesu anaonesha ushiriki wake katika uumbaji alivyokuwa akimsaidia Mungu kuumba. Pia anaonesha kwamba alizaliwa ndipo akawa anamsaidia kuumba.

Lkn wakati wakati wa maisha yake hapa duniani, maranyingi aliishi kwa kutafuta utukufu kwa mwingine ambaye Ni Mungu, japo Kuna sehemu alikuwa akijifunua wazi kwa nafasi yake ya ukuu kabla hajazaliwa.

So kwa mantiki hiyo basi, msomaji na aelewe kwamba namna yeyote unavyopenda kumwita yesu inakubalika na ndivyo ilivyo kwa sababu yesu kwa Sasa anamiliki jina linalopita majina yote na ambalo linapaswa kuabudiwa. Jina la YESU.
 
Yaani wewe Islam unifunze maandiko Mimi? Hahah yaani Mimi kazi yangu mwalimu alafu niende kwa diamond nianze kumkosoa muziki wake sio uchizi huo.
Tafsiri zako unakosea kosea unajua kwanini?

Unajaribu kuisoma biblia kiislam.

Hata Kama Ni mkristo ndo ukariri kariri vifungu weee then uvitafsiri unavyojua wewe? Huna akili hata chembe, yaani unazidiwa na huyo mbongo Islam niliekuwa tunaeleweshana

Hata sijatafsiri mimi soma hapa chini

Kwa maneno yasiotatanisha Yesu Kristo anasema kuwa yeye hakutumwa ila kwa "kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli."

Hakuwajia Waarabu, wala Wazungu, wala Wahindi, wala Waafrika, wala Machina.

Kama hayo hayakutosha kuonyesha kuwa yeye hakuwajia wasio Mayahudi anazidi kufahamisha kwa mfano wa kumkata mtu kiu: Si vema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa."

Ikiwa ipo shaka yo yote katika akili ya mtu kuwa maana ya maneno hayo ni kuwa Yesu anasema kuwa hakutumwa kwa kabila nyengine zo zote ila Waisiraili tu na atazame mwenye shaka tafsiri kubwa kabisa ya Wakristo inayoeleza maana wazi maneno ya Biblia,

The Interpreter's Bible, sahifa 441 jalada VII ambamo imeandikwa hivi:

"Yaonekana wazi kuwa Yesu hakika aliamini kuwa ujumbe wake kwanza na khasa ni kwa watu wake mwenyewe." Ndio maana alisema:

Msiwape mbwa kilicho kitakatifu, wala msitupe lulu zenu mbele ya nguruwe, wasije wakazikanyaga chini ya miguu yao, wakageuka na kuwararua.

Mathayo 7.6

Mbwa na nguruwe ni watu wa mataifa yasiyokuwa wana wa Israili.

Ukristo haufai kufundishwa watu wo wote isipokuwa Mayahudi.

Hayo ndiyo mawazo ya Yesu, au ya hao walioandika Injili na wakatia maneno hayo kinywani mwa Yesu.
 
Yaani wewe Islam unifunze maandiko Mimi? Hahah yaani Mimi kazi yangu mwalimu alafu niende kwa diamond nianze kumkosoa muziki wake sio uchizi huo.
Tafsiri zako unakosea kosea unajua kwanini?

Unajaribu kuisoma biblia kiislam.

Yohana 17:5

[...Sasa, Baba, unitukuze Mimi mbele za uso wako kwa ule utukufu niliokuwa nao PAMOJA NAWE kabla ya ulimwengu kuwako...]

Kulingana na wewe, Yesu wa Kibiblia ni Mungu kwa sababu alikuwa na utukufu uleule 'PAMOJA' na Mungu kabla ya ulimwengu kuwepo.

Kwa kutumia neno 'PAMOJA' katika Yohana 17:5, Wakristo walihitimisha kwamba Yesu alikuwa akishiriki utukufu sawa na Mungu -- kwa hiyo Yesu ni Mungu. Kweli?

UCHUNGUZI
--------------
Neno la Kiyunani kwa ajili ya "KWA" katika Yohana 17:5 ni "para" (παρὰ). Lakini 'pamoja' sio maana yake pekee.
Neno "para" (παρὰ) pia linamaanisha 'KUTOKA'.

Mathayo 21:42

[...Yesu akawaambia, “Je, hamjasoma katika Maandiko Matakatifu kwamba: Jiwe walilolikataa waashi limekuwa jiwe kuu la msingi. Hili lilitoka kwa (παρὰ) kwa Bwana na ni la ajabu machoni petu?"...]

Yohana 1:6

[...]

Ikiwa maana ya "para" (παρὰ) inachukuliwa kutoka kwa mtazamo huu, ni wazi kwamba Yesu katika Yohana 17:5 HAKUWA AKISHIRIKI utukufu sawa na 'NA' Mungu.

Kinyume chake, utukufu huo ulikuwa zawadi 'KUTOKA' kwa Mungu hadi kwa Yesu, kabla ya ulimwengu kuwepo.

Kupewa utukufu kutoka kwa Mungu hakukumfanya Yesu kuwa mungu hata kidogo. Kwa sababu Yesu alipowapa wanafunzi wake utukufu huohuo, hakuna hata mmoja wao aliyekuwa mungu yeyote.

Yohana 17:22

[...] Nimewapa utukufu ulionipa. Na wawe kitu kimoja kama Sisi tulivyo wamoja...]
--------------
Na hakuna kitu maalum kuhusu kauli hiyo ya "kabla ya kuwepo kwa ulimwengu". Kulingana na Biblia, Mungu alifanya mambo mengi pia kwa kundi la watu (sio tu kwa Yesu) hata kabla ya ulimwengu kuwepo.

Waefeso 1:4

[...Hata kabla ya kuumba ulimwengu, Mungu alitupenda hata akatuchagua katika Kristo ili tuwe watakatifu na wasio na hatia machoni pake...]

Kwa hiyo, Yohana 17:5 si ushahidi wenye nguvu wa kuunga mkono ‘uungu’ wa Yesu.

Kwa sababu "para" (παρὰ) haina utata. Inaweza kuwa "na" au "kutoka". Wakati mwingine inaweza kuwa "kwa" au "kando" au "saa" na kadhalika.
--------------
Wakristo daima hutegemea mistari yenye utata katika Biblia ili kutetea imani yao. NA WAKATI HUO HUO, WANAACHA KILA MISTARI WAZI KATIKA BIBLIA!

Kwa nini mnafanya hivi, Wakristo?

Kwa nini umechagua kuamini Aya yenye utata na kutoiamini iliyo wazi?

Ninamaanisha, AYA WAZI kama hii:

Yohana 17:1-3

[...Yesu alisema hayo, akatazama juu mbinguni, akasema, Baba, saa imefika. Mtukuze Mwanao ili Mwanao akukuze Wewe, kwa kuwa ulimpa mamlaka juu ya wote wenye mwili; ili awape uzima wa milele wote uliompa. Uzima wa milele ndio huu, Wakujue WEWE, MUNGU WA PEKEE WA KWELI, na yule uliyemtuma, Yesu Kristo...]

Kulingana na Yesu mwenyewe wa Kibiblia, Baba ndiye "MUNGU WA PEKEE WA KWELI".

Je, ni sehemu gani kati ya hizo isiyoeleweka kwenu, Wakristo?
 
Shida sio uislam au ukristo shida ni raslimali na siasa za dunia. na ndio maana msumbiji walipoanza tu kuchimba mafuta ghafla magaidi wakatokea. by the way mi ni mkristo
 
Maelezo mengi hayana mantiki. Wewe andika kidogo toa ufafanuzi. Kila neno lenye pumzi ya Mungu lafaa kwa mafundisho.
Jaribu kufuta Basi ambayo unaona yanautata.

Nikuulize, wewe yesu unamuona Kama Nani?
Nabii
(b) Mungu
(c) mwana wa Mungu
(d) mtume
Chagua jibu sahihi sitaki maelezo usivyo na akili utaleta maelezo hapa
 
Hilo namwachia Yesu mwenye ajibu

Katika Injili ya Yohana mathalan tunasoma:

Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma. Mimi nimekutukuza duniani, hali nimeimaliza kazi ile uliyonipa niifanye.

Yohana 17.3-4

Kwa unyenyekevu wa safi ya niya Yesu anamkhatibu Mola wake, "Mungu wa pekee wa kweli", siye mungu wa uwongo miongoni wa miungu ya uwongo uwongo iliyokuwa ikiabudiwa na makafiri. Ajuulikane Mwenyezi Mungu na kadhaalika ajuulikane yeye Yesu Kristo, Mtume na mtumishi wa Mwenyezi Mungu. Katika kitabu cha Matendo ya Mitume kiliomo katika Agano Jipya la Biblia tunasoma:

Mungu, akiisha kumfufua mtumishi wake Yesu, alimtuma kwenu ninyi kwanza, ili kuwabarikia kwa kumwepusha kila mmoja wenu na maovu yake.

Matendo 3.26

Mungu wa Ibrahimu na wa Isaka na wa Yakobo, Mungu wa baba zetu, amemtukuza mtumishi wake Yesu, ambaye ninyi mlimsaliti na kumkana mbele ya Pilato, alipokuwa ametoa hukumu yake afunguliwe.

Matendo 3.13

Basi sasa, Bwana, yaangalie matisho yao; ukawajalie watumwa wako kunena neno lako kwa ujasiri wote, ukinyosha mkono wako kuponya; ishara na maajabu vifanyike kwa jina la Mtumishi wako mtakatifu Yesu.

Matendo 4.29-30

Wagonjwa wanaponyeshwa, ishara zinaonyeshwa, na maajabu yanatendeka. Nani afanyae yote haya?

Ni kudra na uwezo wa Mwenyezi Mungu.

Jina la Yesu huenda likatumiwa, lakini ni kama chombo tu, wasila, mwombezi, kwani kama atavyokuwa yeye ni "mtumishi mtakatifu wa Mungu."

Katika Matendo 3.26 na 3.13 hapo juu Paulo aliwaandikia Mayahudi ambao walimkataa mtumishi wa Mungu, Yesu Kristo, alipowajia na utumishi kutoka kwa Mungu wa babu zao Mayahudi, Mungu wa Ibrahimu na wa Isaka na Yakobo.

Mwenyezi Mungu ni yule yule mmoja, Mitume ni mbali mbali, lakini utumishi wao ni mmoja. Mayahudi wakawakubali wote waliotangulia wakamkataa Yesu. Mwenyewe Yesu anawasimanga Mayahudi kama inavyotueleza Injili ya Yohana:

Mimi mnanijua, na huko nitokako mnakujua; wala sikuja kwa nafsi yangu; ila yeye aliyenipeleka ni wa kweli, msiyemjua ninyi. Mimi namjua, kwa kuwa nimetoka kwake, naye ndiye aliyenituma.

Yohana 7.28-29

Katika Injili ya Marko Yesu anasimuliwa alimchukua mtoto akasema:

Mtu akimpokea mtoto mmoja wa namna hii kwa jina langu, anipokea mimi: na mtu akinipokea mimi, humpokea, si mimi, bali yeye aliyenituma.

Marko 9.37

Kama hayo aliambiwa Mtume Muhammad s.a.w. na Mwenyezi Mungu katika Qur'ani:

Sema: Ikiwa ninyi mnampenda Mwenyezi Mungu, basi nifuateni mimi, Mwenyezi Mungu atakupendeni na atakusameheni madhambi yenu, kwani Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.

(Qur'ani) Al Imran 3.31

Yesu amesema:

Chakula changu ndicho hiki, niyatende mapenzi yake aliyenipeleka, nikaimalize kazi yake.

Yohana 4.34

Haya khasa ndio maana ya neno Uislamu. Uislamu ni kujisalimisha nafsi yako kwenye mapenzi ya Mwenyezi Mungu, kutenda apendavyo Mola wako Mlezi.

Na hicho ndicho chakula chake Yesu, kama asemavyo, yaani kama anavyohitaji kula kila siku ili aishi, kama wanavyohitaji wanaadamu wote, basi hali kadhaalika kuwa daima anajisalimu mbele ya matakwa ya Mwenyezi Mungu aliyemtuma duniani kuwa ni Mtume.

Tena Yesu amesema:

Mafunzo yangu si yangu mimi, ila ni yake yeye aliyenipeleka. Mtu akipenda kuyatenda mapenzi yake, atajua habari ya yale mafunzo, kwamba yatoka kwa Mungu, au kwamba mimi nanena kwa nafsi yangu tu. Yeye anenaye kwa nafsi yake tu hutafuta utukufu wake mwenyewe; bali anayetafuta utukufu wake aliyempeleka, huyo ni wa kweli, wala ndani yake hamna udhalimu.

Yohana 7.16-18

Tunaona basi kwa ushahidi wake mwenyewe Yesu kuwa fakhari yake ni kunyenyekea kwa Mwenyezi Mungu wake aliyemuumba na akamtuma kwa Wana wa Israili waliopotea kama kondoo.

Kwa uthibitisho wake mwenyewe yeye ni mtumishi wa haki aliyepewa Unabii na kufanywa Mtume. Hataki utukufu wake yeye, bali utukufu wa Mungu wake aliyemtuma na kumpeleka awaongoe watu wafwate njia iliyo nyooka.

Katika Injili ya Mathayo anazidi kufafanua nini wadhifa wake na nini cheo chake mbele ya Mwenyezi Mungu na mbele ya wanaadamu wenziwe.

Alipowateua wanafunzi wake kumi na mbili kuwapeleka kuwahubiria Mayahudi alisema:

Awapokeaye ninyi, anipokea mimi; naye anipokeaye mimi, ampokea yeye aliyenituma. Ampokeaye nabii kwa kuwa ni nabii, atapata thawabu ya nabii; naye ampokeaye mwenye haki kwa kuwa ni mwenye haki, atapata thawabu ya mwenye haki.

Mathayo 10.40-41

Yeye mwenyewe Yesu amesema kuwa yeye ni Mtume, yeye ni Mtumishi, yeye ni Nabii. Je, nini mawazo ya wale wafwasi wake waliomuamini na wakamwona na wakaishi naye? Injili zinatwambia:

Basi watu wale, walipoiona ishara aliyoifanya, walisema, Hakika huyu ni nabii yule ajaye ulimwenguni.

Yohana 6.14

Nao walipotafuta kumkamata, waliwaogopa makutano, kwa maana wao walimwona kuwa nabii.

Mathayo 21.46

Hata alipoingia Yerusalemu, mji wote ukataharuki, watu wakisema, Ni nani huyu? Makutano wakasema, Huyu ni yule nabii, Yesu, wa Nazareti ya Galilaya.

Mathayo 21.10-11

Na tazama, siku ile ile watu wawili miongoni mwao walikuwa wakienda kijiji kimoja, jina lake Emau, kilichokuwa mbali na Yerusalemu kama mwendo wa saa mbili. Nao walikuwa wakizungumza wao kwa wao habari za mambo hayo yote yaliyotukia. Ikawa katika kuzungumza na kuulizana kwao, Yesu mwenyewe alikaribia, akaandamana nao. Macho yao yakafumbwa wasimtambue. Akawaambia, ni Maneno gani haya mnayosemezana hivi mnapotembea? Wakasimama wamekunja nyuso zao. Akajibu mmoja wao, jina lake Kleopa, akamwambia, Je! wewe peke yako u mgeni katika Yerusalemu, hata huyajui yaliyotukia humo siku hizi? Akawauliza, Mambo gani? Wakamwambia, Mambo ya Yesu wa Nazareti, aliyekuwa mtu nabii, mwenye uwezo katika kutenda mbele za Mungu na watu wote.

Luka 24.13-19

Injili kwa umoja wao zinathibitisha kuwa watu wake Yesu waliokuwa naye na kumuamini na wakaona miujiza yake tangu kuzaliwa kwake mpaka mwisho wake walimjua kuwa ni Nabii wa haki, naye ni mtu, mwanaadamu.

"Hakika huyu ni nabii", anasema Yohana.

"waliwona kuwa nabii", anasema Mathayo.

"Huyu ni yule nabii, Yesu", anasema tena Mathayo.

"Yesu wa Nazareti, aliyekuwa mtu nabii", anasema Luka.

Jinsi ya hadhari zake asisingiziwe kuwa anazo au anadai sifa za ungu, Yesu alikataa hata kuitwa "Mwalimu mwema". Sikiliza masimulizi ya Injili ya Marko:

Hata alipokuwa akitoka kwenda njiani, mtu mmoja akaja mbio, akampigia magoti, akmwuuliza, Mwalimu mwema, nifanye nini nipate kuurithi uzima wa milele? Yesu akamwambia, Kwa nini kuniita mwema? hakuna aliye mwema ila mmoja, ndiye Mungu.

Marko 10.17-18
 
Umeuliza swali la kivivu ukitarajia upate ufafanuzi ambao tayari kwa jinsi ulivyouliza swali yamkini unajibu lako hivyo wewe haupo tayari kuujua ukweli.

Ikiwa utautaka ukweli itabidi urudi nyuma uanze kusoma historia ya dunia na umalize usome siasa za dunia.

Hapo utapata ukweli kama lengo lako ni kujifunza na unataka kujua. Mpende kujifunze na kusoma itawasaidia kuwa na majibu ya maswali mepesimepesi.

Wewe hata nchi za kikiristo huzijui na bado unauliza swali la kitoto.Nina mashaka na uwezo wako wa akili na matumizi yake😄😄😄

Pia wewe hujui matumizi ya hiyo simu uliyonayo.

#ELIMU! ELIMU!ELIMU!
Fafanua Sasa!
 
Nchi kama hizo haziwezi kuwa na vita sababu tayari Zina makoloni yao wanayochota mali kwa wapumbavu huku Africa na America .......haujui kua kanisa la Roma sadaka huenda hadi Vatican then wenye akili hula Bata na hizo pesa?
Yes nchi kama Libya,Iraq,Syria hizo lazima ziwe na vita sababu raia hawawezi kubali madini yao kuchotwa kizembe eti uwekezaji, ama eti parokia iwepo watu wachange hela zao zikaliwe Europe
Sasa Raha yake Nini hivyo vita!
 
Kwahiyo wafuasi wa Alkah hawana akili? Wakiona silaha tu wanaanza kupigana? Basi allah atakuwa mpumbavu sana.
Hivyo ni vikundi vilivyotengenezwa na vikiwa na malengo ya kisiasa (sio ya kidini) na uchu wa madaraka na kufadhiliwa na watoa silaha. Dini imetumika tu kwa malengo ya kisiasa. Ukilielewa hili upofu utakutoka.
 
Hizi ni baadhi ya nchi zinazo endeshwa kwa misingi ya kikristo na huwezi kuwa kiongozi wa dola ikiwa wewe si mkristo Malta, Armenia, Vatican, England, Denmark, Norway, Iceland nk.

Swali langu ni kwanini huwezi sikia vikundi vya waasi wa kilokole au waasi wa kikatoliki wakiwa msituni wakimpambania mola wao?

Kwanini nchi nyingine kama Syria utasikia sijui wa sunni wameingia msituni kupambana na wasia? Je wanafeli wapi?

Je, nchi zinazo jinasibu zinaongozwa kwa dini ya amani zinawezaje kukosa utulivu miaka nenda rudi?
Kwenye hz nchi, dini si swala la kiserikali, hata za kiislam zisizofata political islam, Amani IPO, saudia,turkey, nk, kenge ni wale Yemen, Pakistan, Afghanistan,
 
Ni kweli kutokana na kusoma kwangu biblia Sana Sana, kwa Sasa mtu akiniuliza swali hili kumjibu kuwa yesu sio Mungu haiwezekani. Lakini pia kumjibu moja kwa moja kwamba yesu Ni Mungu pia haiwezekani.

Kulingana na maandiko, jibu zuri kwa swali Hilo naweza kusema kwamba yesu Ni MWANA WA MUNGU.

Jibu hili linabalance kotekote.
Kwanini tunasema hivi? Ukisoma mithali 8:22 hapa yesu anaonesha ushiriki wake katika uumbaji alivyokuwa akimsaidia Mungu kuumba. Pia anaonesha kwamba alizaliwa ndipo akawa anamsaidia kuumba.

Lkn wakati wakati wa maisha yake hapa duniani, maranyingi aliishi kwa kutafuta utukufu kwa mwingine ambaye Ni Mungu, japo Kuna sehemu alikuwa akijifunua wazi kwa nafasi yake ya ukuu kabla hajazaliwa.

So kwa mantiki hiyo basi, msomaji na aelewe kwamba namna yeyote unavyopenda kumwita yesu inakubalika na ndivyo ilivyo kwa sababu yesu kwa Sasa anamiliki jina linalopita majina yote na ambalo linapaswa kuabudiwa. Jina la YESU.
Ndio maana nilimwambia member mmoja kuwa Biblia ndio yenye shida hasa katika hili suala la Yesu, watu hutofautiana kuhusu Yesu na tatizo sio uelewa wao tu bali biblia hufanya kila upande kutoa andiko kwenye biblia hiyo hiyo kusapoti hoja yake.
 
Back
Top Bottom