Nchi za Magharibi wailalamikia sana Urusi! Wanadai inatumia gesi kama silaha . Hivi walipoiwekea vikwazo zaidi ya 6,000 walidhani itatulia tu?

Nchi za Magharibi wailalamikia sana Urusi! Wanadai inatumia gesi kama silaha . Hivi walipoiwekea vikwazo zaidi ya 6,000 walidhani itatulia tu?

Kitu ambacho sina uhakika ni kuwa, hawa viongozi wa nchi za magharibi je wameshawishika kabisa mioyoni mwao kuwa ni kosa kwa urusi kukataa kuuza gesi yake kwa euro au dola ambayo hairuhusiwi kuitumia? Kama ni hivyo basi wanatia huruma sana!

Au viongozi wa Urusi walishakaa nakufikiria kabisa ni kosa kwa nchi huru kujiunga na muungano wanaoona wao unawafaa, kama ni hivyo basi pombe Kali zimewaharibu kifikra.
 
Kwa kweli hii dunia ni mbovu sana!! Anayeweka tumaini lake duniani hapa ana hasara kubwa! Fikiria mabilionea kama kina Abramovich na wenzake ambao wamepokonywa mabilioni ya dola, walizojikusanyia kwa bidii kwa miaka mingi! Kwa kauli tu ya kibabe!! Hayo mabilioni wangekuwa wamewekeza katika ufalme wa Mungu ingekuwa heri sana kwao!! Duniani ni dhulma kwa kwenda mbele!! Ninashukuru sana kwa kuwa nimekabidhi maisha yangu kwa YESU!!
Na fikiria jinsi watu wanavyouwawa pale Ukraine na Majeshi ya mvamizi eti kisa uoga na ujinga wa Putin.
 
Kila mtu ashinde mechi zake, wao walifunga biashara zao, wamefanya kila kitu, sasa nae mrusi kafanya yake.

Nipo mabwepande naangalia nani ataibuka kidedea..

Sisi ndio wale tusiofungamana na upande wowote [emoji1787]
 
ila ww ulipue viwanda , viwanja vya michezo , maduka ya watu na makazi yao la unaona sawa tu ?
Kwani kalipua kwako? Kama unaona kafanya vibaya na ukamuwekea masharti ya kutokutumia Hera yako unayomlipa, Sasa unataka ukimlipa aifanyie nini?!
 
siku urusi ikikushushia kipondo utarud kurekebisha kauli yako
Amerika ndio waonevu kuliko taifa lolote duniani. Imevamia mataifa kibaao kuua watu na viongozi wao. Acha kutetea mchawi huyo.
 
Yaani Rusia alitakiwa Aikate hiyo Gesi kama Umeme,Yaani paap hakuna Gesi na Baridi hili hapa,Sema amekuwa fair sana anaikata huku anawapa taarifa.Kama ni mimi ningeikata kama nazima taa.
 
Yaani Rusia alitakiwa Aikate hiyo Gesi kama Umeme,Yaani paap hakuna Gesi na Baridi hili hapa,Sema amekuwa fair sana anaikata huku anawapa taarifa.Kama ni mimi ningeikata kama nazima taa.
sure mkuu!
Hata Mimi ningewaambia walipe kwa ruble then nakausha. Ile baridi siku ya pili nazima paah then nakausha, watajiset wenyewe kwenye mstari kama wanafunzi wa darasa la Saba.

Au unapiga ya baba mwenye nyumba unawasha asubuhi unazima usiku.
Ncheeee aisee liwalo na liwe.
 
Sema Mrusi ni Mtu mwema sana na ana huruma
 
Nchi za magharibi zinadhani zenyewe ndio zina haki ya kuadhibu nchi zinmgine, na hazitegemei nchi zingine kujitetea kwa namna yoyote ile!

Nchi za magharibi na washirika wao waliiwekea vikwazo lukuki urusi ikiwemo kutokuruhusiwa kufanya miamala kwa kutumia Euro na dola.

.Kwao hiyo ni sawa!! walitegemea Urusi iendelee kulipwa kwa Euro na dola kwa mauzo ya gesi na mafuta yake hata kama hizo Euro na dola haina faida nazo maana hairuhusiwi kuzitumia!!

Wao kutumia Euro na dola kama silaha ni sawa!! Lakini Urusi kutumia gesi yake kwenye biashara kama silaha ni haramu!!

Vikwazo vya kiuchumi ni vita vya kiuchumi! Silaha katika vita hii ya kiuchumi ni fedha na bidhaa!!

Nchi za magharibi zilitegemea kuipiga Urusi kiuchumi na Urusi ingetulia tu bila yenyewe pia kuzipiga nchi za magharibi kiuchumi pia!! Inachekesha, zinasema zitaishtaki Urusi!!

Mashitaka yenyewe ni haya: Urusi imekataa kupokea dola na Euro(kwenye mauzo ya gesi yake) ambazo tulimpiga marufuku kuzitumia kwenye miamala yake!

Anataka tumlipe kwa ruble anazoweza kuzitumia!!
Wao wamemla vikwazo kama vyote sasa wanalalamika nini.
Yani unipge ngumi halafu nikirudisha ulalamike kuwa ngumi yangu inauma zaidi
 
Marekani alishamuonya Ujerumani kupunguza utegemezi wake kwa gesi ya Russia (mradi wa NORD stream 2) kwani alijua kuna siku Russia ataitumia gesi kama silaha.
 
Kwa kweli hii dunia ni mbovu sana!! Anayeweka tumaini lake duniani hapa ana hasara kubwa! Fikiria mabilionea kama kina Abramovich na wenzake ambao wamepokonywa mabilioni ya dola, walizojikusanyia kwa bidii kwa miaka mingi! Kwa kauli tu ya kibabe!! Hayo mabilioni wangekuwa wamewekeza katika ufalme wa Mungu ingekuwa heri sana kwao!! Duniani ni dhulma kwa kwenda mbele!! Ninashukuru sana kwa kuwa nimekabidhi maisha yangu kwa YESU!!
Mtumishi ubarikiwe sana!
 
Back
Top Bottom