Nchimbi: Mimi hata mambo ya kugombana kivyama vyama siyapendi naona ni ujinga tu

Nchimbi: Mimi hata mambo ya kugombana kivyama vyama siyapendi naona ni ujinga tu

Mim nafikiri badala ya kumkatisha tamaa nchimbi tumuunge mkono. Hakuna kiongozi yeyote katika nchi hii Kwa sasa atasimama na kuongea kama alivyoongea nchimbi. Kuna kitu hakiko sawa nanauona ufa kati ya lile genge na wazalendo wakiongozwa na nchimbi
Naona ni utapeli tu wa kiccm. Samia baada ya kufariki Magufuli alikuja na lugha hizi hizi za kujifanya sijui kulileta taifa pamoja. Yako wapi lei hii?
 
Maneno mazuri vitendo zero,na kuna mtu kanuna ila vice president hafukuzwi kazi la sivyo kesho Nchimbi angeamka jobless
 
Kama kweli huyapendi, mbona unaendelea kuwa sehemu ya serikali inayoyapenda na kuyashabikia?

labda ili aibomoe na kukomboa nchi wafungwa wote wataachiwa, rasilimali zetu kama bandari zilizoporwa zitarudi, demokrasia kurudi tena n.k. kikulacho kinguoni mwako ...
 
Hii ilikuwa bonge la pointi, ingepita bila kuandikwa waandishi wangekuwa maandazi waliojitia upofu wa kuona pointi za kuandika. UVCCM wajifunze maana huwa wanawadis vijana wenzao wa vyama vingine wakati wote wanajenga nchi
 
Kama kweli huyapendi, mbona unaendelea kuwa sehemu ya serikali inayoyapenda na kuyashabikia?
jamaa ni snitch of all time...2015 alikataa uteuzi wa jiwe kupitishwa kinyume na taratibu zao...afu 2025 amekubali yeye na yule kupitishwa kinyume na taratibu zao....hakuna mwenye afadhali kule mbogamboga
 
Acha unafiki - achia ngazi basi tuone kama wewe kidume nanunamqqnisha - na mwamhie boss wako live amwachie Polepole na akome kuteka na kuua Watanganyika. Aache vyama vifanye siasa na atoke hadharani atubu aliyoyafanya October 29.

Bila hivyo, wewe na yeye woote chungu kimoja.
Kwahiyo unataka aache kazi anayoipenda kisa ujinga wa baadhi ya watu? Kumbuka huyo ana ndoto ya kuwa Raisi so haiwezi kufuata ushauri wako ambao usijua siasa za Tanzania zinaendeshwa vipi
 
Anaongea upuuzi gani huyo Nchimbi wakati chama chake ndio kinara wa huu uhuni. Anapojiweka tofauti inasaidia nini wakati hawezi kutatua tatizo lililopo?
Yeye ana mamlaka gani kwenye hii serikali katili? Maana umeongea as if kama cheo chake kina nguvu
 
Umeishia njiani, mkuu 'FUSO'.

Serikali aliyomo yeye huyo Nchimbi, ni serikali HARAM. Amwambie huyo boss wake wakae pembeni waTanzania waweke viongozi wanaowataka wao wenyewe, bila ya mizengwe.

Hizi ngonjera za kujifanya yeye kuwa tofauti na wengine ni mbinu zilezile walizozibuni siku hizi za karibuni kuhadaa watu.
Jaji Mkuu katumia mbinu hizo hizo za kuhutubia mambo asiyoweza kuyafanya huko mahakamani.

Wanachofanya sasa hivi ni kampeni za kufukia uovu, huku wakiwa na matumaini ya kuwa waTanzania watasahau uovu wao.
Wewe umjui vizuri nchimbi
 
Wameamua kutumia mbinu hiyo wakidhani waTanzania ni wajinga wasioelewa kitu..
Masaju juzi katoa bonge la hotuba, kwa mahakama yake haifanyi kazi kwa kupokea maelekezo.
Polisi wakitoa tangazo kukanusha uwepo wa TFF, ukisoma tangazo hilo utasema hao siyo polisi wa Tanzania, kwa namna wanavyojitangaza kufanya kazi kwa weledi wa hali ya juu sana..

Yote haya ni mwendelezo wa ulaghai na hadaa zilezile anazotumia huyu mwanamke shetani kabisa.
Ungekuwa unamjua vizuri Nchimbi usingeongea hivyo, wewe umewahi kusikia Nchimbi ana kashfa za ufisadi? au anatajwa kwenye Mambo maovu?
 
Vizuri.
Angalau ameweka hadharani msimamo wake juu ya uonevu wa watawala dhidi ya wananchi.

Shida ni kuwa kwa mfumo wa Tanzania, makamo wa rais ni kama msindikizaji tu
Lazima mumpongeze sababu mwenzenu ktk imani...
 
Back
Top Bottom