Nchimbi ni Shujaa wa Taifa au kajiuzulu kwasababu zake?

Nchimbi ni Shujaa wa Taifa au kajiuzulu kwasababu zake?

IMG-20260828-WA0079.jpg
 
Kama sio shujaa toka kweny hiyo ID fake itisha press zungumza aliyozungumza Nchimbi kwamba watanzania tupiganie katiba mpya na hizi kesi za ovyo ovyo zifutwe toka utamke aya maneno alafu utapata Mrejesho kwamba ni shujaa au sio shujaa
 
Wa Tanzania 🇹🇿 hili swala la Nchimbi lililosimamisha nchi tafsiri yake imekaaje?

Kuna maswali najiuliza hapa Naomba ku share nanyi

Hawa wafuasi waliojitokeza kumsifia Nchimbi na kumuona shujaa ni wana CCM wenyewe au ni wanachama wa vyama vingine?

Je, nani anajua Nchimbi amejiuzuru kwa maslahi binafsi au kwa maslahi ya taifa?

Na kama amejiuzuru kwa maslahi binafsi, bado anafaa kuonekana shujaa?

Na kama ni kwa maslahi ya taifa zima je ni mambo gani aliyofanya mpaka tuseme huyu kajiuzuru kwa maslahi ya taifa?
Kama yapo share hapa!

Jambo lingine, hili swala la Nchimbi kujiuzuru kwa nini linasherehekewa na upinzani wakati huo huo upinzani unasema hautambui serikali iliyopo?

Inawezekaje je kusherekea mtu kujiuzuru nafasi ambayo wewe huitambui?
Hii imekaaje?

Na kama tunasema kujiuzuru kwake ni jambo kubwa na la kupongezwa basi tunapaswa pia kujiuliza:

Ni nini hasa alichokifanya mpaka kuondoka kwake kuwe jambo la kusherehekea?

Tusije tukawa tunasherekea mtu kwa sababu tu ameondoka kwenye nafasi, bila kuangalia sababu ya kuondoka kwake na impact yake kwa taifa

Karibuni kwa maoni Kosoa, ila weka FACT

Na pia shauri nini kifanyike

Maswali ni mengi, wewe chagua kipande chako, weka maoni yako

ShesRise_1 🤚
Jumaa Kareen ShesRise_1
Nimependa sana namna ulivyoweka maswali yako. Kitu kinachoonekana kwako ni kwamba hupendi kukimbizana na hisia za mitandaoni unapenda kuanzia kwenye facts kabla ya kutoa hitimisho. Hili ni jambo zuri

Umeuliza maswali yanayolazimisha watu wafikiri badala ya kushabikia

Nitarudi nipo kwenye updates za mahakamani
 
Sawa vipi una maoni mengine zaidi kuhusu mada ?
Nchimbi anaweza kubanwa na kubambikiwa kesi ya uhaini, lakini kwa upande mwingine hiki kilichotokea kinazidi kuiharibu taswira ya CCM.

Yeyote anaamini tena CCM kutoka moyoni basi ni punguani wa kutupwa.

Babu yako nilichoma kadi ya chama baada ya huyu shetani kuingia kwa madaraka.
 
Kama sio shujaa toka kweny hiyo ID fake itisha press zungumza aliyozungumza Nchimbi kwamba watanzania tupiganie katiba mpya na hizi kesi za ovyo ovyo zifutwe toka utamke aya maneno alafu utapata Mrejesho kwamba ni shujaa au sio shujaa
Relax kwanza mkuu swala la mimi kutoka kwenye hii I'D fake sio hoja

Labda unisaidie jambo moja
Je Nchimbi amejiuzulu kwa maslahi ya taifa ?
Na unisaidie pia kabla ya kujiuzulu alikua ni nani hasa?
 
Back
Top Bottom