Nchimbi ni Shujaa wa Taifa au kajiuzulu kwasababu zake?

Nchimbi ni Shujaa wa Taifa au kajiuzulu kwasababu zake?

Jumaa Kareen ShesRise_1
Nimependa sana namna ulivyoweka maswali yako. Kitu kinachoonekana kwako ni kwamba hupendi kukimbizana na hisia za mitandaoni unapenda kuanzia kwenye facts kabla ya kutoa hitimisho. Hili ni jambo zuri

Umeuliza maswali yanayolazimisha watu wafikiri badala ya kushabikia

Nitarudi nipo kwenye updates za mahakamani
Shukran bro 🙏
Karibu hapa
 
Nchimbi anaweza kubanwa na kubambikiwa kesi ya uhaini, lakini kwa upande mwingine hiki kilichotokea kinazidi kuiharibu taswira ya CCM.

Yeyote anaamini tena CCM kutoka moyoni basi ni punguani wa kutupwa.

Babu yako nilichoma kadi ya chama baada ya huyu shetani kuingia kwa madaraka.
Ngoja tuone kama atafunguliwa kesi ya uhaini
Asante kwa maoni
 
Ni mahangaiko
Kila siku jipya
Jana nliahidi kuachana na haya mambo Leo nakuta habari Abdul ndio kakalia kitu Cha mkuu wa usalama wa taifa
Kwa Hali hii tutapona?
Mange hasemagi uongo aliwaambia mwaka jana mapema Kuna kontena la silaha limeingizwa mkamuona hamnazo mamlaka zikakanusha,haya niulize Oct 29 Yale masilaha kiwango Cha vitani yalitoka wapi?
Unayo yasema ni kweli?
 
Mimi bado sijaona misimamo yake,kama kweli ana misimamo basi angekataa uteuzi wa umakamu tangu day one ilq sasa yeye alipenda teuzi halafu anajifanya anajiuzulu kwani ccm imeanza kuwa mbaya leo
Swali la msingi liko hapa
Kwanini alikubali uteuzi !

Sasa hivi tuna amini vipi kama alichofanya ni kwa maslahi ya taifa au matarajio aliokua nayo yameyeyuka
 
Mimi naona kashaona how impossible is for him to sit on the throne akatumia strategy hiyo. Huenda akatangazwa chadema huyu!

Jokes aside, jamaa kaona how hellish namna uchafu wa walioko madarakani unavyo umiza watanzania na yeye khususika nao ni kujiletea laana bure. Katumia akili kuona ata haribu reputation yake
 
Upuuzi
Hakuna shuja yeyote,mtu matukio yanatokea kwenye uchaguzi halafu wewe unakubali kuchaguliwa kuwa makamu unakubali unatumikia cheo
Leo kisa kusema tu habari za katiba ndo uwe shujaa!!

Kina Lissu kila siku wanazungumzia habari za katiba hawaitwi mashujaa halafu mtu kwa siku moja tu ndo aiitwe shujaa how!
UTAPELI wa kisiasa.
 
Kama ungesoma taarifa ya Dr. Nchimbi akitangaza kujiuzulu ungekuwa na majibu ya hayo maswali yako.

Dr. Nchimbi alisema; "Nimeamua kujiuzulu baada ya kujiridhisha kuwa Mh. Rais hana nia ya kuendelea kufanya kazi na mimi".

Hapo ndipo utajiuiiza, kosa la Dr. Nchimbi ni lipi?

Utagundua Dr. Nchimbi hana kosa, kutaka watanzania tupiganie Katiba Mpya ni haki yetu, na ni uhuru wake kutoa maoni yake.

So, kujibu swali lako, Dr. Nchimbi ni shujaa wa watanganyika.
 
Upuuzi
Hakuna shuja yeyote,mtu matukio yanatokea kwenye uchaguzi halafu wewe unakubali kuchaguliwa kuwa makamu unakubali unatumikia cheo
Leo kisa kusema tu habari za katiba ndo uwe shujaa!!

Kila Lissu kila siku wanazungumzia habari za katiba hawaitwi mashujaa halafu mtu kwa siku moja tu ndo aiitwe shujaa how!
UTAPELI wa kisiasa.
Hili swala linashangaza
Mtu kutamka neno katiba anapewa ushujaa

Yaani marafiki wawili waliopendana kwa shida na raha wakakutenga
Leo wagombane mmoja wapo aje kwako akidai wewe ni mtu mzuri sana

Yaani uzuri wako anauona baada ya kukosa option?
 
Kama ungesoma taarifa ya Dr. Nchimbi akitangaza kujiuzulu ungekuwa na majibu ya hayo maswali yako.

Dr. Nchimbi alisema; "Nimeamua kujiuzulu baada ya kujiridhisha kuwa Mh. Rais hana nia ya kuendelea kufanya kazi na mimi".

Hapo ndipo utajijliza, kosa la Dr. Nchimbi ni lipi?

Utagundua Dr. Nchimbi hana kosa, kutaka watanzania tupiganie Katiba Mpya ni haki yetu, na ni uhuru wake kutoa maoni yake.

So, kujibu swali lako, Dr. Nchimbi ni shujaa wa watanganyika.
Nani alipendekeza jina la Nchimbi before ya kuteuliwa kuwa makamu

Nieleweshe kwa upole
 
More of a personal gains kama Polepole tu.

Lakini tunawashukuru kwa kuongea Lugha moja na wananchi walio wengi, mengine tuwaachie wapambane na chama chao hadi badamu bamwagike 😂
Upo Sahihi hawa ni wale wale..
Ajabu unawezakujashangaa eti amerudi chamani kaomba msamaha na hata akagombea CCM tena..
 
Hakuna shujaa taifa hili zaidi ya Tundu Lissu, Nchimbi angekua shujaa asingekubali hata kula kiapo siku anaapishwa ilimpasa akae pembeni tangu mwanzo ili kuonyesha msimamo wa kutokukubaliana na uchaguzi ule batili uliojaa damu na uchafuzi, alijiuzulu akikwepa impeachment kwasababu alijua ameshayakoroga ijapokuwa amekumbuka shuka kukiwa kumekucha
 
More of a personal gains kama Polepole tu.
Pigia msitari hapa koleza na wino 📌
Lakini tunawashukuru kwa kuongea Lugha moja na wananchi walio wengi, mengine tuwaachie wapambane na chama chao hadi badamu bamwagike 😂
Sisi hapa tunapaswa kuwaacha mtu na ndugu yake wamalize baasii!

Hii tabia ya kuvika watu ushujaa haina maana

Tuna mambo mengi ya kujadili
Ila hatujadili tuna mpa airtime mtu aliekaa kimya kipindi tumefungiwa ndani kama kuku aibu yetu!
 
Back
Top Bottom