Nchimbi ni zaidi ya mhaini, alaaniwe na kila mtanzania

Sema wewe ni mtu wa zamani sana hizi kauli wala haziku fit
Sawa lakini nimemjibu jinsi alivyokuja mkuu. Mwiba siku zote hutokea pale ulipoingiliašŸ¤£šŸ˜…šŸ˜‚
 
Sasa Nchimbi asisitize na aje na kauli rasmi Tanzania inahitaji katiba mpya na aitishe mikutano tujadili wananchi tukakiwashe
Asipofanya hivyo, bora tu wamuue kama walivyowaua Ndugai na Polepole. Atakuwa hana faida yoyote ktk taifa hili.
 
Nyuma ya hizi Keyboard kila mtu shujaa...
MAFAO YA MAKAMU WA RAIS ALIYEJIUZULU

1 Pensheni sawa na 80% va mshahara wa Makamu atakayemrithi

2 Kiinua mgongo sawa na 50% va mishahara yake yote aliyopokea akiwa Makamu wa Rais.

3 Posho ya kufungia (winding up allowance ambayo itahesabiwa kwa kuangalia mshahara nkubwa zaidi aliowahi kupokea.

4 Mwenza wake atapokea jumla ya mafao ambayo ni sawa na robo ya mishahara yote aliyopokea akiwa kama Makamu wa Rais-

5 Passport ya kidiplomasia pamoja na mwenza wake.

6 Magari mawili ambayo yatabadilishwa kila baada ya miaka mitano pamoja na Matengenezo ya magari hayo;

7 Nyumba yenye vyumba vya kulala vitatu au zaidi na samani zake Nyumba ya Wafanyakazi (servant quarter)

8 Posho ya kujikimu sawa na 80% ya mshahara wa mwezi (NB: Hii ni tofauti na ile Pensheni);

9 Gharama za matibabu ndani na nje ya nchi.

10 Posho ya kujikimu sawa na 80% ya mshahara wa mwezi (NB: Hii ni tofauti na ile Pensheni).

11 Gharama za matibabu ndani na nje ya nchi

12 `Usafiri daraja la kwanza anaposafiri nje ya nchi Usafiri daraia la kwanza kwa mwenza na msaidiz mmoja anayesafiri naye nje ya nchi

13 Gharama zote za Usafiri anaposafiri ndani ya nchi pamoja na Gharama za madereva anaposafiri ndani ya nchi.

14 Ulinzi kwake na familia yake Msaidizi binafsi: Mpishi; Dobi; Mfanyakazi wa ndani; Mtunza bustani; Madereva wawili

15 Haki ya kutumia sehemu za watu mashuhuri (VIF lounge);

16 Gharama za mazishi yake na ya mwenza wake
 
May be atakuwa another Polepole, an activist.

To me naona kama ni retreat. Since jamaa ni mkongwe wa game najua atakuwa na plan na atakuwa na watu.

I believe kuna comeback.
Je, hiyo comeback itakuwa facilitated na watu ndani au nje ya maCCM?
 
Ibara ya 50 ya katiba haitaji suala la uanachama, uanachama ni kigezo cha kuchaguliwa kuwa Makamu wa Rais lakini haujatajwa kama kigezo cha kumuondoa Makamu wa Rais.

50. Muda wa Makamu wa Rais kushika Madaraka

(1) Isipokuwa kama atajiuzulu atafariki mapema zaidi, mtu aliyechaguliwa, au kuteuliwa kwa mujibu wa ibara ya 37(5), kuwa Makamu wa Rais, bila ya kuathiri masharti mengine ya ibara hii, atashika kiti cha Makamu wa Rais kwa muda wa miaka mitano tangu alipochaguliwa kuwa Makamu wa Rais.

(2) Makamu wa Rais atashika kiti hicho hadi–

(a) muda wake utakapokwisha;

(b) akifariki dunia akiwa katika madaraka;

(c) atakapojiuzulu;

(d) atakapoapishwa kuwa Rais baada ya kiti cha Rais kuwa wazi;

(e) atakapotiwa hatiani kwa kosa la jinai linaloonyesha utovu wake wa uaminifu;

(f) atakapoapishwa Rais mwingine kushika nafasi ya Rais pamoja na Makamu wake;

(g) atakapoondolewa madarakani baada ya kushtakiwa Bungeni kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (3) ya Ibara hii;

(h) atakapoacha kushika kiti cha Makamu wa Rais vinginevyo kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.
Fast forward—nadhani sasa umeshajionea mwenyewe jinsi mambo yanavyofanyika kwenye nchi hii. Katiba yetu ya sasa imejenga mfumo wa kututengenezea mungumtu, sio Rais wa kawaida wa nchi.
 
Ndugu zangu, nimesoma bandiko la mtoa mada 'tpaul' na kwa kweli ninalazimika kuunga mkono hoja zake kwa 100%. Watanzania wengi wamezoea kushangilia matukio ya kisiasa kwa mihemko, lakini tpaul ameweka pembeni ushabiki na kutazama uhalisia wa mambo kiuchumi na kiutendaji. Huu hapa ni mchanganuo wa kwa nini hoja zake zina msingi imara:
  1. Uhaini wa Kiuchumi na Mzigo kwa Mlipakodi
    Hili ndilo eneo la msingi ambalo watu hawataki kuliona. Kujiuzulu kwa Nchimbi hakumfanyi anyooshwe mfuko wake; kisheria na kikatiba anahesabika kama Makamu wa Rais mstaafu. Hii ina maana gani kwetu sisi walipakodi tunaosaga lami?
  • Yeye na mwenza wake wataendelea kuvuta 80% ya mshahara wa Makamu wa Rais aliyepo madarakani maisha yao yote.
  • Serikali itatumia mamilioni ya fedha kumjengea nyumba mpya ya kifahari, kumpa walinzi wa kutosha, mafuta, magari, madereva, na wapishi.
  • Hapa ndipo pointi ya tpaul inapokuwa na nguvu: Amekuwa "mtumishi hewa" wa daraja la juu. Anapokea kila kitu bila kufanya kazi yoyote, huku mtoto wa mkulima kijijini akikosa dawa hospitalini na akila mlo mmoja kwa mbinde. Kushangilia kujiuzulu huku ni sawa na mtu anayeshangilia kuongezewa mzigo wa deni kichwani mwake.
  1. Kunguru Mwoga na Kuachia "Mafisi" Nchi
    Tpaul yuko sahihi anapomlinganisha na ujasiri wa Rigathi Gachagua kule Kenya. Ushujaa sio kukimbia vita na kwenda kula pensheni ya kifahari pembeni; ushujaa ni kukomaa humo humo ndani hadi kieleweke.
  • Kitendo cha Nchimbi kuachia ngazi kirahisi baada ya shinikizo dogo la mitandao ya ndani ya chama kimeonyesha udhaifu wake mkuu.
  • Kuondoka kwake kumeacha ombwe kubwa la madaraka (power vacuum) ambalo sasa linakwenda kujazwa kikamilifu na genge la wanamtandao ("Msoga gang & Co").
  • Wakati akiwa humo ndani, angalau uwepo wake ulikuwa unaleta urari wa nguvu (balance of power) uliowazuia mafisi wengine kumeza kila kitu. Sasa usukani umeachwa mikononi mwa kundi moja linalokwenda kuitafuna nchi hadi mfupa wa mwisho bila hofu ya kukosolewa ndani ya vikao vikuu.
  1. Mbinu ya Kupoteza Maboya (Political Diversion)
    Katika sayansi ya siasa, hii inaitwa 'Agenda-Setting' au 'Smoke Screen'. Serikali au chama tawala kikiwa kwenye shinikizo kubwa—iwe ni kubanwa kwa misaada kutoka kwa wafadhili wa nje au mijadala mizito ya kijamii—hutengeneza "tamthilia ya kisiasa" ili kuhamisha akili za wananchi.
  • Ghafla bin vuu, nchi nzima imesahau ajenda za msingi. Kesi ya uhaini ya Tundu Lissu iliyokuwa inafuatiliwa kwa ukaribu na kutikisa nchi sasa hivi imepoteza mshiko kwenye masikio ya watu.
  • Wananchi wameingizwa kwenye mtego wa kujadili nani atateuliwa kuwa Makamu wa Rais mpya (huku tetesi zikimtaja Ridhiwani Kikwete), wakisahau kabisa kufuatilia madudu yanayoendelea nyuma ya pazia, ubadhirifu wa fedha za umma, na utoroshaji wa rasilimali. Tumekuwa kama nyumbu kweli!
  1. Kipimo cha Ushujaa ni Katiba Mpya, Sio Kujiuzulu
    Ninamalizia kwa kusisitiza hoja ya mwisho ya mtoa mada. Nchimbi asisifiwe kwa sababu tu ameweka kalamu chini na kukimbilia kwenye mafao ya kifahari. Ushujaa wake wa kweli utapimwa sasa akiwa nje ya madaraka.
  • Kama kweli alikuwa anapigania maslahi ya umma na Katiba Mpya, aendelee kusimamai msimamo huo sasa hivi akiwa raia wa kawaida bila uoga, kama alivyofanya Humphrey Polepole hadi mwisho wa maisha yake.
  • Kama atakaa kimya na kuanza kufurahia hayo mamilioni ya pensheni huku nchi ikizama, basi thibitisho litakuwa wazi kuwa alikuwa mbinafsi aliyetanguliza tumbo lake na uoga wake mbele.
Mtoa mada tpaul ametufumbua macho na kutupa uchambuzi thabiti. Huu ni uhaini wa kiuchumi na kisiasa unaotugharimu sisi raia wa kawaida, na hatuna sababu yoyote ya kushangilia tamthilia hii ya CCM.
Nawasilisha hoja kuunga mkono!
 
Naingia kwenye mada moja kwa moja bila kuwachosha. Mambo ya leo ni mengi. Alichokifanya bwana Nchimbi kutangaza "kujiuzulu" umakamu wa rais ni zaidi ya uhaini. Nasema haya kwa sababu anuai.

Kwanza, kitendo cha kukubali kuachia nafasi yake baada ya kushinikizwa na wanaCCM mtandao, kinaashiria jinsi alivyo muoga kama kunguru, tofauti na watu wengine wanavyompamba na kumuona kama shujaa. Huyu jamaa sio shukaa bali ni mnafiq na muoga kama walivyo waoga wengine. Kama kweli Nchimbi ni mwanaume rijali, alipaswa kukomaa. Sio kuachia madaraka kirahisi rahisi kama alivyofanya. Kuachia madaraka kirahisi baada ya shinikizo dogo tu kutoka kwa wanamtandao, kutawapa kiki sana Msoga gang & Co. Sasa wataanza kuitafuna nchi kama mchwa na kuna tetesi Ridhiwani Kikwete ndiye anapigiwa chapuo kuteuliwa kuwa Makamu wa Rais. Sasa manyang'au wataanza kuitafuna nchi hadi mfupa wa mwisho.

Nchimbi angekuwa jasiri, angepigana vita akiwa humo humo ndani hadi afukuzwe, kama alivyofanya Rigath Gachagua kule Kenya. Lakini, kinyume na matarajio ya wengi, amekubali kuwa kunguru muoga amekimbiza mbawa zake na kuwaachia mafisi waendelee kuitafuna nchi bila uwoga. Afadhali alipokuwa anaunguruma akiwa jikoni, mafisi walikuwa wanaogopa kuchukua minofu yote. Baada ya kuondoka sasa tutarajie mafisi kula hadi mzani. Na tusisahau wazungu wamemnyima misaada Samuya na genge lake. Kuanzia sasa, hicho kidogo kinachopatikana kutokana na vyanzo vya ndani kitakuwa kinapitiwa na mafisi kama upepo.

Pili, kwa mujibu wa katiba, Nchimbi anahesabika kama Makamu wa Rais mstaafu. Kwa maana hiyo, yeye na mwenza wake wataendelea kulipwa 80% ya mshahara wa Makamu wa Rais aliyepo madarakani. Aidha, serikali itamjengea nyumba, kumpa walinzi, mafuta, madereva, wapishi, nk. Kwa ufupi, ataendelea kuenjoy maisha kama Makamu wa Rais. Na haya yote yanagharamiwa na kodi za wanachi maskini wanaokula mlo mmoja baada ya siku 2. Kwa mukdhata huu, mtu yeyote makini na mwenye akili zilizotimia, hawezi kushangilia kujiuzuru kwa Nchimbi kwani kitendo alichofanya ni mzigo kwa taifa na walipakodi wa nchi hii. Kwa maana nyingine, Nchimbi ameamua kuwa mtumishi hewa kwa kuamua kukaa pembeni huku akiendelea kula bata 80% ya Makamu wa Rais mpya atakayeteuliwa. Huu ni zaidi ya uhaini. Watu wanalia kila siku kuhusu uhaini ambao hauwaumizi wanaacha uhaini wa Nchimbi utakaowachakaza kiuchumi moja kwa moja.

Hii nchi ina wananchi wenye akili za kinyumbu sana. Tazama Tundu Lissu anataabishwa kwa zaidi ya mwaka gerezani kwa uhaini wa mchongo huku wananchi hao hao wakishangilia uhaini wa Nchimbi na kumuona shujaa! Ama kweli ni bora mtu ukose mali upate akili. Watanzania ni nani aliyewaroga?

Tatu, kitendo cha kujiuzulu kwa Nchimbi kitawasahaulisha wananchi mambo muhimu yanayoendelea hapa nchini. Kwa mfano, ghafla bin vuu kesi ya uhaini wa mchongo wa Tundu Lissu sasa imepoteza mashiko. Sasa hivi watu wote wamehamia kwa Nchimbi. Yaani watu tunaacha kufuatilia mambo ya msingi yenye umuhimu wa kitaifa tunafuatulia tamthlia za CCM za "kujiuzuru" kwa Nchimbi. Na sio tu kwamba CCM wametupoteza maboya kwa hii tamthlia bali watatumia mwanya huu kuiba fedha za umma na kuzitorosha nje ya nchi kwa manufaa yao na vizazi vyao. Huu sasa ndio uhaini halisi.

MAONI YANGU
Nitamuona Nchimbi shujaa ikiwa ataendelea na msimamo wake ule ule wa kudai Katiba Mpya. Polepole alipojiuzulu aliendelea na msimamo wake hadi walipomuua. Naye anapaswa kusimamia msimamo wake bila kujali chochote, hata ikibidi auawe kama Polepole alivyouawa. Akifanya hivyo atakuwa shujaa wa taifa na kila mtanzania atamkumbuka kwa ushujaa wake.

Nawasilisha.
​
Hapana,kwa sasa tumwache aendelee na maisha yake.Ni binadamu kama sisi
 
Ndugu zangu, nimesoma bandiko la mtoa mada 'tpaul' na kwa kweli ninalazimika kuunga mkono hoja zake kwa 100%. Watanzania wengi wamezoea kushangilia matukio ya kisiasa kwa mihemko, lakini tpaul ameweka pembeni ushabiki na kutazama uhalisia wa mambo kiuchumi na kiutendaji. Huu hapa ni mchanganuo wa kwa nini hoja zake zina msingi imara:
  1. Uhaini wa Kiuchumi na Mzigo kwa Mlipakodi
    Hili ndilo eneo la msingi ambalo watu hawataki kuliona. Kujiuzulu kwa Nchimbi hakumfanyi anyooshwe mfuko wake; kisheria na kikatiba anahesabika kama Makamu wa Rais mstaafu. Hii ina maana gani kwetu sisi walipakodi tunaosaga lami?
  • Yeye na mwenza wake wataendelea kuvuta 80% ya mshahara wa Makamu wa Rais aliyepo madarakani maisha yao yote.
  • Serikali itatumia mamilioni ya fedha kumjengea nyumba mpya ya kifahari, kumpa walinzi wa kutosha, mafuta, magari, madereva, na wapishi.
  • Hapa ndipo pointi ya tpaul inapokuwa na nguvu: Amekuwa "mtumishi hewa" wa daraja la juu. Anapokea kila kitu bila kufanya kazi yoyote, huku mtoto wa mkulima kijijini akikosa dawa hospitalini na akila mlo mmoja kwa mbinde. Kushangilia kujiuzulu huku ni sawa na mtu anayeshangilia kuongezewa mzigo wa deni kichwani mwake.
  1. Kunguru Mwoga na Kuachia "Mafisi" Nchi
    Tpaul yuko sahihi anapomlinganisha na ujasiri wa Rigathi Gachagua kule Kenya. Ushujaa sio kukimbia vita na kwenda kula pensheni ya kifahari pembeni; ushujaa ni kukomaa humo humo ndani hadi kieleweke.
  • Kitendo cha Nchimbi kuachia ngazi kirahisi baada ya shinikizo dogo la mitandao ya ndani ya chama kimeonyesha udhaifu wake mkuu.
  • Kuondoka kwake kumeacha ombwe kubwa la madaraka (power vacuum) ambalo sasa linakwenda kujazwa kikamilifu na genge la wanamtandao ("Msoga gang & Co").
  • Wakati akiwa humo ndani, angalau uwepo wake ulikuwa unaleta urari wa nguvu (balance of power) uliowazuia mafisi wengine kumeza kila kitu. Sasa usukani umeachwa mikononi mwa kundi moja linalokwenda kuitafuna nchi hadi mfupa wa mwisho bila hofu ya kukosolewa ndani ya vikao vikuu.
  1. Mbinu ya Kupoteza Maboya (Political Diversion)
    Katika sayansi ya siasa, hii inaitwa 'Agenda-Setting' au 'Smoke Screen'. Serikali au chama tawala kikiwa kwenye shinikizo kubwa—iwe ni kubanwa kwa misaada kutoka kwa wafadhili wa nje au mijadala mizito ya kijamii—hutengeneza "tamthilia ya kisiasa" ili kuhamisha akili za wananchi.
  • Ghafla bin vuu, nchi nzima imesahau ajenda za msingi. Kesi ya uhaini ya Tundu Lissu iliyokuwa inafuatiliwa kwa ukaribu na kutikisa nchi sasa hivi imepoteza mshiko kwenye masikio ya watu.
  • Wananchi wameingizwa kwenye mtego wa kujadili nani atateuliwa kuwa Makamu wa Rais mpya (huku tetesi zikimtaja Ridhiwani Kikwete), wakisahau kabisa kufuatilia madudu yanayoendelea nyuma ya pazia, ubadhirifu wa fedha za umma, na utoroshaji wa rasilimali. Tumekuwa kama nyumbu kweli!
  1. Kipimo cha Ushujaa ni Katiba Mpya, Sio Kujiuzulu
    Ninamalizia kwa kusisitiza hoja ya mwisho ya mtoa mada. Nchimbi asisifiwe kwa sababu tu ameweka kalamu chini na kukimbilia kwenye mafao ya kifahari. Ushujaa wake wa kweli utapimwa sasa akiwa nje ya madaraka.
  • Kama kweli alikuwa anapigania maslahi ya umma na Katiba Mpya, aendelee kusimamai msimamo huo sasa hivi akiwa raia wa kawaida bila uoga, kama alivyofanya Humphrey Polepole hadi mwisho wa maisha yake.
  • Kama atakaa kimya na kuanza kufurahia hayo mamilioni ya pensheni huku nchi ikizama, basi thibitisho litakuwa wazi kuwa alikuwa mbinafsi aliyetanguliza tumbo lake na uoga wake mbele.
Mtoa mada tpaul ametufumbua macho na kutupa uchambuzi thabiti. Huu ni uhaini wa kiuchumi na kisiasa unaotugharimu sisi raia wa kawaida, na hatuna sababu yoyote ya kushangilia tamthilia hii ya CCM.
Nawasilisha hoja kuunga mkono!
Asante kwa kunielewa na kuwafafanulia zaidi wadau wengine mkuu. Ulichoandika hapa ndicho nilichomaanisha šŸ’Æ%. Tatizo la nchi hii nyumbu ni wengi kuliko kawaida. Na wametengenezwa na CCM kwa makusudi ili waendelee kuitafuna nchi bila kuhojiwa.
 
Shukrani sana mkuu tpaul, tuko pamoja kabisa na nafurahi kuwa tulikuwa ukurasa mmoja katika kuuchambua huu mchezo wa kuigiza.
Ukiangalia kwa jicho la ziada, hili tatizo la kutengeneza "nyumbu" nchini lina mizizi mirefu sana ya kimfumo na kiutawala. Nilikua natafakari kwa kina na kujiuliza swali moja la msingi sana: Je, unadhani ni kwa nini huko nyuma wamiliki wa watumwa (Slave owners) walikuwa wakikataa kabisa na kupiga marufuku kuwasomesha slaves wao?
Jibu liko wazi kabisa; hii ndiyo tabia thabiti inayotumiwa na serikali nyingi duniani, ikiwemo hii yetu, kuwanyima watu uwezo wa kuwa na fikra tunduizi (critical thinkers). Ukiwapa watu maarifa na elimu bora, unawapa uwezo wa kuhoji minyororo yao na hatimaye kujikomboa. Ndio maana mfumo wetu wa elimu unazidi kushushwa hadhi kwa makusudi kabisa.
Sasa hivi, mbinu hii imepinduliwa kisasa kupitia hili ombwe la "machawa." Kuibuka na kupewa nguvu kwa watu kama kina Dotto Magari, ambao wamefikia hatua ya kuwatukana na kuwadunisha wasomi hadharani, sio jambo la bahati mbaya. Ni mkakati ulioratibiwa kwa makusudi kabisa ili watoto wetu na wajukuu zetu waone umuhimu wa kuwa machawa kuliko kuwa wasomi. Mfumo unataka jamii iamini kuwa kupiga vigelegele na kusifu ndio sifa ya kufanikiwa, huku kusoma na kuhoji kukiacha mtu kwenye umaskini na dharau.
Tukiruhusu mkakati huu wa CCM utawale akili za vizazi vyetu, tutakuwa tumebariki utumwa mpya wa kisaikolojia na kiuchumi unaokwenda kuitafuna nchi hii kwa miaka mingi ijayo bila mtu wa kupaza sauti.
 
Upo sahihi kabisa mkuu. Leo nilikuwa nafanya doria kwenye mitandao ya kijamii, nikakutana na andiko hili hapa mambalo linasadifu kabisa hiki unachikisema kuhusu elimu yetu inavyodunishwa na CCM kwa makusudi ili kutengeneza vilaza wasiokuwa na uthubutu wala maarifa ya kuhoji chochote kutoka kwa hawa wakoloni weusi:
1000362070.jpg
 
View attachment 3658166
duh
 
Fast forward—nadhani sasa umeshajionea mwenyewe jinsi mambo yanavyofanyika kwenye nchi hii. Katiba yetu ya sasa imejenga mfumo wa kututengenezea mungumtu, sio Rais wa kawaida wa nchi.
Katika suala la Nchimbi kujiuzulu kuna matatizo mengi sana, ya utamaduni, ya siasa zetu, na kadhalika.

Lakini hakuna tatizo la moja kwa moja la kikatiba.

Kwa sababu kama Nchimbi kakubali kujiuzulu mwenyewe, tatizo hapo ni Nchimbi kukubali kujiuzulu, si katiba.

Hakuna sehemu ambapo katiba inampa Rais nguvu za kumuondoa Makamu wa Rais useme kifungu hiki cha katiba ndicho kimempa nguvu Rais kumtoa Makamu wa Rais.

Tuna tatizo la viongozi wasioweza kusimamia principles. Nchimbi kashindwa kukataa kujiuzulu. Hilo ni tatizo la principle za mtu si tatizo la katiba.

Pengine tuna tatizo Watanzania hawakuweza kujitokeza kumuunga mkono Nchimbi. Pengine hawakumuamininsana, nchi ngumu hii hata amana tu ni shida. CCM yeyote kuaminika ni shida sana.

Nchimbi kamuahidi Samia kuwa wakati wowote Samia asipomtaka atajiuzulu.

Hili si tatizo la katiba, jili ni tatizo la utamaduni. Too much reverence to the president.

Hilo si tatizo la katiba, hili ni tatizo la Nchimbi kukosa principle, kukosa kusimamia principle kuwa yeye kachaguliwa na Watanzania (let's say kachaguliwa for arguments sake), hawajibiki kwa Samia anawajibika kwa Watanzania waliomchagua yeye na Samia.

Ndiyo katiba inampa nguvu kubwa sana Rais kiujumla, lakini specigically katika hili kuna matatizo mengi ya kiutamaduni na kisiasa kupita katiba.

Hakuna kifungu cha katiba kinachompa Samia nguvu za kumuondoa Nchimbi.
 
I don’t think you fully appreciate the havoc that the current constitution has wreaked in this country.

In Tanzania, the ruling party, Chama Cha Mapinduzi (CCM), holds immense institutional power. If a VP loses the backing of the party's Central Committee or falls out with the President (who doubles as the CCM Party Chair), his or her position becomes completely untenable—(s)he is cut off from the party apparatus, his or her political base is dismantled and (s)he faces total isolation within the cabinet.

Rather than enduring a long, embarrassing public ousting or triggering a constitutional crisis, the VP is quietly given an ultimatum: resign gracefully or face total political destruction.

Unadhani recent verbal attacks against Nchimbi (zilizofanywa na Simai na mazafakas wenzake) zilikuwa za kujituma wenyewe? Kwenye hii nchi, the president isn’t your everyday president!
 
I do appreciate very much the constitutional problems.

But not everything is due to the constitutional problems.

Some of these problems are due to sheer cowardice.

Cowardice is not a constitutional problem.

Sasa Nchimbi afanyiwe "total political destruction" gani zaidi ya hii?

Mbona Tundu Lissu kafungwa jela, lakini kakataa ku compromise kwenye principles zake?

Tatizo Nchimbi hasimamii principle, anasimamia convenience na self preservation.

Alimjambisha Samia kindezi kama Polepole tu, akajibiwa kibabe kwa kuvuliwa uanachama.

Nchimbi could have chosen to battle it out with Samia. After all, his position does not even depend on him being a CCM member.

Currently he is the VP, without being a CCM member.

Tanzania Rais ana nguvu nyingi kaoewa na katiba, hilo ni tatizo kubwa. Nalijua. Wala sitaki kulidogosha.

Lakini tatizo kubwa zaidi wala si nguvu Rais anazopewa na katiba, ni nguvu Rais anazopewa na watu tu ambazo hata kikatiba hazipo.

Nchimbi kamuahidi Samia kwamba siku yoyote Samia atakapomchoka, Nchimbi ataondoka katika nafasi yake.

Hilo si tatizo la katiba, hilo ni tatizo la Nchimbi kuahidi vitu ambavyo Rais hata hana nguvu hizo kikatiba. Tatizo la uchawa uliopitiliza, tatizo la fake modesty, tatizo la Nchimbi kutowajibika kwa watu waliompigia kura (in theory) na kutaka kuwajibika kwa Rais.

Hapo tatizo si katiba, kikatiba Rais hana nguvu ya kumuondoa Makamu wa Rais.

Hiki ni tatizo la utamaduni wa kumpa nguvu Rais, nguvu ambazo hazipo kikatiba.

Huelewi wapi hapo?
 
Unasema, ā€œCurrently he is the VP, without being a CCM memberā€. You ain’t serious! He is VP in name only. Sasa hivi hata mtendaji wa kata yangu is more powerful than Nchimbi.

Usichokielewa ni kwamba Katiba ya sasa imempa Rais nguvu ya kutengeneza mfumo kwa namna anayotaka mwenyewe. Kwa mfano, hakuna mwanachama wa CCM anayeweza kuwa mbunge kama Rais (ambaye ni mwenyekiti wa CCM) hamtaki. Kwa maneno mengine, caucus ya wabunge wa CCM ni genge la loyalists wa Rais. So, amini usiamini, fazafaka angetaka Nchimbi awe impeached na Bunge, angekuwa impeached asubuhi na mapema!

Vivyo hivyo kwenye Mhimili wa Mahakama. Rais anajaza allies wake. Kuna mazafakas wengi kwenye Mhimili wa Mahakama ambao ni TISS operatives.

In substance, Tanzania is an autocracy!
 
Kawa VP in name only kwa sababu kajiuzulu, si kwa sababu Samia ana nguvu ya kikatiba kumtoa.

Mbona Samia alikuwa hapendwi na Magufuli, katengwa, kafanyiwa visa kibao, na hakujiuzulu, kakomaa mpaka Magufuli kafariki, Samia akachukua urais?

Mbona Magufuli na ubabe wake wote hakuweza kumtoa Makamu wa Rais ambaye hakumtaka?

Mambo mengine mnampa Samia nguvu ambazo hana kikatiba, mnampa wenyewe, halafu mnailaumu katiba.

Katiba imempa nguvu sana Rais.

Lakini katiba haijampa Rais nguvu ya kumtoa Makamu wa Rais.

Yani hata kama kqeli Raia ana ngivu sana, haitakiwi Makamu wa Rais ajiuzulu kiboya tu. Inatakiwa akatae, awe imoeachwd bungwni, tuone nani anam support na nani anamtosa, tujue wapi panavuja na wapi pako imara.

Kujiuzulu kindezi kunaondoa process yote ya kujua mengi zaidi. Nchimbi kakosa hata nafasi ya kusema mengi sana ambayo alitakiwa kusema yawekwe kwenye Hansard.

Na pengine kakataa kusema hivyo kakimbilia kujiuzulu kwa sababu na yeye anajijua si msafi hivyo, ana madudu yake.

Kwa hivyo kukubali kirahisi hoja ya "Rais ana nguvu sana" actually kunawapunja wananchi kujua nchi yao inavyoendeshwa, kuna ugomvi gani, wanakosa kujua mengi sana.

Hapa kuna matatizo ya uchawa tu, uchawa si katiba.

Picha linaanza, Nchimbi kabla ya kuchaguliwa anaahidi aiku yoyote Samia asipomtaka atajiuzulu.

Hili ni tatizo. La Nchimbi. Si la katiba.

Hakuna kifungu cha katiba kinachompa Rais nguvu ya kumuondoa Makamu wa Rais.

Huelewi wapi?

Nchimbi kama anaamini anachosimamia alitakiwa kukataa kujiuzulu tuone anafukuzwa kikatiba.

Lakini hana ushujaa huo, hana principle kihivyo, kaogopa.

Hapa tatizo si katiba, tatizo ni Nchimbi kukosa principle, kukosa ushujaa, kuwa muoga.

Msipende kujificha kwenye chaka la katiba kwenye mambo ambayo hata kikatiba hayapo na mnampa Samia nguvu ambazo hata kikatiba hazipo wenyewe.
 
Sijui hivi vitu vingine nani amekudanganya. Kwenye nchi hii, hakuna VP anayeshindikana kung’oka. Akili za wale waliomvua Nchimbi uanachama hazina tofauti na za wale walioko Bungeni. Lile Bunge, kimsingi, ni extension ya Mhimili wa Executive. Watu hawaendi Bungeni kwa kupendwa tu na wapigakura wao! Where’s Mpina? Where’s Mwalimu? Where’s Makamba? Why is Tulia no longer Speaker? Hawa wote ni wahanga wa mfumo hatari uliowezeshwa na Katiba ya sasa!

Wewe unataka kuona Ibara kwenye Katiba inayosema Rais ana authority ya kumuondoa VP, lakini unasahau kwamba Katiba imempa Rais nguvu ya kutengeneza mfumo unaowezesha matamanio yake kutimia hata kama Rais hana mamlaka ya moja kwa moja.
 
Back
Top Bottom