Teknolojia ni Yetu sote
JF-Expert Member
- Apr 28, 2020
- 1,386
- 2,833
Hivi utajisikiaje ukiwa umepanda Ndege halafu unasimama kama kwenye mwendokasi freshi sio!!
Shirika moja nchini Ireland linaitwa Rynair limeleta safari za ndege za gharama nafuu kwa kuweza kupunguza nauli za ndege na kuondoa viti kwenye baadhi ya safari zake.
Mpango huu ni kuwezesha abiria kuweza kusafiri kupitia kusimama wakati wote wa safari,
kwa kutumia mikanda salama maalum ambayo imeambatanishwa kwenye Kuta za ndege. Teknolojia hii kwa sasa iko kwenye hatua za Majaribio.
Kwa mujibu wa taarifa zilizosambaa mtandaoni mfano wa safari nauli yake inaweza kuwa Euro ๐ถ 10 ambapo sawa na Tanzania shilingi elfu thelathini ambapo safari itakua kutoka Tanzania kwenda ufaransa umbali wake ni masaa 9 angani.
Lengo ni kuwezesha watu wa kipato cha chini kuweza kusafiri kutoka nchi moja kwenda nyingine bila shida yoyote. Unasemaje kuhusu Teknolojia je iletwe au lah tuachie maoni yako?