StudentTeacher
JF-Expert Member
- Jan 30, 2019
- 7,043
- 8,478
Hapo sawa!Muheshimiwa,nimeandika kwa ufupi tu.Ila,we had a great lesson together.Alinielewa.
Hapo sawa!Muheshimiwa,nimeandika kwa ufupi tu.Ila,we had a great lesson together.Alinielewa.
Shida inakuja huyo bonge nyanya hataki kuitwa bonge nyanya 😀Sasa mtu Kama chivayo unaweza kumwitaje zaidi ya bonge Nyanya SI ndio alivyo
Wakati mwingine upekee wa mtu ndio unakua utambulisho wake mfano toll, short , bonge , ras, kibonge , cheusi , zeruzeru , chiba, kilaza ipo hivyo
Hii nchi yetu ni shida sana mkuuSalama wakuu?
Kuna hii kitu inaitwa bullying ama Kwa lugha ya kiswahili tuite labda uonevu.hii kitu ni common sana na inachukuliwa kawaida na jamii yetu kiasi inaleta madhara lakini hatuyaoni na hata tukiyaona tunayafumbia macho na kuona ni kawaida.
Kuna bullying za aina tofauti kama
• Kimwili: Kupigwa, kusukumwa ovyo, au kuumizwa.
• Kinywa / Maneno: Kuitwa majina yasiyofaa, kutukanwa, au kutishwa.
• Kihisia na Kisaikolojia: Kutengwa, kudhalilishwa nk
Ningesema ni tatizo la hivi karibuNi lakini nikikumbuka katika ukuaji wangu na matukio naona ni kitu haakijaanza Leo na akili zetu zimeadapt kwamba ni kawaida Haina shida.
Kuanzia wanawake,wanaume,vijana,watoto na wazee.
Sio shuleni,sio vyuoni,sio ma hospital hasa za serikalini,viongozi wa serikali,viongozi wa vyama vya siasa,mbaya zaidi mtaani.
Ni kawaida kukuta watu wanatungana majina Kwa muonekano, maumbile ama changamoto,ama tukio
Unakuta mtu mweusi anaitwa cheusi Mangala,mfupi wanamuita kijeba,kidingi..
Mpaka wanaume weupe wanakuwa bullied na wanaume wenzao wakiwaona kama wanawake,mtu mrefu anaitwa ngongoti
Mtu aliezaliwa na changamoto ya miguu kupishana urefu wanamuita chiba,mtu mwenye akili ziko slow kuadapt wanamuita zezeta.mwenye kushindwa kuelewa jambo na kulifanya Kwa ufanisi anaitwa kilaza nk
Na mengine mengi sana.
imekuwa common sana.hali inayopelekea wengine kushindwa kustahimili,Kuna wanaojidhuru,Kuna wanaathirika kisaikolojia na kuwa na msongo wa mawazo,na wengine wanajichukia na kukosa kujiamini haswa Kwa watoto na ma teenager ambao bado hawajakomaa kisaikolojia na kiakili kukabiliana na mengi.
Wakati nchi za ughaibuni wamepitisha kama ni kosa kumbully mwenzio.Mfano nchini Korea ikiwa mwanafunzi atambully mwenzie basi atakuwa suspended.
Sawa najua Africa sio kwaajili ya mtu dhaifu,tuna namna yetu ya kurespond Kwa bullies aina zote,lakini ingependeza kama tulngelichukulia Kwa uzito kama lenye madhara Kwa ustawi wa watu na jamii Kwa ujumla.tunaweza kuona ni kawaida ila ni ajabu na aibu.
Juzi juzi tu hapa Kuna cashier wa supermarket kapigana na mteja baada ya mteja kudai kamuita "shangingi"
Mashindano yanaoyoendelea ya Miss grand international waTanzania wameingia kwenye shutuma za bullying Kwa kuachia comments zinazosanifu washiriki wengine,Yale wanayoandika nchi nyingine Wana translate wanasoma.imefikia wanashangaa.
Yangu ni hayo tu.
Kazi sana...Media pia zina bulliying sana, kuna siku napita pita huko mtandaoni nakuta clip ya Crown Media wamemualika kwenye kipindi huyo mgeni sijui anaitwa somo sijui kungwi, huyo mgeni bila aibu anasema" mtaachwa sana kwa kusingizia mishono" yaani anawasema vibaya wamama waliojifungua kwa mishono kisa wanashindwa kufanya majukumu yao kama wanawake wenginw. Cha kushangaza mtangazaji nae ni mwanamke na yeye anasupport huyo somo anavyowasimanga watu wanaopitia maumivu ya mishono baada ya kujifungua kwa upasuaji.
majina ya kuitana mkuu hayo ya kutunga mengine yamekaa kidhalilishaji..Sasa mtu Kama chivayo unaweza kumwitaje zaidi ya bonge Nyanya SI ndio alivyo
Wakati mwingine upekee wa mtu ndio unakua utambulisho wake mfano toll, short , bonge , ras, kibonge , cheusi , zeruzeru , chiba, kilaza ipo hivyo
Itachukuwa muda sana.Kwa sababu Sisi ni Underdeveloped Kantri. Siku tukitoka kwenye umaskini huu wa mchongo,watu wakiwa wanakula wanashiba na kusaza. Wanapata elimu bora,matibabu yaliyonyooka ndio siku tutakapoanza kufikiria sio tu kuzitungia sheria kali tabia mbovu kama hizo za bullying bali hata haki za wanyama and the like. Kwa sasa bado sana!.
Tukijite kwenye Katiba mpya kwanza!
Nimekuelewa mkuuBullying ni SILIKA ya viumbe vyote vilivyo hai. Ni namna mojawapo ya kuhakikisha kiumbe kinatambulika miongoni mwa viumbe vingine vilivyopo mahalia. Utasikia kwenye mimea (Plant kingdom)majina kama magugu, invasive species n.k. Hiyo ni mimea inayokaba nafasi au inayovamia maeneo kwa kuishinda ile iliyopo.
Kwa wanyama utasikia kitu kinaitwa vices e.g. kuku kuna "pecking" habits, kwa ng'ombe utasikia "mounting habits" n.k.
Kwa binadamu ndo hiyo inaitwa bullying. Ni kama aina ya Tabia mbovu au mbaya isiyokubalika na jamii au kundi lililopo mahali kwa wakati maalum. e.g. Huko mashuleni esp.boarding sec. schools wavulana wanaoingia kuanza F-one ni lazima wakumbane na jambo hilo kutoka kwa form 2 - hata waalimu wapigie kelele kiasi gani, wakemee haisaidii.
Huko maofisini nako sio haba. Waajiriwa wapya wakifika Ofisini kuripoti kwa mara ya kwanza wakisha ripoti kwa mkuu wa Idara na wakawa-Introduced kwa staff member wengine kinachofuata ni Utelekezwaji. Mtu anaachwa hapo ajijue mwenyewe - atapata wapi nyumba ya kuishi/kulala,chakula n.k. nk.
Matendo au Hali ya kuwa Bullyed around yanajitokeza katika nyanja nyingi sio tu unyanyasaji, udhalilishaji au kufanyiwa vitendo vya kifedhuli, kejeli, kero za kulazimisha n.k. n.k....
Solution: Kama unaweza ni kupuuzia au kama ni lazima kutoa "warning" toa warning ya kiwango cha lami ili iwe ni fundisho na kwa wengine. Usimchekee mtu anayekufanyia bullying kwa kudhamiria. Make or change his/her Perpendicularity into Horizontality absolutely.
Bullying zingine zina madhara makubwa sana. Usikubali kuwa mnyonge.
Hapo kwenye taarab umepatia mkuu,nikiwa mdogo taarab zilinifanya nijiulize watu wa pwani wanaishije maana sio kwa maneno yale. Eti mtu anajisifu kuchukua mume wa mtu😂😂😂Kazi sana...
Hivi unasikia wanavyoimba kwenye taarabu tangu miaka na miaka haswa wanawake?
Kawaida kwao..bado ulieibiwa mume hujaitwa majina kibao ikiwemo sanamu la Michelin😄Hapo kwenye taarab umepatia mkuu,nikiwa mdogo taarab zilinifanya nijiulize watu wa pwani wanaishije maana sio kwa maneno yale. Eti mtu anajisifu kuchukua mume wa mtu😂😂😂
Hebu elezeaBullying ya ukweli ni ile inayofanywa na chama dola, hayo mengine ni rasharsha/ kudeka
Tuko pamoja sana.Nimekuelewa mkuu
Hapa ndiyo kabisa, hapatoshiHata humu jamiiforums bullying ipo sana...
Jeshi la watu wawili tu, lakini wanapeleka moto siyo kitoto🤣🤣🤣bullying wanazofanya Tlaatlaah na Lucas Mwashambwa kwenye Jukwaa la Siasa sio poa kabisa
Hili silifahamuNipo hapa kupata ilmu,Hivi mgongo wazi ni kama alivyo petro magoti au ni kitu kingine tofauti?
Mgongo wazi yaani mgongo unakuwa na kama kishimo kabisa, hicho kishimo huwezi kukiona labda avue nguo. Wanaozaliwa na huo ugonjwa sidhani kama huwa wanatoboa kufika ukubwani. Mgongo wazi na kichwa kikubwa ni ndugu maana vyote chanzo ni mama kukosa folic acid akiwa mjamzito.Nipo hapa kupata ilmu,Hivi mgongo wazi ni kama alivyo petro magoti au ni kitu kingine tofauti?
Somo hili liwafikie walimu,Tukiwa watoto tulipitia hayo.tunaweza epushia watoto wetu pia.
Wengine hawana nguvu ya kustahimili.
Nje wakimbully,wewe ndani mpe moyo na hamasa.
Ikiwa tu jamii itashindwa kubadilika
Tatizo hili linaweza kuisha kisheria.Tatizo likishaota miziz linachukua muda na juhudi sana kuling'oa.Nina Imani i
po siku tutaachana na haya.